Serikali ya awamu ya 5 andaeni mpango kazi

sizzya007

JF-Expert Member
Mar 15, 2016
771
2,415
Wajameni, hamna mtu anayelipinga swala vijana kupata kazi na kujishughulisha, hayupo! Isipokuwa na vigumu sana kuamini yanayofanya na serikali ya awamu hii ya tano, mengi yanaonekana yako kisiasa, na hii ni hatari, nchi inaongozwa kwa mihemko ya kisiasa zaidi! Nitatoa mifano ya mambo kadhaa.

Alipoingia madarakani tu, Raisi Magufuli alitembelewa na Prof. Lipumba pale ikulu, Raisi Magufuli akampa Lipumba kazi ya kuandika tathmini ya hali ya uchumi ya nchi, ilitangazwa na wote tukajua, je! Ripoti hiyo tayari Mh. Raisi anayo? Ndio hiyo anayoifanyia kazi? Na kama anayo mbona haikuwekwa katika magazeti ya serikali ili na sisi waajiri wake (wananchi) tupate kuisoma?! Hapa ndio naanza kuyatilia shaka baadhi ya mambo, hili lilifanyika kama tukio la kisiasa zaidi, i believe! Binafsi ningependa nijue hali ya uchumi ya nchi yangu na kwanini tumekuwa tukifanya vibaya gor the last ten years, maana yule mstaafu aliwahi kusema hajui kwanini kaya yake ni maskini, Lipumba angeweza kutoa jibu ambalo wengi tulitamani Raisi wetu mstaafu kulitolea majibu ila alishindwa!

Serikali hii inajinadi kwa kauli mbiu ya HAPA KAZI TU, ni kauli tamu na nzuri, ila binafsi nilisha kataa kuamini kauli mbiu tamu tamu, waswahili wanasema tamu ni haramu, hapa kazi tu, kazi hizo ni zipi, zimeandaliwa mazingira gani ya kuwa kazi bora?! Sheria za kazi zimebadilishwa?! Kuna sheria kandamizi dhidi ya wafanyakazi, vipi hizi kwanza ziko sawa?! Na vipi viwanda tulivyoambiwa kuwa vitajengwa na ajira tutapewa navyo viko tayari?! Kama lah! Vijana hawa kazi wakazifanyie wapi? Shambani? Sawa! Swala la ruzuku za pembejeo zimetolewa?! Waziri wa kazi anajua nchi yake inaweza kuzalisha ajira ngapi kwa mwaka?

Yakk mengi ambayo yanatakiwa kujibiwa kabla ya kuanza kukurupuka!

Aliyepita kipindi anaingia aliingia hivi, HALI MPYA NGUVU MPYA KASI MPYA.

Baada ya miaka mitano hali ilikuwa mbaya, nguvu ikashuka kabisaaa na kasi ikapungua na kuwa ya kobe.

Akaja tena na HALI ZAIDI NGUVU ZAIDI NA KASI ZAIDI, silizungumzi hili, wote tunajua nini kilifuata baada ya hapo (MAJIPU).

Rai yangu (binafsi) kwa serikali hii, ni vizuri zaidi kutatua tatizo moja at a time, Magufuli kuongoza nchi ni kugumu kuliko kuongoza familia, tatua tatizo moja baada ya jingine, HAIWEZEKANI kutatua kila unaloliona tatizo ndani ya mwaka mmoja wa uongozi, ndio maana kuna miaka mi5 ya kuongoza! Ni bora uhangaike na jambo moja kubwa muhimu kwa miaka miwili, na kulilatia ufumbuzi wa kudumu, na tutakukumbuka kwa hilo kuliko kudandia kika tatizo, hapo ndio tutaishi kwa kutumbua majipu tuu bila kusonga mbele, kama uneamua kusafisha ofisi za umma fanya hivyo kwanza na uhakikishe hilo linaisha.

Tujadili.
 
Hakujiandaa, ndio maana anarudisha sera ya nguvu kazi iliyoshindikana miaka ya 80. Hajui afanyeje kutimiza ahadi imebaki vitisho.
 
Rai yangu (binafsi) kwa serikali hii, ni vizuri zaidi kutatua tatizo moja at a time.

Kama ingekuwa raisi anatatua tatizo moja at a time kusingekuwa na wizara nyingi.Kiongozi hata mzazi kazi yake ni kutatua matatizo mengi kwa mara moja.Akitatua moja kwa mara moja ni hatari.Chukulia angetatua tu la bandari akatulia.TRA wangekuwa wanaendelea kuiba,Nida wanaendelea kuiba,Tanesco wanaendelea kuiba nk hiyo concept yako ni jipu inatakiwa itumbuliwe.
 

Haujanielewa vizuri!! Chukulia Raisi aamue kuwa mie katika kipindi hiki nataka kutatua tatizo la ajira kwa vijana kwa kujenga viwanda na kujenga vyuo vingi vya ufundi ili vijana wakapate maarifa ambayo yanaweza kuwakwamua kutoka katika janga la kukosa ajira, hili ni jambo moja, ila hili likushughulikiwa vizuri na kwa ufanisi effects zake zinaspread eccentrically.....

Kipindi wizara nyingine zinashughulikia mambo mengine, raisi yeye anajikita zaidi na wizara moja lets say wizara inayodeal na mambo ya ajira kwa miezi sita fully, mpaka kumaliza muda wake wa miaka mitano, tunaweza tukatatua matatizo sita (kwa wastani). Huo ni mfano fikirishi tu!

Na katika kutazama mambo kwa pembe tofauti kama hii tunarudi katika mjadala wa kuwa na malengo ya kitaifa. Ni vizuri na ni heri zaidi tuwe na malengo matatu ambayo si serikali yoyote itayasimamia hata kama ni kwa miaka kumi mfululizo, ila tuhakikishe tunafanikiwa kwa kiwango kikubwa katika jambo moja kwa mafanikio yanayoonekana.
 

Vyote lazima viende sambamba. Sasa atatatuaje suala la ajira kama hamna umeme ambao unategemewa na viwanda. Labda wewe sema uandaliwe mpango makkati wa seckta zote na uwekwe wazi kwa wananchi woote. Lakini watu hawawezi wakakaa tu wanangojea zamu ya kuhusu kazi za vijana baada ya miaka 3 watakula nini. Na kwa kawaida huwa kuna mpango wa muda mfupi, wa kazi na mrefu kwamfano hilo lakuwaambia vijana wasicheze pool wafanye kazi! Hilo lingojee tena mwaka gani ni kutekeleza immedeately. Tena namuunga mkono Rais. Niliwahi kushiriki kwenye research moja ward moja niliona jambo la ajabu baadhi ya wazazi wanadekeza watoto sijawahi kuona esp. wa kiume. Yaani tulikuwa tunenda asubuhi. Wazazi wanajishughuklisha na biashara vijana kuamka kwao sijui saa 3 wakiamka wananawa wanakunywa chai vijana hata kuondoa vyombo hamna wakishakunywa tu chai hao wanaenda kijiweni huko ni michezo mbalimbali , football, etc. wanangojea time ya chakula kwa ukweli lazima tubadilike maendeleo ya mtu mmoja mmoja ndio maendeleo ya taifa kwa ujumla! Serekali iweke bayana fursa zilizopo kwa vijana ( mpango wa kati sasa) ili waweze kuzitumia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…