Serikali kutoa ajira mpya zaidi ya 70,000 kuanzia Julai mwaka huu

Bilionea Asigwa

JF-Expert Member
Sep 21, 2011
16,515
28,493


SERIKALI imesema itaajiri watumishi wa kada mbalimbali 71,496 mwaka wa fedha 2016/17.
Hayo yalisemwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Utumishi na Utawala Bora, Angela Kairuki, wakati akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Mbulu Mjini (CCM), Zacharia Issaay.

Mbunge huyo alihoji kuwa nafasi za watendaji wa vijiji na kata zimekuwa wazi ni kwanini serikali isione umuhimu wa kutoa nafasi kwa vijana waliomaliza vyuo kuanza kujitolea katika kipindi cha mpito ili baadae waingie kwenye mfumo wa ajira.

Kairuki alisema pamoja na ufinyu wa bajeti, serikali katika mwaka ujao wa fedha unaoanza Julai, mwaka huu, itaajiri watumishi wa kada mbalimbali, wakiwamo watendaji wa vijiji na kata ambapo ajira zao zitaanza kutolewa mwezi huu.

"Serikali imekuwa ikipandisha kima cha chini cha mshahara kulingana na uwezo wa bajeti (mapato ya ndani) na kwa kuzingatia gharama za maisha," alisema.

Kairuki alisema maombi ya nafasi za ajira serikalini hufanyika kwa uwazi kupitia bajeti ya serikali ambayo huidhinishwa na Bunge. Alisema nafasi hizo za ajira hutolewa baada ya waajiri kuwasilisha maombi yao serikalini na kuidhinishwa kwa kuzingatia ukomo wa bajeti ya mishahara serikalini.

Source: Nipashe
 
Mkuu kwa nini watu hawana imani na serikali yao??
mara nyingi ahadi zinakuwa hazitekelezeki hasa unapifikia wakati wa kuteleza kuna majibu mengi ya kusababisha ahadi hiyo kutokutelezwa
 
Kwa bajeti ya mwaka 2015/2016 ajira hazijatolewa licha ya bajeti kupangwa. Huyo waziri kujibu hivyo anamaanisha bajeti ipi? Au kwa sababu kila kitu sasa hupangwa na mtu mmoja ndiyo maana bajeti hiyo ya mwaka jana imewekwa mfukoni. Bunge inatakiwa kuisimamia serikali na si kupokea maelekezo ya serikali ifanye hiki na kuacha kile. Bajeti ni muelekezo wa matumizi ya serikali na hivyo inapaswa isimamiwe ili iwanufaishe wote. Sasa kama Bunge kila siku itakuwa ya kupokea amri ya kufanya moja mbili basi itakuwa chombo cha kustarehesha watu fulani tu. Tufike mahala mbunge ajute kubeba bendera ya wananchi kwa namna nafasi yake itakavyokuwa imejaa changamoto za wananchi waliomtuma bungeni.
 
Mkuu kwa nini watu hawana imani na serikali yao??
Haisemi ukweli, yaani kila jambo wao ni wanaharakati wa kupiga porojo tu. Kila siku utasikia wimbo 'tuko mbioni' wakati kila tunaposhiriki olympic watanzania hatuambulii hata medali moja ya shaba. Bwana hawa wanakera sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…