Serikali yachukua hisa asilimia 100 katika kiwanda cha General Tyre

RUCCI

JF-Expert Member
Oct 6, 2011
1,701
1,714
Waziri wa Viwanda na Biashara Charles Mwijage amesema katika mchakato wa kufufua viwanda serikali imepanga kukirejesha kiwanda cha General Tyre, na tayari serikali imekwisha chukua hisa asilimia mia moja na wako mbioni kuanza uzalishaji.

Katika hatua nyingine amawataka wadau wakiwemo wananchi wanaowafahamu wafanyabishara wanaoficha sukari wawafichue ili wawashughulikie.

Amesema kwa taarifa ambazo serikali inazo mpaka sasa hakuna upungufu wowote wa sukari na kusema mfanyabiashara atakaebainika kuficha sukari serikali haitasika kuwafutia leseni zao.
 
Wako mbioni kuanza uzalishaji wa tyres.....how soon....na technology itakuwa ya nchi gani.Turudi Akron makao makuu ya General Tyre intl,hivi hivi hakuna kitu.
 
Serikali lazima iwe makini sana na kujiingiza kwenye umiliki wa viwanda. Tulitoka huko na tukashindwa. Sioni sababu kwa nini sasa tutaweza.

Kuhusu suala la sukari ni hivyo hivyo. Sukari inapanda bei kutokana na uhaba. Maneno matupu ya mawaziri siyo mbadala wa uwepo wa sukari. Hakuna mfanyabiashara mjinga ambaye ataweka pesa yake kwenye sukari kwa ajili ya kuhodhi tu bila sababu. Kwanza kisheria hiyo sukari ni ya huyo mfanyabiashara. Si ameinunua?

Ni muhimu viongozi wetu watumie busara katika kuongoza na siyo kukurupuka tu. Yanayotokea sasa hivi ni marudio. yalitokea hapo zamani na madhara yake wengi tulioishi enzi hizo tunayajua.



Those who fail to learn from history are doomed to repeat it - George Santayana
 
Tatizo siyo umiliki bali ni "Royalty". Hatuwezi kuzalisha matairi bila kutumia wataalamu toka "brand" kubwa duniani na ili utumie technolojia yao lazima tulipe Royalty.

Hakuna mwendawazimu atayekubali kuhatarisha maisha yake kwa kutumia matairi yasiyoeleweka "brand"
 
Ni habari njema sana ila Naishauri serikali isijihusishe na uendeshaji wa viwanda maana huko ndiko tulikotoka tukashindwa.Kiwanda kitafanya vema ktk utawala wa magufuli atujui ajaye atakuwa vipi.

Ni vema Serikali ikatafuta mwekezaji asiye mbabaishaji akaleta teknolojia ya kisasa kiwanda kibaki mali ya Serikali Mwekezaji apewe bure awekeze na kukiendesha Serikali iwe na hisa.Hapo tutakuwa na faida mbili kodi pamoja na gawio la hisa.

NAOMBA KUWAKILISHA HOJA.
 
Matairi ya Kichina yameanza kutumiaka nchini juzi juzi tu, sidhani kama yana miaka walau 10, Goodride, Savero nk; yana brand gani haya? General tyre kilikuwepo na tairi zake tunazifahamu. Binafsi kwa ajili ya kuipenda nchi yangu nitakua mtumiaji mzuri tu wa haya matairi, napendekeza ili kue na uzalendo wa moja kwa moja basi matairi ya magari yote ya serikali na taasisi zake zote watumie tairi za General tyre tu.
 
Hii serikali ya ccm inashangaza sana, wanapokuja mbele ya wananchi na kujitapa kuwa wanarudisha umiliki wa kiwanda asilimi a100, kwa mbwembwe na majigambo, utafikiri waliporwa kwenye mapambano na sasa wamepambana wakawanyang'anya waliio wapora, serikali yenyewe ilishindwa ikaviua vitu vingi wamefanya kwa maamuzi yao kwa ufisadi wao, na kwa jinsi wanavyokurupuka tusubiri aina nyingine ya uwekezaji.
 

Pendekezo lako linaweza kuwa zuri. Lakini tusijefika siku tukaambiwa kuwa hakuna kuagiza matairi kutoka nje kwa sababu ya General Tyre yapo.
 
kuna namna nyingi ya uendeshaji viwanda serikali inaweza kumiliki kiwanda ikatoa mtaji lakini ikakodisha menejimenti ambayo itaendesha kiwanda kazi ya serikali itakuwa ni kumwekea malengo kwa tabia zetu za kupeana ajira kindugu na kirafiki pamoja na wizi na ubadhilifu hatuwezi kuendesha viwanda
 
Pendekezo lako linaweza kuwa zuri. Lakini tusijefika siku tukaambiwa kuwa hakuna kuagiza matairi kutoka nje kwa sababu ya General Tyre yapo.
kama kiwanda kitakuwepo hamna haja ya kuzuia matairi toka nje ni kuweka kodi kubwa na wakati huohuo kutoa ruzuku kwa kiwanda cha general tyre
 
Pendekezo lako linaweza kuwa zuri. Lakini tusijefika siku tukaambiwa kuwa hakuna kuagiza matairi kutoka nje kwa sababu ya General Tyre yapo.
Sidhani kama tunaweza kufika huko, kwanza sidhani kama General tyre itakua na uwezo wa ku supply matairi ya kutosheleza magari yote ya hapa nchini hilo 1 lakini la 2 ni hili, zipo machine za wawekezaji kama zile za kule migodini, watengenezaji wa machine hizo hua wamewekeana mikataba na viwanda vikubwa vya matairri duniani, utakuta karibu zote zina tairi ya Micheline au Good year n.k. Nijuavyo mimi huwezi piga marufuku uagizaji wa vitu toka nje hadi ujiridhishe kama viwanda vyako vinatosheleza mahitaji ya ndani kwanza. Kingine ambacho pia naomba kuongezea ni hiki, Watanzania tulio wengi sio wapenzi sana wa vitu vya ndani, utakuta Mtanzania wa Mwanza, Kagera, Geita n.k ana agiza maji ya kunywa ya Rwenzori kwa bei ya Tsh 1000 kwa chupa yenye ukubwa wa lita 1.5 na anaacha maji ya Dasani, Uhai, JAMBO ambayo ni ya hapa hapa nchini tena Dasani na Jambo yanatengenezwa kwenye kanda hiyo hiyo; hili jambo linatakiwa shule special kabisa na hili ndio linalo tutofautisha sisi na Wakenya, Mkenya ni vigumu sana kumkuta ananunua kitu cha nje kama ndani ya nchi yake kipo but also this goes hand in hand na wenye viwanda wa Tanzania, kama bidhaa ulioitengeneza ilikua BORA na sisi kama walaji tumekuunga mkono, maintain UBORA huo huo mara zote.
 
Wakati Tanzania ina magari yasiyozidi asilimia tano ya yaliyopo sasa ilikuwa na kiwanda cha matairi ya magari kikiendeshwa kwa faida, leo hii yapo magari mengi sana yanayohitaji matairi nchi haina kiwanda cha matairi.
Pana hoja hapa kwa wenye kutumia vichwa vyao kufikiri na si wale wanaotumia makalio!
 
Siakuelewa una maana gani? ukiongelea kuhusu asilimia lazima uoanishe na jumla.. sasa unaongelea asilimia halafu unaiacha hewani, huwezi kueleweka
 
Brand si hiyo general tyre au?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…