Nchi rafiki zilikuwa zinalalamika, Zinajitolea kuprovide Scholarship inayocover Tuition fee pamoja na accommodation fee, lakini Wanafunzi bado wanakuwa hawaendi!. Tatizo ni uwezo wa kulipia nauli za ndege!.
Hapo ndipo serikali ilikuwa inaona aibu, kwamba watoto/vijana wetu wapewe ng'ombe mzima sisi tushindwe kuchangia hata mkia?. Ndipo serikali ilipokuwa inachangia japo nauli ya ndege kwa hawa vijana!
Serikali zote zilizopita zilifanya hivi, Nashangaa serikali yetu hii inayokusanya matrilioni ya pesa kila mwezi inashindwe kuona aibu, yaani China ikusomeshee watu wako bure, Iwape Stipend kila mwezi bure, Iwape malazi bure, halafu serikali yetu ishindwe kuchangia japo kiduchu?
Hii ni aibu!