Robert Heriel Mtibeli
JF-Expert Member
- Mar 24, 2018
- 28,188
- 67,753
SERIKALI MNAJUKUMU LA KUWASAIDIA HAO VIJANA WA NETO NA WATANZANIA WOTE NA SIO KUWALETEA UKOROFI. TUSIWE KAMA WATU WASIO NA AKILI TUSIOJALI.
Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli
Vijana Wasomi wote wanahaki zote kuitaka serikali iwaajiri. Hao NETO ni sehemu ya vijana hao.
Achana na kina Siye kina Taikon ambao tulisoma kwa mapenzi yetu. Yaani hata serikali isingelazimisha Sisi tungesoma tuu kwa Sababu tulikuwa tunapenda mambo ya kitaaluma, Elimu, maarifa, na ufahamu.
Lakini lipo kundi kubwa la vijana ambao kama sio kulazimishwa na kudanganywa, kutapeliwa kwa ahadi za Uongo kuwa mtu akisoma basi atapata Ajira nzuri na Kuishi maisha mazuri. Kwa kauli za hapa na pale kama Elimu ni ufunguo WA maisha na nyinginezo. Vijana hao wasingesoma Kabisa na Wala Wazazi wao wasingethubutu kuwapeleka shuleni.
Wapo wazazi kimakusudi kwa hiyari yao walikataa kupeleka watoto wao shule Miaka hiyo nasoma, lakini serikali iliwashinikiza kwa nguvu kuwa ni Amri wazazi wapeleke watoto wao shule. Basi ikawa hivyo.
Mbunge wa Kahama, Mhe. kishimba aliwahi alezea Jambo hili kwa uchungu Mkubwa.
Wazazi wameuza mashamba, Ng'ombe, na Mali nyingine wakijua wanawekeza kwa watoto wao kama walivyoambiwa na Mifumo ya serikali kuwa Elimu ni uwekezaji.
Matokeo yake watoto wamemaliza Shule, hakuna lolote la maana linaloendelea.
Wametapeliwa?
Wamedanganywa?
Vijana wamesota,
Vijana wamekesha usiku kucha kwa kile kiitwacho Elimu.
Vijana wamepoteza Muda wao mwingi.
Vijana wamepoteza pesa Zao za Kutosha.
Vijana wamebaki na Madeni ya Bodi ya Mikopo.
Vijana wamejikuta katika hasara karibu ya kila Kitu.
Leo vijana wanaishinikiza serikali iwaajiri kuna watu wanawaona ni wahalifu Kweli?
Sio ninyi mliowaambia wasome ili waajiriwe?
Najua mtawakana,
Kama mtawakana lakini Mtaala wa Elimu mliyokuwa mkiwapa unawaumbua.
Vijana wamefundishwa ili waje waajiriwe na sio kujiajiri.
Mtaala wa Elimu haupo kuandaa mtu kujiajiri isipokuwa kuajiriwa.
Mtu kasomea Udaktari au uhasibu anatafuta Ajira ya Udaktari mumuajiri mnamuambia sio lazima awe Daktari. Anaweza kujiajiri hata kuuza chips au bodaboda. Sasa kama ni hivyo kulikuwa na ulazima gani wa kulazimisha watu wasome na kupoteza Muda na Mali wakati Mbeleni uwekezaji huo unakuwa hauna maana.
Serikali imeshindwa kusimamia suala la ajira na HAKI za vijana wanaofanya Kazi.
Hata wakiajiriwa huko sekta binafsi wanalipwa pesa za ajabuajabu. Wanalipwa pesa kidunchu zisizoendana na elimu zao. Viongozi wenye dhamana wapo sio kwamba hawajui wapo Kimya.
Hivi Mwalimu wa degree analipwa Laki Moja unusu kweli na serikali IPO. KWELI?
Madaktari na Afisa tabibu wanalipwa mishahara ya mbuzi mee. Serikali ipo haifanyi chochote. KWELI?
Wakaguzi wa mashule, na hospitali wanafanya Kazi gani Mpaka vijana wanalipwa pesa zisizoendana na elimu zao.
Ati vijana wajitolee, hivi mnaakili sawasawa? Kwa nini hamna Roho ya KUJALI watu wenu?
Kwa nini mnapuuza vijana Maskini wa nchi yenu?
Yaani mzazi asomeshe mtoto wake ili aje ajitolee. KWELI?
Serikali, nilishasema pigeni Marufuku vijana kujitolea.
Mnawafanya vijana Watumwa kwenye nchi Yao wenyewe. KWELI?
Na hamjali! KWELI?
Kijana akiongea, mnamkamata na vikesi vya hapa na pale. KWELI?
Hiyo sio HAKI.
Wapendeni vijana wa nchi yenu.
Pendeni wale mnaowaongoza. Huo ndio uongozi. Huo ndio uzalendo.
Mnafurahi kuona vijana wakihangaika kwenye nchi Yao kana kwamba hakuna serikali. KWELI?
Nilishawaambia, tusipovamia tutavamiwa. Ona sasa! Tazama! Vijana Wasomi ati serikali haijui pakuwapeleka. Inashangaza!
Wanakuja wageni wanatamba mbele ya wenyeji. Mpo tuu!
Mnawaita wawekezaji. Sawa! Sheria za kulinda maslahi ya vijana wa Tanzania kwa hao wenyeji zinasemaje. Vijana kwenye viwanda wanalipwa pesa za Usukule, utumwa, hakuna anayejali.
Viongozi ninyi ndio Wazazi WA vijana wa taifa Hili.
Niliwahi andika kuwa, hatutaki viwanda vinavyogeuza vijana wetu kuwa Watumwa na misukule. Ni Bora tusiwe na kiwanda hata kimoja kuliko watoto wetu wenyewe tuliowazaa kuwageuza Watumwa na kuwatoa Kafara wawe mandondocha ya kuwanufaisha watu wengine.
Mnasema vijana wajiajiri kwenye Kilimo sijui kwenye vitu gani
Sio ninyi mliowaambia Wasome?
Ikiwa mliwaambiwa wasome mkawatelekeza Mnafikiri watawaamini mkiwambia wajiajiri ili muwatelekeze tena?
Wangapi wamejiajiri kwenye Kilimo lakini wameishia Kupata hasara na Kupata Magonjwa ya moyo baada ya Kilimo kuwapiga KO.
Kama mliwambia wasome na hamkujiandaa kuweka mazingira ya kuajiri iwe sekta binafsi au serikali. Mtaweza kuwasaidia wakijiajiri wenyewe?
Achana na wazo kuwa watapata wapi mtaji.
Tufanye wanamitaji serikali imejiandaaje kuwalinda na kulinda mitaji Yao?
NINI CHAKUFANYA;
1. Serikali ipige Marufuku Wahitimu au Wasomi kujitolea. Adhabu Kali zichukuliwe kwa taasisi, mashirika na makampuni yanayochukua vijana wanaojitolea.
2. Serikali ichukue hatua Kali kwa makampuni, mashirika, taasisi zinazolipa Mishahara kinyume na kima kilichotolewa na Serikali.
3. Serikali ihakikishe mashirika, taasisi na makampuni yanatoa mikataba halali ya kisheria kwa Wasomi.
4. Vyama na Bodi za taaluma zipige Marufuku wanataaluma katika vyama na Bodi Zao kujitolea kwenye taasisi, makampuni au shirika.
5. Vyama na Bodi za taaluma zifungue Kesi kwa makampuni, mashirika na taasisi zinazofanya uonevu, utapeli, na dhulma kwa wanachama wao.
6. Serikali ianze utekelezaji wa Sera ya UVAMIZI wa NCHI zingine kwa kuandaa Mipango na mikakati katika Kusaidia watu wa nchi yetu na taifa letu.
7. Bidhaa zetu kama za Kilimo zisiwe na ku-bet. Liwepo soko la uhakika hasa Nje ya Nchi kwa bei itayosaidia vijana wetu.
8. Ipigwe Marufuku wananchi wa nchi jirani kuzurura zurura ndanindanj ya nchi kuchukua bidhaa za Kilimo. Yaani huko mashambani.
Yawepo Masoko ya nafaka ya kimataifa ambapo Raia wa kigeni akiingia ndani ya nchi ataenda kununua kwenye Masoko hayo.
Sio Mtu kutoka Kenya aingie Tanzania, asonge Mpaka vijijini ndanindani huko achukue bidhaa zetu kwa bei Sawa na Bure. Huo ni upumbavu.
Napendekeza; Ukanda wa Nyanda za juu Kusini (labda Songea) lijengwe soko kubwa la nafaka la kimataifa ambapo wageni wanachukua nafaka hapo.
9. Hati za kusafiri (Passport) kusiwe na Mlolongo Mrefu. Vijana wenye uhitaji wa kufunguka na kutanua uwanja wa utafutaji Nje ya Nchi wapewe waende. Wapate changamoto kwenye Visa lakini sio changamoto kwenye passport
10. Elimu ya Digital na mtandaoni zitolewe. Serikali ipunguze gharama za bando vijana wajiajiri mtandaoni
11. Serikali itoe Mikopo kwa Makundi ya vijana wenye kuonyesha uthubutu na Ubunifu.
Kwa mfano hao NETO, hakukuwa na sababu ya kusumbuana nao. Lilikuwa ni Jambo la kuwaambia kuwa ni kweli tuliwadanganya au pengine hatukuwa na Nia ya kuwadanganya kuhusu kusoma na kuwaajiri lakini mipango sio matumizi. Tumesomesha wengi na sasa uwezo wa kuajiri umekuwa mdogo.
Lakini mnaweza kuwasaidia kama watatengeneza vikundi vya vijana Wasomi wenye mawazo yanayofanana, wapewe Mkopo na serikali itawasimamia.
Ingawaje NETO Kuna MADAI Yao kadhaa wamepuyanga ikiwepo dai la kutokutaka Usaili.
Lakini hiyo haimaanishi tusiwachukulie kama watoto na vijana wetu.
Tusiangalie namna ya kuwakomoa au kuwakatisha tamaa. Bali tulichukulie Jambo hili positive.
Wasaidiwe.
Robert Heriel
Taikon Master
Kwa sasa Dar es salaam