Serikali imetangaza kuanza ukaguzi na kutaifisha ardhi yote iliyovamiwa ikiwemo ya maeneo ya wazi, pamoja na kufuta umiliki wa maeneo makubwa yakiwemo mashamba yasiyoendelezwa na yanayotumika kinyume na matumizi yaliyoombewa na kurudisha serikalini katika benki ya ardhi.
Akizungumza na waandishi wa habari katika uzinduzi wa mradi wa wajibu wa uwekezaji katika mali na ardhi-RIPL-kwa niaba ya Katibu Mkuu, wa wizara ya ardhi, nyumba na maendeleo ya makazi Mpimaji mkuu wa serikali Bwana Nassor Duduma amesema serikali imeunda kitengo maalum cha uwekezaji ardhi kilicho chini ya kamishina wa ardhi ambacho kitazunguka nchni nzima, kikianzia mkoani Dar es Salaam na kuwataka wote waliomiliki ardhi, kinyume na taratibu, wasiondeleza wajiandae kurudisha ardhi serikalini.
Akianisha changamoto katika sekta ya ardhi nchni Mkurugenzi wa jumuiko la maliasili Tanzania Bwana Joseph Olila amesema licha ya kuwepo kwa miongozo na sheria katika sekta ya ardhi lakini bado vitendo vya uvamizi wa ardhi vinaongezeka kutokana na tatizo la elimu kwa wananchi, kwa upande wa vijijini amesema michakato wa uwekezaji hauko wazi kutokana na sheria na miongozo ya kitaifa haipelekwi katika maeneo hayo hali inayosababisha migongano.