Serikali: Marufuku kufukuza wanafunzi shule binafsi wanaofeli wastani

Return Of Undertaker

JF-Expert Member
Jun 12, 2012
4,572
26,883


Maswali:

1. Hivi yale madaraja ya division yanapangwa kwa lengo gani?
2 Mbona vyuoni kuna sup na disco au nayo itakuja pigwa marufuku?
3. Mitihani ya darasa la NNE, SABA, FORM TWO, FORM FOUR na Form six itafutwa?

======


Serikali kupitia Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imezitaka shule zote zilizowataka wazazi/walezi kuwahamisha watoto wao kwa kigezo cha kutofikia wastani wa ufaulu, kufuta agizo hilo na kuendelea na wanafunzi hao bila masharti yoyote.

Taarifa iliyotolewa jana kwa vyombo vya habari na Kaimu Kamishna wa Elimu, Nicolas Buretta imeeleza kuwa wazazi wenye wanafunzi waliorudishwa nyumbani kwa sababu hiyo wahakikishe wanawarudisha kwenye shule walizokuwa wakisoma ili waendelee na masomo yao kama kawaida.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Serikali imefikia hatua hiyo baada ya kubainika kuwa bado kuna shule nyingi za msingi na sekondari hususani zisizo za Serikali na zaidi za kidini zinazoendelea kukaririsha, kuhamishia shule nyingine au kuwafukuza wanafunzi kwa kigezo cha kutofikia alama za ufaulu zilizowekwa na shule hizo jambo ambalo ni kinyume cha sheria.

Badala ya shule hizo kuchukua hatua hiyo, wizara hiyo imesema, “...Ziwe na utaratibu wa kuinua viwango vya taaluma kwa wanafunzi wenye ufaulu mdogo na hivyo siyo ruhusa kukaririsha darasa wanafunzi kwa kigezo cha kutofikia wastani wa ufaulu uliowekwa na shule. Ikitokea, ni lazima kufanya hivyo, taratibu zilizopo zifuatwe.”

Taarifa hiyo imeelekeza wadhibiti ubora wa shule, kanda na wilaya, maofisa elimu wa mikoa na wilaya kusimamia utekelezaji wa agizo hilo katika maeneo yao.

“Shule yoyote itakayokiuka maagizo hayo itachukuliwa hatua kali kwa mujibu wa sheria zilizopo.”

Akizungumzia agizo hilo la Serikali, Katibu wa Shirikisho la Wamiliki na Mameneja wa Shule na Vyuo Binafsi Tanzania, (Tamongsco), Benjamin Nkonya amesema wanachama wake hawafukuzi wanafunzi baada ya kushindwa vigezo bali, inaangalia uwezo wake wa kujifunza mambo mawili; ung’amuzi wa kujifunza kwa nadharia na ufundi au mchindo.

“Tukiona mwanafunzi amefeli katika ung’amuzi, mfumo ambao Serikali inauzungumzia, tunampeleka katika mchindo ambao ni ufundi stadi na siyo kuwarudisha nyumbani,” amesema Nkonya.

Amefafanua kwamba, mchindo ni kama chuo cha Veta ambacho dereva asiyejua kusoma na kuandika anakwenda kujifunza na mwishowe anakuwa dereva bora.

Amesema mfumo huo unasaidia kukuza wabunifu hasa katika mapinduzi ya Serikali kuwa nchi ya viwanda.

Hatahivyo, Waziri Kivuli wa Elimu, Suzan Lyimo amesema kinachofanyika kwa mujibu wa agizo hilo ni Serikali kutaka shule za Serikali na binafsi ziwe na mfumo wa utoaji elimu unaofanana jambo ambalo ni gumu.

Ameitaka Serikali iunde mamlaka ya kudhibiti huduma za utoaji wa elimu ili ijiondoe katika usimamizi wa moja kwa moja katika uendeshaji wa sekta hiyo.

Chanzo: Mwananchi
 
Mi naona ni sawa. Utakuta shule inakuwa na mwanafunzi wanakubali karo yake ila ikakaribia mwisho wanasema hatafanya mtihani atafutiwe shule nyingine. Kama wanaona mwanafunzi hafai basi wamuondoe kwenye interview. Siyo anaingia halafu wanakuja kumfukuza na wakati hel yale wamekula.. wakimuondoa kwenye interview atajua la kufanya.
 
Siku zote elimu yetu imekuwa ikichezewa akija huyu anakuja na mawazo yake hakuna muongozo halisi.., kama mwanafunzi hana sifa aaachwe tu ili mwisho wa siku atie aibu kama waleeee baadhi ya wanafunzi wa shule za serikali wanavyochora zombie..., ni nani aliyeliroga taifa hili!!!!!
 
Serikali haina ubavu wa kuzipangia shule binafsi zifanye nn. kuna shule ziliwahi kuburuzwa mahakamani na kushinda kesi baada ya kuwafukuza watt wa vigogo kwasabb walipata alama ambazo ni chini ya wastani waliojipangia, japo kwa vigezo vya kitaifa watt wale walikuwa wamefaulu

shule binafsi huwa zina wasainisha wazazi makubaliano maalumu (mkataba) ambao hukubalika mahakamani.

shule binafs hz zina ada binafsi, mihula binafsi, taratibu binafsi na haya yote wazazi wanayakubali. serikali isimamie shule zake tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…