Serikali kuwatumbua wadaiwa bodi ya mikopo

Ni muhimu taarifa zote za mikopo kwa wanafunzi ziwekwe wazi ili wanufaika waweze ku access taarifa hizo kupitia index number zao kwenye website ya bodi ama taarifa zitumwe kwenye email zao.
Hivi sasa kuna student wanapata allocation ya mkopo but sio pesa zote zinaingizwa kwenye account zao. Kuna loan officers wanachezea pesa za watu. Dr. Ndalichako tunaamini utalimaliza hili, maana kama utaratibu wa utoaji hauko makini basi hata utaratibu wa ulipaji tusitegemee uwe makini.
 
karibia nusu ya wafanyakazi wote tz hawata ruhusiwa kusafiri.
 
Hapa kuna tatizo. Wale waliopewa mkopo kutoka Zanzibar hawadaiwi kwasababu ni wazanzibar, wanapewa bure!!

Walipewa mikopo hiyo kwasababu ya uzanzibar na sasa anayebeba mzigo ni Mtanganyika

Hata wakiambiwa walipe, CAG hana mkono, na wala wizara ya elimu haihusiki huko znz

Hakuna anayeweza kufuatilia nani kaajiriwa wapi huko znz.

Wanafunzi wa znz wanatakiwa kurudisha ZHSLB tu, haya mengine hayawahusu Watanganyika si ndio JMT?
 
kusema mtu ambaye hana kazi maalumu ya kumpa kipato alipe mkopo ni kubwabwaja....wanufaika wengi wa mikopo hii ni watoto wa maskini hawana nyumba hawana shamba hawana kiwanja sasa hizo fedha atazirejesha vipi wakati hana ajira.
Mara ya kwanza mlisema wanufaika wa mkopo ni watoto wa matajiri!
 


SAFI SANA MAGUFULI. HII KITU NIMEKATWA SANA NA MWAJIRI NIKAWA NAHUZUNIKA KWA KUCHEKWA SASA NA MIMI NITACHEKA KIDOGO.

DAWA YA DENI NI KULIPA.
 
Zikirejeshwa fedha zote tulizoobiwa na mafisadi nami nitawapa hilo deni vinginevyo nami ni mgawo wangu wa keki ya taifa kufidia maumivu niliyosababishiwa na mafisadi
 
Hivi kesi za madai wanaona ni kama Maji ya kunywa sio. Haya ngoja tuone. Huruma kwa MAHAKAMA kuendelea kurundikiwa mizigo hisiyostahili.
 
Mzizi wa tatizo ni set up ya Muungano!

Hili tatizo la mikopo kuhusu Wanafunzi wanaotoka Zanzibar ni tawi tu la mzizi wa tatizo.

Huu Muungano wetu kwa karibu unafanana na Muungano wa UK.

Kama ilivyo kwa Watanganyika na Wazanzibar, wanafunzi wa vyuo kutoka Scotland hawana mikopo bali wanapewa education grant lakini wale wa England walidaiwa mikopo ya elimu kwa sababu wanapewa education loan.

Dawa ya muungano wa aina hii siyo serikali mbili, tatu au nne. Dawa yake ni kuuvunja tu ili kila nchi ibebe mzigo wake.
 
Kitu kisichoeleweka ni hiki, wanafunzi wa ZNZ kupitia ZHSLB ni wachache kuliko wanaopewa grant ya HESLB.

SMZ inawakalia kidete warudishe ZHESLB, wakiambiwa warudishe HESLB kama wenzao wa Tanganyika inakuwa nongwa.

SMZ inawakingia kifua hawana uwezo, wakati wana uwezo wa kurudisha ZHESLB.

Kwa maneno mengine wao wana uhalali wa kusoma kupitia migongo ya Watanganyika ambao hawawezi kupata ZHESL hata kwa bahati mbaya kwasababu tu si Wazanzibar

Kupata HESLB lazima uwe mtanzania,wznz wapo, ili upate ZHESB lazima uwe mzanzibar.

Gharama za wananfunzi wa znz,wengi kuliko SMZ inavyodhamini inalipwa na Tanganyika.

Tunasikia wakatwe 8% ya mishahara ili baadaye itoe grant kwa wznz siku za baadaye

Halafu utawasikia wazanzibar wakipiga makelele ya kuonewa na muungano.
Haya hawazungumzi kabisa kwasababu kupata ni haki yao.

Nadhani serikali 3 zinaweza kutoa jibu, kila mmoja ajitahidi kwa upande wake. Panapohitajika nguvu ya pamoja wote wawe washiriki.

Kwanini kusiwe na grant kwa wananchi wa Singida ambao kieleimu wanahitaji msaada!

Yaani grant zetu zinatoka kwa uzanzibar na si kwa kigezo cha uwezo! hili halipo sawa

Nimemsikia waziri makamba akisema wanashughulikia suala ajira na mgao wa benki kuu

Kwasababu za kisiasa watawatwisha Watanganyika mzigo usio na sababu

Ukitoa ajira kwasababu ya muungano, una maana wznz wapate ajira maalumu hata maeneo yasiyo ya muungano.

Hao watakaopata ni wale waliochukua mkopo HESLB bure kwa uzanzibar, upendeleo unaendelea katika ajira. Wanaolipa 8% hawana upendeleo bara na wala visiwani

Akina Makamba wana entertain haya bila kujali ili tu wadumu kisiasa

Kuhusu bank kuu, sioni kwanini wasipewe shea yao.

Huko nako kuna tatizo tusiloliona. ZNZ wanpewa 4% ya pato la Taifa.

Yaani pato la Tanganyika hata kama hawachangii, linasemwa ni shea yao benki kuu.

Piga hesabu za pato la Taifa halafu uangalie ni kiasi gani wanapata ukilinganisha na uchumi wao unavyotoa. Haya hatuyaoni
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…