Serikali iwaache wachina wafanye biashara Kariakoo: watanzania wameibiwa na kudhulumiwa sana na wale wafanyabiashara wanaojiita wazawa

Sangamwalogesha

JF-Expert Member
Mar 10, 2025
357
373
Baba wa Taifa alituaambia kaburu siyo rangi, hata km we ni mweusi km tabia zako ni za kikaburu za kibaguzi we ni kaburu tu!

Wafanyabiashara wale ni wezi, ni waongo, bei wanazouzia bidhaa ni za dhuluma, kwanini bei yao itofautiane sana na ya wachina. Wachina wale zile bidhaa kule kwao hawapewi bure wananunua, na bado wanasafirisha na kodi zote wanalipa kwanini tofauti kubwa hivyo?

Waache kulialia wanatafuta utajiri wa dhulma wakijua watanzania wengi hawajui bei wanazonunulia kule China au Dubai. Mbona Uingereza wamejaa wahindi na mataifa mengine hata waafrika wanafanya biashara na hakuna huo ubaguzi?

Hao makajanja wamezoea uwizi na kubebwa na bila aibu wanaweza kutisha serikali kugoma, hivi mtu akigoma kwenda shambani kwake unahangaika naye wa nini? Watafungua wenyewe. Mh. Rais usikubali kupotoshwa watanzania siyo wa kuwaendekeza ni wapenda kitonga.

Siyo wachina tu hata mataifa mengine wafanye biashara wachangamke waache uvivu wa kulialia. Waache kuwaibia watanzania tumewachoka, ni makajanja wajanjawajanja
 
serikali inayoruhusu wageni wamiliki njia kuu za uchumi na wageni kufanya biashara za wazawa ni serikali ya kijinga.

Serikali zinazojielewa huwa zinawalinda wafanyabiashara wazawa wa ndani ya nchi kama serikali ya Donald Trump inavyofanya.
 
Baba wa Taifa alituaambia kaburu siyo rangi, hata km we ni mweusi km tabia zako ni za kikaburu za kibaguzi we ni kaburu tu! Wafanyabiashara wale ni wezi, ni waongo, bei wanazouzia bidhaa ni za dhuluma, kwanini bei yao itofautiane sana na ya wachina. Wachina wale zile bidhaa kule kwao hawapewi bure wananunua, na bado wanasafirisha na kodi zote wanalipa kwanini tofauti kubwa hivyo?
Waache kulialia wanatafuta utajiri wa dhulma wakijua watanzania wengi hawajui bei wanazonunulia kule China au Dubai. Mbona Uingereza wamejaa wahindi na mataifa mengine hata waafrika wanafanya biashara na hakuna huo ubaguzi? Hao makajanja wamezoea uwizi na kubebwa na bila aibu wanaweza kutisha serikali kugoma, hivi mtu akigoma kwenda shambani kwake unahanhaika naye ya nini? Watafungua wenyewe. Mh. Rais usikubali kupotoshwa watanzania siyo wa kuwaendekeza ni wapenda kitonga. Siyo wachina tu hata mataifa mengine wafanye biashara wachangamke waache uvivu wa kulialia. Waache kuwaibia watanzania tumewachoka, ni makajanja wajanjawajanja
Wabongo ni wavivu wa kufikiria, hv wanafikiri wa china ni wanyarwanda au warundi wakufukuza tu mpakani kama wanavyofanya kule kigoma, na kagera,? Ao wa china wapo kwa mgongo wa serikali ya china, inayowapa mikopo ma ccm, na sasa hv yakiwagusa tu raia wao, mchina anaminya makende mrudishe mikopo yake ya flyovers zote,
Lakini hv hao wa china ni wangapi? Hawafiki hata 100! Makelele mengi, mbayawenu ni samia na ccm yake
 
serikali inayoruhusu wageni wamiliki njia kuu za uchumi na wageni kufanya biashara za wazawa ni serikali ya kijinga.

Serikali zinazojielewa huwa zinawalinda wafanyabiashara wazawa wa ndani ya nchi kama serikali ya Donald Trump inavyofanya.
Trump mwenyewe anahitaji wawekezaji nchini mwake (mtu hata mwenye mtaji wa Bil2 -3 na mwenye uwezo wa kuajiri wa marekani kuanzia 10 anakaribishwa), wewe kama huna uwezo wa kuwekeza kwenye biashara anayoifanya mchina bado hakuondoi ukweli kuwa kwa wakati husika huna uwezo /mtaji wa hicho wanachokifanya, Sidhani kama ukienda kutafuta eneo la kuanzisha Car Wash mikocheni mwenye eneo ataangalia kama wewe ni mchina au Mtanzania as long as una vibali na una uwezo wa kuilipa kodi yake
 
Back
Top Bottom