Habari,
Wadau naomba tujadiliane kuhusu best brain za tanzania kuishia kwenye mashirika binafsi. Serikali inabidi iweke mkakati thabiti wa kuhakikisha best brain zinabaki serikalini ilikufainkisha maendeleo ya nchi yetu. kwa hali nionavyo sasa wale vichwa wetu wote wakimaliza chuo wanaishia taasisi binafsi na wachache wanabaki vyuooni kufundisha.
Ili inchi yetu iendelee tunahitaji watunga sera na wanamipango wabunifu na wenye uwezo mkubwa wa kufikiri na kubuni mambo ambao bahati mbaya kwasasa wengi wao wanaajiriwa na taasisi binafsi kwasababu ya malipo na benefits bora. Ila hawa watu wamesomeshwa kwa pesa za walipa kodi inabidi wawajibike kwa taifa lao sisemi wakiwa taasisi binafsi hawawajibi kwa taifa ila wangetoa mchango mkubwa zaidi kama wangekuwa serikalini kwasababu wangegusa sekta zote ikiwemo binafsi pia.
Serikali haina budi kuboresha mazingra ya kazi na malipo ili tuweze kuwa maintain hawa vipanga wa nchi, leo hii mtu akimaliza Bachelor yake ya Telecom na akawa anahitajika na makapuni ya simu bila shaka hawezi kuchagua TTCL akaacha TIGO au VODA vivyo hivyo kwa kada zingine.
Karibuni tujadili wadau