SI KWELI Shadrack Chaula aliyechoma picha ya Rais Samia ameripotiwa kufariki, Agosti 15, 2024

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Source #1
View Source #1
Inadaiwa kuwa kijana aliyefungwa jela kwa kuchoma picha ya Rais Samia kisha wananchi wakachanga kumtoa amefariki dunia.

Kijana huyu amekuwa haonekani kwa siku nyingi sasa baada ya kuchukuliwa na watu wasiojulikana.

1000111299.jpg
 
Tunachokijua
Ufuatiliaji wa kimtandao wa JamiiCheck umebaini taarifa hiyo inayosambaa ni ya kutengeneza na haijawahi kuwekwa kweye kurasa rasmi za Millard Ayo kama ambavyo inasambaa kwa kutumia jina lake.

Aidha JamiiCheck pia imewasiliana na Baba wa Shadrack anayejulikana kwa jina la Mzee Chaula ambaye amesema tangu kupotea kwa mtoto wake mpaka sasa hakuna taarifa yoyote zaidi ya ile ya vyombo vya usalama kuendelea kufanya uchunguzi. Akiifafanulia JamiiCheck Mzee huyo amesema

"Hakuna kinachoendelea, polisi bado wanaendelea kufanya uchunguzi na hakuna taarifa yoyote ambayo nimeipata. Leo Agosti 15, 2024 nimewasiliana na Afisa Upelelezi Rungwe naye kasema bado uchunguzi unaweza kuendelea naye"

Naye, Mweyekiti wa Serikali ya Mtaa kijiji cha Nzunda amesema "Sisi kama kijiji tunaendelea kupeana taarifa kwamba popote watakapomuona basi watoe taarifa. Kama kijana angepotelea ndani ya kijiji hiki angeonekana lakini kwakuwa alichukuliwa na kutolewa nje ya kijiji ndiyo maana bado hatujafanikiwa kumpata"
Hiyo habari haipo kwenye ukurasa rasmi wa Millard Ayo, kwa hiyo chanzo chake hakiaminiki. Leteni habari ya kuaminika ili tuwe tofauti na Facebook

JamiiForums, Home of Great Thinkers​
 
Hiyo habari haipo kwenye ukurasa rasmi wa Millard Ayo, kwa hiyo chanzo chake hakiaminiki. Leteni habari ya kuaminika ili tuwe tofauti na Facebook

JamiiForums, Home of Great Thinkers​
Kwahiyo millard ayo ndiye anayetoa habari za kuaminika!
 
Kwenye moja ya posts X nimeona hiyo picha ikiwa juu, kisha chini yake kukiwa na ujumbe huu:

"Najua sana habari hii si kweli.
Nimeweka makusudi kwa malengo mazuri, hata kama ni kinyume na sheria, niko tayari.
Huu upuuzi wa kuteka na kupoteza watu unapaswa kupingwa kwa njia yoyote inayowezekana, lkn isiyoumiza wengine. Kukaa kimya ni sawa na kujisalimisha kwa watekaji."
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom