Serikali yatenga Shilingi Bilioni 34 kujenga Makumbusho ya Marais Dodoma

Waufukweni

JF-Expert Member
May 16, 2024
724
1,877
Serikali imetenga Shilingi bilioni 34 kwa ajili ya utekelezaji wa mradi wa Makumbusho ya Marais nchini, unaotarajiwa kujengwa katika eneo la Mtumba, Dodoma. Mradi huo utatekelezwa kwenye eneo lenye ukubwa wa ekari 50 na unalenga kuhifadhi kumbukumbu za viongozi wakuu wa nchi pamoja na historia ya taifa.

Akizindua kitabu cha aliyekuwa Waziri Mkuu wa Tatu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Edward Moringe Sokoine (MAISHA NA UONGOZI WAKE) JNICC, Jijini Dar es Salaam Rais Samia amesema kwa kuanza mwaka huu zimetengwa zaidi ya Sh. Bilioni 1 ili kuanza utekelezaji.

Soma:
=> Bashungwa: Makandarasi wazawa kupewa miradi hadi yenye thamani ya bilioni 50
=> Dar: Shilingi bilioni 18 zatengwa kwa ajili ya kuimarisha upatikanaji wa maji safi Msumi iliyopo kata ya Mbezi
=> Waziri Mkuu Majaliwa: Serikali yatenga sh. Bilioni 787 za mikopo ya wanafunzi
 
Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan amesema Serikali imetenga Tsh. bilioni 34 kwa ajili ya mradi wa makumbusho ya Marais ambao utajengwa Dodoma ili kuweka historia na kumbukumbu za Viongozi hao.

Rais Samia amesema hayo Jijini Dar es salaam leo September 30,2024 wakati akizindua kitabu cha Sokoine (Maisha na Uongozi wake).

"Nataka nizungumzie pendekezo lililotolewa na Balozi Sokoine kwamba kuwe na kituo mahususi cha kuweka historia na kumbukumbu za Viongozi, nataka nitoe taarifa kwamba pendekezo hili limeanza kufanyiwa kazi, kuna mradi wa makumbusho ya Marais, mradi huu ni mradi namba 5221 eneo liko Mumba na tumetenga Tsh. bilioni 34 kwa ajili ya mradi huu na mwaka huu tumeanza kutenga bajeti ndogo kama bilioni 1 na kitu na eneo lile lina ukubwa wa ekari 50 pale Dodoma kwahiyo hili tunalifanyia kazi" — Rais Samia.

Chanzo; Millard Ayo
 
Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan amesema Serikali imetenga Tsh. bilioni 34 kwa ajili ya mradi wa makumbusho ya Marais ambao utajengwa Dodoma ili kuweka historia na kumbukumbu za Viongozi hao.

Rais Samia amesema hayo Jijini Dar es salaam leo September 30,2024 wakati akizindua kitabu cha Sokoine (Maisha na Uongozi wake).

"Nataka nizungumzie pendekezo lililotolewa na Balozi Sokoine kwamba kuwe na kituo mahususi cha kuweka historia na kumbukumbu za Viongozi, nataka nitoe taarifa kwamba pendekezo hili limeanza kufanyiwa kazi, kuna mradi wa makumbusho ya Marais, mradi huu ni mradi namba 5221 eneo liko Mumba na tumetenga Tsh. bilioni 34 kwa ajili ya mradi huu na mwaka huu tumeanza kutenga bajeti ndogo kama bilioni 1 na kitu na eneo lile lina ukubwa wa ekari 50 pale Dodoma kwahiyo hili tunalifanyia kazi" — Rais Samia.​

Chanzo; Millard Ayo
Hiyo ni kupoteza raslimali za nchi yetu pasipo sababu ya.msingi

Hivi wawezaje katika nchi masikini kama yetu, kuamua kutumia shilingi bilioni 34 Kwa ajili tu ya makumbusho ya viongozi wetu, wakati mahitaji ya msingi ya watanzania hamjatimiza??

Kwenye nchi ambayo watanzania walio wengi, hawana hata vibanda vya chumba kimoja Cha kujisitiri, hayo ni matumizi ya hovyo kabisa ya Kodi zetu!😳
 
Hizo hela afadhali angezielekeza kwenye ujenzi wa shule na kuweka mazingira mazuri ya walimu!
Hii nchi bado ujingaa ni mwingi sana.
Ujenzi wa shule ingekuwa uamuzi sahihi.

Au zingejengwa zahanati maana hii nchi mikoani huko watu wanaenda umbali mrefu sana kufuata huduma za matibabu.

Maana sioni hayo majengo ya kuwakumbuka maraisi kama yataleta manufaa kwenye jamii.
 
Hii nchi hela zinachezewa sana aisee 34B kwa ajili ya makumbusho ya Marais ya nini, impact yake ni nini kwa mwananchi wa kawaida!?

Huo mzigo kama ungewekwa ili kukopesha vijana ni maisha ya vijana kiasi gani yangebadilika ambao sasa hivi wanastruggle na ajira na mitaji hawana na wala hawakopesheki na banks
 
Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan amesema Serikali imetenga Tsh. bilioni 34 kwa ajili ya mradi wa makumbusho ya Marais ambao utajengwa Dodoma ili kuweka historia na kumbukumbu za Viongozi hao.

Rais Samia amesema hayo Jijini Dar es salaam leo September 30,2024 wakati akizindua kitabu cha Sokoine (Maisha na Uongozi wake).

"Nataka nizungumzie pendekezo lililotolewa na Balozi Sokoine kwamba kuwe na kituo mahususi cha kuweka historia na kumbukumbu za Viongozi, nataka nitoe taarifa kwamba pendekezo hili limeanza kufanyiwa kazi, kuna mradi wa makumbusho ya Marais, mradi huu ni mradi namba 5221 eneo liko Mumba na tumetenga Tsh. bilioni 34 kwa ajili ya mradi huu na mwaka huu tumeanza kutenga bajeti ndogo kama bilioni 1 na kitu na eneo lile lina ukubwa wa ekari 50 pale Dodoma kwahiyo hili tunalifanyia kazi" — Rais Samia.​

Chanzo; Millard Ayo
Hiki nacho ni kipaumbele cha serikali? Mimi nilidhani mambo yanayoweza kusubiri inawezekana na tukaanza na pressing needs? Sielewi kabisa!
 
Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan amesema Serikali imetenga Tsh. bilioni 34 kwa ajili ya mradi wa makumbusho ya Marais ambao utajengwa Dodoma ili kuweka historia na kumbukumbu za Viongozi hao.

Rais Samia amesema hayo Jijini Dar es salaam leo September 30,2024 wakati akizindua kitabu cha Sokoine (Maisha na Uongozi wake).

"Nataka nizungumzie pendekezo lililotolewa na Balozi Sokoine kwamba kuwe na kituo mahususi cha kuweka historia na kumbukumbu za Viongozi, nataka nitoe taarifa kwamba pendekezo hili limeanza kufanyiwa kazi, kuna mradi wa makumbusho ya Marais, mradi huu ni mradi namba 5221 eneo liko Mumba na tumetenga Tsh. bilioni 34 kwa ajili ya mradi huu na mwaka huu tumeanza kutenga bajeti ndogo kama bilioni 1 na kitu na eneo lile lina ukubwa wa ekari 50 pale Dodoma kwahiyo hili tunalifanyia kazi" — Rais Samia.​

Chanzo; Millard Ayo
Hivi hiyo pesa sawa na barabara ya rami kilomita ngapi?aliyetuloga wafrika alikufa,
yaani viongozi wakiwa na maisha mazuri wanajua watanzania wote tunamaisha mazuri?
Kwanza kila siku wanawaza jinsi ya kutuongezea kodi
 
Hiyo ni kupoteza raslimali za nchi yetu pasipo sababu ya.msingi

Hivi wawezaje katika nchi masikini kama yetu, kuamua kutumia shilingi bilioni 34 Kwa ajili tu ya makumbusho ya viongozi wetu, wakati mahitaji ya msingi ya watanzania hamjatimiza??

Kwenye nchi ambayo watanzania walio wengi, hawana hata vibanda vya chumba kimoja Cha kujisitiri, hayo ni matumizi ya hovyo kabisa ya Kodi zetu!😳
Bongo bhana...... kazi kweli kweli...ukihoji utaambiwa hata yasipojengwa shida za Watanzania hazitakwisha.
 
Back
Top Bottom