SautiYaMnyonge
JF-Expert Member
- May 13, 2018
- 439
- 742
Na Mwandishi Wetu,
Mikocheni-Dar es Salaam.
Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa itikadi na Uenezi Ndg. Shaka Hamdu Shaka usiku wa tarehe 01/07/2021 ameungana na watanzania wengi ambao ni wana michezo katika hafla fupi ya uzinduzi wa mashindano ya mpira wa miguu maarufu kama NDONDO CUP hatua ya 32 bora, utambulisho wa jezi zitakazotumika kutoka kampuni ya Umbro pamoja na michuano ya wanawake katika michuano hiyo 'Malkia Ndondo Cup'. Michuano hii hufanyika kila mwaka chini ya Clouds Media group na chama cha soka mkoa wa Dar es salaam (DRFA).
Uzinduzi huo pia ulihudhuriwa na wabunge mbalimbali, pia wanasiasa kutoka vyama mbalimbali.
"Kati ya michuano ambayo imekuwa ikiibua vipaji vya wachezaji kadhaa na kufanikiwa kucheza soka ndani na nje ya Nchi ni hii Ndondo CUP wakati umefika sasa ubunifu huu kuwa wa Kitaifa." Alisema Shaka H Shaka.
Lakini pia Shaka ametumia Jukwaa hilo kufikisha salamu za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. SAMIA SULUHU HASSAN ya kwamba anathamini na kutambua mchango wa Clouds Media na wadau wengine Katika kuwaunganisha Vijana kupitia mashindano hayo ya NDONDO CUP.
#KaziIendelee
#TanzaniaNiSisi