A
Anonymous
Guest
Nimelazimika kuandika huku Jamii Forums baada ya kuona hali inazidi kuwa mbaya, wazee wetu wanakufa wakiwa na masononeko na Serikali yao.
Waliokuwa Wafanyakazi zaidi ya 700 wa kiwanda hicho wamekuwa wakidai malipo yao ya mishahara tangu Mwaka 1997 hadi 1998.
Mzee wangu na wenzake wamepokea ahadi mara kwa mara kutoka Hazina kuhusu malipo haya, lakini hadi leo (Septemba 2024) hakuna hatua madhubuti zilizochukuliwa.
Hazina iliahidi kuanza mchakato wa malipo Mwaka 2021 kwa jumla ya Shilingi Bilioni 123 na Milioni 400, lakini hakukuwa na utekelezaji wowote tangu wakati huo.
Soma Pia: Vilio vya Wastaafu wa majeshi vitatuliwe haraka, kinachoendelea ipo siku kitatengeneza ‘matunda yasiyofaa’