Serikali ya awamu ya tano imesaini mikataba 41 na nchi 9 kwa Maendeleo ya Nchi

MLAU

JF-Expert Member
Aug 23, 2007
4,726
3,359
Toka awamu ya tano iingie madarakani imesaini mikataba 41 na nchi 9 katoka nyanja mbalimbali za Huduma za jamii

Kama elimu afya na maji.biashara, miundo mbinu Huduma ya usafiri,fedha na uchumi n.k

Kutokana na mikataba hii 41 kutoka nchi 9 tunategemea mabadiliko makubwa kwa maisha ya watanzania chini ya utawala wa Rais Dr John Magufulu

Waliopewa dhamana ya kusimamia na kufuatilia tafadhali tusimamie vizuri mikataba hii.

Kumbuka mikataba hii mingine ni msaada lakini mingine ni mikopo ambayo inaongeza deni la Taifa.
 
Hebu tupe list mkuu! Mimi nakumbuka 35 tuu...

Wachina mikataba 17
Morocco mikataba 9
Uturuki mikataba 9

Jumla hapo ni 35! Nimesahau ya nchi ipi?
 
Vipi vile alivyoombwa Mfalme wa Morocco msikiti na uwanja wa mpira vimeshaanza kujengwa??

Mgeni anakuja kwako anakukuta una njaa na mahitaji mengine muhimu lakini cha maana cha kumuomba unaona ni msikiti na uwanja wa mpira..!!
 
Vipi vile alivyoombwa Mfalme wa Morocco msikiti na uwanja wa mpira vimeshaanza kujengwa??

Mgeni anakuja kwako anakukuta una njaa na mahitaji mengine muhimu lakini cha maana cha kumuomba unaona ni msikiti na uwanja wa mpira..!!
Usiwe na wasi mkuu, huyu forward kazoea kutoa boko. Sasa hapo mi naona kawaida sana
 
Hio mikataba yao. Ni ya kufikirika sana ... Kwa sababu serikali hii inachokiamini sio realistic kabisa..
Kama-
-Serikali inaamini hakuna njaa
-inaamini kuwa haijisiki kwenye tetemeko
- kwenye kampeni hakuahidi tetemeko
- je:-
Hio mikataba kweli ina uhalisia gani na jamii?
Uwezekano mkubwa sana hio mikataba haina lolote la maana.
Au inaakisi mambo ya ajabu ajabu.
Kama kuna njaa na wananchi nchi nzima
wanalalamika njaa ila serikali tu rais na viongozi wake aliowateua wao ndio hawana njaa.
Na zaidi magazeti yakiandika yanachochea.
Sasa watu hawa hawa watadhindwaje kusaini mikataba kama ya Mangungo.
Kwa sababu jamaa ni wabishi sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…