Serikali ya Magufuli ikubali kujitathmini, hatutaki CCM ipotee

mkafrend

JF-Expert Member
May 12, 2014
3,047
1,503
Watanzania wenzangu, salaam!
Mimi kwa upande mmoja naipongeza serikali inayoongozwa na Mhe Dkt John Pombe Magufuli kufuatia uwezo na weledi ktk vita dhidi ya ufisadi nchini.

Hata hivyo kuna issue ambazo kama zikiachwa zilivyo zinatia shaka uhai wa CCM, hatutaki tuendelee kushinda uchaguzi kwa kusaidiwa na vyombo vya usalama wala polisi. Hebu sasa tukiwa wanaccm tulioiva tushauri serikali ibadiri mienendo hii:-
1. Sakata la dawa za kulevya polisi ndio wahusike kupeleleza, kubaini na kukamata wahusika badala ya kutajataja majina kienyeji as if hakuna professional police waliobobea ktk upelelezi.

2. Katika mabadiriko ya baraza la mawaziri ajaribu kutoa kipaumbele kwa Wabunge waliochaguliwa majimboni ambao wana uwezo wa kusimamia wizara. Kuteua uwaziri toka kundi la Wabunge walioteuliwa kunatia ukakasi na kuwafanya walioachwa waone kama wametengwa, (tukumbuke walioteuliwa nafasi za juu ni Tulia Acksoni (spika), Ndalichako (waziri elimu), Mbalawa (waziri uchukuzi), Mpango (waziri fedha), Posi (naibu waziri), Mahiga (waziri mambo ya nje) nk nk hii list hapendezi kabisa kwa kuwa Bungeni tuna mtaji mkubwa wa Wabunge toka majimboni.

3. Katika baadhi ya mikoa imethibitika taarifa ya hali ya chakula, njaa na mikakati ya uzalishaji mazao iliwasilishwa. Hivyo, tusivutane ktk hili kwa kuwa baadhi ya maeneo tayari yana upungufu mkubwa wa chakula. Serikali ithibitishe kuwa pamoja na upungufu huo hakuna mwananchi atakayekufa kwa njaa,

4. Mivurugano na mivutano ya kimaslahi - katika vita dhidi ya kukuza uchumi pamoja na kuwa kipaumbele chako ni Tanzania ya viwanda lakini tufahamu kuwa hivi tumefika idadi ya watu takribani 50milioni. Ambapo kati ya idadi hii 70% ni wakulima, hivyo kipaumbele cha kwa kinapaswa kuwa Tanzania ya Kilimo cha kisasa. Viwanda inapaswa kuwa kipaumbele cha pili.

5. Tathmini juu ya mikopo ya wanavyuo wa elimu ya juu - maskini ni wengi

6. Tathmini ya ajira - hapa vijana wengi wako mitaani na fursa za nje ya mfumo wa umma haziwezi kuwafikia wote hivyo upanuzi wa wigo wa sekta binafsi ni muhimu.

7. Watumishi wa umma ni kaa la moto.

Nwasalisha.
Msakila KABENDE
KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI
 
Chama chetu cha mapinduzi kiko imara na wala hakiwezi babaishwa na hawa wauza madawa ya kulevyaaa mkuuuu. Tumedhamilia kuiokoa tanzania na kila mwenye tuhuma hatapona ata mumojaaa.
Haiwezekani madawa ya kienyeji yauzwe kama karanga eti ccm tukae kimya kisa tunalinda wapiga kura, lazima watuhumiwa wawajibishwe kwa viwango vya hali ya juuu ilikujenga tanzania mpyaaa
Kwahiyo serikari ya magufuli iko imara na haitayumba mileleee.
 
A politician looks forward only to the next election. A statesman looks forward to the next generation- Thomas Jefferson

Wewe unafikiria uchaguzi wa kesho wakati Rais Magufuli anafikiria Tanzania ya karne ijayo.
 
A politician looks forward only to the next election. A statesman looks forward to the next generation- Thomas Jefferson

Wewe unafikiria uchaguzi wa kesho wakati Rais Magufuli anafikiria Tanzania ya karne ijayo.
Salute mkuu..

Mawakala wa DZK wanaibuka na utetezi ktk style mbalimbali...
 
A politician looks forward only to the next election. A statesman looks forward to the next generation- Thomas Jefferson

Wewe unafikiria uchaguzi wa kesho wakati Rais Magufuli anafikiria Tanzania ya karne ijayo.
Haha hii ya chini nilitaka nikukumbushe kuwa umeisahau!!!
keep it up kijana wa ukweli siku moja juhudi hizi zitakulipa dada
 
A politician looks forward only to the next election. A statesman looks forward to the next generation- Thomas Jefferson

Wewe unafikiria uchaguzi wa kesho wakati Rais Magufuli anafikiria Tanzania ya karne ijayo.
Karne ijayo kutakua na vilaza wengi kuliko kawaida angalia mfano wa elimu takwimu zina poromoka mfumo unabomolewa eti elimu bure mikakati 0% tutaendelea kuburuzwa anglia watawala/viongozi mbali mbali wamepata elimu ya ainagani watoto wao vipi. Wewe unandaliwa mazingira ya kutawaliwa tu. Tanzania ya viwanda wakati uti wa mgongo ni kilimo na hujaiupa kipao mbele kwani hatuna ziada alafu eti viwanda au ndoturudi kwa makaburu tukaburuzwe huko viwandani mpaka bas kwa kufanya vibarua huku wajiriwa wakitoka nje .... tunajitengnze bomu kesho tujiripue wenyewe nikitazama naona kila mtanzania jipu
 
Ni ushauri na wala siumi meno - tukiendelea kusifiana ili kutafuta sifa hasara itakuwa kwa kizazi kijacho. Pia wanaofahamu nimesema kuwa vita dhidi ya mihadarati ni nzuri lkn polisi kupitia kitengo cha madawa ya kulevya wafanye juu chini kuwatia watu wakiwa na mizigo isiwe mtu mwingine kutajataja tu
 
Aongoze kwa kufata sheria na katiba sio mabavu ktk maamz, aangalie vipaumbele vinavyonufaisha umma hasa maskn, mf kuwainua kimaisha, ktoa mikopo kwa umma na Elimu juu,dawa hospt, elimu iboreshwe ikiwemo nyenzo zote na walimu,

VIWANDA sawa lakn ss wengi wakulima hivyo havitusaidii moja kwa moja, Ajira ni muhimu sana kwa vijana hasa maskn wasokua hata namitaji ya kujiajiri lakn serikali imekalia uhakiki na ktoajiri vjana wanazd kulundkana mtaani tu, ndege na viwanja sawa muhimu lakn sio kwa watu masikn kama watanzania, haikupaswa kuwa kipaumbele sema mnapenda sifa sana kutaka kusifiwa tu,

Mnafikr ndege hata bb zetu watapanda? Dawa hospt c watatbiwa! Mkiajiri walimu c watafndsha watoto wa maskn angalau kupungza dv 0!

Mnafanya mambo kuwa kipaumbele yasiyosaidia maskn kwa muda huu, huwez kuweka paa wakat hujajenga msing na ukta, mm binafsi sikupgia ccm kura na stapgia ccm kura hasa JPM, mmejaa kejeli na dharau,mnafkr ndo mmekuja milele madarakani?

Ajira mwaka mzma ni zakuteauana tu vp vijana graduate toka 2015? Hovyoooooo!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…