LGE2024 Shangwe Ayo (ACT Wazalendo): Tunakwenda kumuondoa shetani Uchaguzi wa Serikali za Mitaa

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

Cute Wife

JF-Expert Member
Nov 17, 2023
1,292
3,593
Wakuu,



Naibu Katibu wa Idara ya Habari, Uenezi, na Mahusiano ya Umma wa chama cha ACT Wazalendo taifa, Shangwe Ayo ametaka sheria za uchaguzi za serikali za mitaa zifuatwe ili wananchi wa watimize azma yao ya kupata viongozi bora watakaowatumikia kwa kipindi cha miaka mitano ijayo.

Shangwe ametoa wito huo akizungumza na wananchi wa mtaa wa Tembo Nyambwela, kata ya Tandika, jimbo la Temeke mkoani Dar es Salaam Novemba 24, 2024.

Kupata taarifa na matukio ya kimkoa kuhusu Uchaguzi Serikali za Mitaa ingia hapa: LGE2024 - Special Thread: Orodha ya Mijadala ya Mikoa yote Tanzania Bara inayoshiriki katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

“Siku ya uchaguzi tunawatangazia vita, mlipolala tunaamkia, shuka mlilojifunikia ndilo sisi tumelivua jana yake, mliponyanyua mguu sisi ndipo tumeweka. Sasa kama hamtaki haya kutokea fuateni sharia”, amesema Shangwe.

Kwa upande wake mgombea uenyekiti wa mtaa wa Tembo Nyambwela Mussa Mussa amesema amekuwa sehemu ya maendeleo ya mtaa huo kabla ya miaka mitano iliyopita kwa kuwezesha kujengwa kwa ofisi katika mtaa huo

Hata hivyo amekilaumu Chama Cha Mapinduzi kilichokuwa kikitawala mtaa huo kwa kipindi cha miaka mitano kwa kushindwa kuitunza ofisi hiyo na kuwaomba wananchi wa Tembo kumpigia kura ili aweze kuleta maendeleo makubwa kwao.
 
.How? Kwa mbinu ipi, ikiwa uchaguzi tayari umevhezewa?

Hivi wanasiasa mnapoongea huwa wanakiwa wamevuta mibangi?
 
Back
Top Bottom