Serikali kujenga daraja la Pili Kigamboni (Magogoni-Kivukoni)

ChoiceVariable

JF-Expert Member
May 23, 2017
58,647
69,269
Serikali ya awamu ya 6 inayoongizwa na Rais Samia ambae ni Suluhu ya matatizo ya Watanzania imekusudia kuanza Ujenzi wa Daraja la Pili linalounganisha Dar es Salaam na Wilaya ya Kigamboni.

Daraja Hilo litajengwa eneo la Kivukoni-Magogoni kuanzia mwaka ujao Kwa kushirikiana na sekta binafsi Kwa utaratibu wa PPP.

Daraja Hilo litakuwa la Pili baada ya like la Kurasini (Nyerere Bridge) lililojengwa awamu ya 4.

Aidha hatua hiyo ni muendelezo wa kusambaza Upendo Kwa Wananchi wa Dar hasa Kigamboni wanaovuka Kwa pantoni.

Ikumbukwe pia Serikali anaenda kupiga daraja refu sana eneo la jangwani Ili kukomesha zile shida za usafiri kutatizika Kwa sababu za kujaa maji.

===

My Take
Heko Samia piga kazi,Mama huna Makelele ila vitendo vyako vinaongea Sauti kubwa sana. Kazi iendelee.

Angalizo: Pamoja na kazi hii nzuri,ila Serikali ielewe kwamba Tanzania hii sio Dar pekee.Mikoa zaidi ya 15 haijaunganishwa na Barabara za lami za Mkoa Kwa Mkoa na Nchi jirani.

Ni vyema Kupeleka maendeleo Kwa uwiano badala ya kupendelea Dar es Salaam pekee.
 
Hii ndio mipango ya kijinga kabisa.
Ni muendelezo ule ule wa miradi ya kipigaji.
Badala ya kumalizia miradi iliyodorora kama Kigogo Busisi, wao wanafiria kuanzisha miradi mipya ambayo kiutekelezaji ni hadithi tupu.

Nini mantiki ya kujenga daraja jipya Kigamboni wakati daraja la kwanza lilishajengwa? La kwanza lilijengwa mahali pasipo sahihi? La kwanza limeshindwa kutatua changamoto za usafiri wa Kigamboni?

Kuhusu daraja la jangwani (ambalo ni hadithi ya kuimbwa karibu kila mwaka na kila serikali), wataalamu walishasema, daraja sio suluhisho kamili, suluhisho kamili liko kwenye kuboresha mikondo wa maji na mito iliyofukiwa pale kwa ujenzi holela wa Dar. Chochote kitakachofanyika Jangwani bila kutatua kiini cha tatizo kinaweza kuzaa tatizo lingine kubwa zaidi maeneo mengine yote jirani. Usipodhiti na kulinda mikondo ya maji ya bonde lote la mto msimbazi ipo siku mafuriko ya Jangwani yatahamia eneo lote la Kariakoo, Magomeni na Upanga
 
Kigongo-Busisi Iko 90% wewe unasema umedorora? Huo mradi unakabidhiwa disemba 2024.

Hiki ni kituko,Unapinga Hadi daraja la jangwani? 😁😁

Sababu za kujenga daraja la Magogoni soma hapo zimeelezwa bayana.
 
Nashauri design ya Ujenzi wa daraja pia ulenge kuweka sehemu za recreational kama restaurant, cafe hata garden.
Kuna daraja Iran Tabiat Bridge imejengwa nchi kavu imepata tuzo nyingi kwa design yake kujumuisha recreational activities .
Huo wa kwetu eneo la bahari itakuwa na kuvutio kubwa sana na kuongeza hadhi ya jiji kiutalii.
 
Unajua cost ya daraja la Nyerere bado hamjalipa NSSF ni 11 trilions.

Non sence na ufikiri wako finyu unafikiri.Daraja sio matundu ya choo
Unaelewa maana ya ubia? Unapopita pale unalipia toll unajua ni kufanya nini kama sio malipo?

Wacha ujinga ,ule mradi una miaka waliyokubaliana kulipa Kwa toll,hata Hilo jingine litakuwa la kulipia pia.
 
Serikali ya awamu ya 6 inayoongizwa na mama wa Taifa Samia S.Hassan Ambae ni Suluhu ya matatizo ya Watanzania imekusudia kuanza Ujenzi wa Daraja la Pili linalounganisha Dar es Salaam na Wilaya ya Kigamboni.

Daraja Hilo litajengwa eneo la Kivukoni-Magogoni kuanzia mwaka ujao Kwa kushirikiana na sekta binafsi Kwa utaratibu wa PPP.

Daraja Hilo litakuwa la Pili baada ya like la Kurasini (Nyerere Bridge) lililojengwa awamu ya 4.

Aidha hatua hiyo ni muendelezo wa kusambaza Upendo Kwa Wananchi wa Dar hasa Kigamboni wanaovuka Kwa pantoni.

Ikumbukwe pia Mama anaenda kupiga daraja refu sana eneo la jangwani Ili kukomesha zile shida za usafiri kutatizika Kwa sababu za kujaa maji.

View: https://www.instagram.com/p/C7i8_A9Nlme/?igsh=MTlsbzdtOTgwZjh1bg==

My Take
Heko Samia piga kazi,Mama huna Makelele ila vitendo vyako vinaongea Sauti kubwa sana.Kazi iendelee.

View: https://www.instagram.com/p/C7jFcBFxMr3/?igsh=cnhlbmkxdHFsOG5l

Angalizo: Pamoja na kazi hii nzuri,ila Serikali ielewe kwamba Tanzania hii sio Dar pekee.Mikoa zaidi ya 15 haijaunganishwa na Barabara za lami za Mkoa Kwa Mkoa na Nchi jirani.

Ni vyema Kupeleka maendeleo Kwa uwiano badala ya kupendelea Dar es Salaam pekee.

Wafanye mpango wa kutanua na mipaka ya mkoa wa Dar ili na siye wengine tuhamie huko tukale keki ya nchi...
 
Back
Top Bottom