SoC04 Serikali iunde Mamlaka Huru ya Usimamizi wa Jeshi la Polisi na maofisa wake ili kusimamia weledi katika kazi

Tanzania Tuitakayo competition threads

ConcH2SO4

New Member
Jun 21, 2024
4
1
UTANGULIZI.
Kwa miaka mingi sasa Jeshi la Polisi limekuwa likilalamikiwa na wananchi pamoja na taasisi mbalimbali zinazojihusisha na haki za binadamu na uhuru wa watu kwamba linajihusisha na vitendo viovu kinyume na miiko na kanuni na miongozo ya kazi Yao.

Jeshi la Polisi limekuwa likituhumiwa kuua, kutesa, unyang’anyi wa mali za watu na kujihusisha na rushwa, kadhalika jeshi la polisi limekuwa likitumiwa na baadhi ya wanasiasa na hata serikali kuwashurutisha wakosoaji kinyume na kanuni na sheria za nchi.

Kwa sasa Polisi anaweza kukamata mtu pasipokufuata utaratibu na asiwajibishwe kisheria kitu kinachopelekea kuminywa kwa haki za wegine na wananchi kupewa mashitaka yasiyo na ukweli.

Ili kuongeza weledi katika jeshi la polisi iundwe mamlaka huru ya usimamizi wa utendaji kazi wa jeshi la polisi itakayotambulika kama “TANZANIA INDEPENDENT POLICING OVERSIGHT AUTHORITY (TIPOA)” itakayokuwa na mamlaka kamili kisheria kusimamia weledi na kuwajibisha jeshi la polisi ama afisa wa polisi pale itakapo thibitika kwamba alitenda kinyume na kanuni na sheria za kazi.

Kupitia mamlaka hii mwananchi yeyote ataweza kuripoti vitendo vya tofauti alivyotendewa na afisa wa polisi ama jeshi la polisi na mamlaka itachunguza, ripoti hizo zitawasilishwa kwa tume kupitia mfumo maalumu wa simu ya kawaida ama kidigitali kupitia programu maalumu ya simu itakayoundwa.

MUUNDO WA TIPOA.
Mapendekezo ya muundo ya TIPOA ni kama ifuatavyo;

Bodi.
Iundwe na wajumbe wasio pungua saba na wasiozidi Kumi ambao watakuwa ni wabobezi wa masuala ya sheria, usimamizi wa sheria, na uchunguzi.
Wajumbe hawa watateuliwa na Rais na kuidhinishwa na Bunge, ambapo Bunge lisipowaridhia italazimu Rais kuteua wengine kwa mujibu wa sheria zitakazotungwa.

Bodi itaongozwa na mwenyekiti ambaye atateuliwa na Bunge baada ya bodi kupitishwa

Bodi itakuwa na jukumu la kuweka mwelekeo wa kimkakati wa Mamlaka,kuunda sera, kusimamia shughuli zake, na kuhakikisha sheria zinafuatwa na kuzingatiwa.

Sekretarieti.
Hiki kitakuwa ni chombo cha uratibu na usimamizi wa shughuri zote za TIPOA kitakachokuwa chini ya mkurugenzi wake atakaye ajiriwa kwa mujibu wa sheria zitakazotungwa,ita simamia shughuli za kila siku za Mamlaka, ikiwa ni pamoja na uchunguzi, ukaguzi, na uhamasishaji wa umma.

Idara.
Napendekeza TIPOA iwe na idara zifuatazo ili kuhakikisha ufanisi kazi katika mamlaka,
  1. Idara ya Uchunguzi: Itasimamia uchunguzi wa vifo na majeraha makubwa yaliyosababishwa na polisi kwa watuhumiwa wakati wakitimiza majukumu yao,itachunguza rushwa,unyanyasaji,pamoja na malalamiko ya kutowajibika kwa polisi.
  2. Idara ya Ukaguzi: Itatekeleza ukaguzi wa vituo vya polisi, vituo vya mafunzo, na vituo vingine vya polisi,ukaguzi wa vitabu vya usajiri wa kesi,utendaji kazi kwa kufuata kanuni za kazi,matumizi sahihi ya silaha na
  3. Idara ya Utafiti na Sera: Itashughulikia masuala yote ya utafiti kuhusu taratibu na sera za polisi, na kuunda mapendekezo ya mageuzi katika jeshi la polisi.
  4. Idara ya Uhamasishaji wa Umma na Malalamiko: itapokea na kushughulikia malalamiko kutoka kwa umma kuhusu kutowajibika kwa polisi, na kuelimisha umma kuhusu mamlaka ya TIPOA,na umuhimu wakufichua taarifa za polisi kwa TIPOA,malalamiko hayo yatawasirishwa kupitia nambari maalumu ya matumizi kwa umma ama programu ya simu itakayoundwa na mamlaka
  5. Idara ya Huduma za mamlaka: Itatiaia usaidizi wa kiutawala kwa Mamlaka, ikiwa ni pamoja na rasilimali watu, fedha, na manunuzi.
  6. Idara ya teknolojia na mawasiliano: hii itahusika na uundwaji wa mifumo ya kompyuta itakayowezesha mamlaka kufanya kazi, na jeshi la polisi kufanya kazi,kufanikisha uchunguzi wa kimtandao kulingana na tuhuma zidi ya jeshi la polisi au afisa wa polisi.
MAJUKUMU YA TIPOA.
  1. Kuchunguza vifo na majeraha makubwa waliyosababishiwa watuhumiwa ama wananchi wakati polisi wakitelekeza majukumu yao: TIPOA itavhunguza matukio yakuimiza ama kuua kulikosabbabishwa na polisi na kutoa mapendekezo Kuhusu hatua Za kuchukua kama hatua za kinidhamu au kushtaki ikiwa inafaa.
  2. Kuchunguza malalamiko ya kutowajibika kwa polisi: Hii inajumuisha tabia yoyote ya maafisa wa polisi inayokiuka sheria au kanuni za polisi kama vile kusimamia usalama pale inapobidi.
  3. Kusimamiza, kukagua na kufanya uchunguzi na hatua zinazochukuliwa na Kitengo cha Mambo ya Ndani ya polisi:Uchunguzi wa mashitaka mbalimbali kwa sasa unafanywa na kitengo cha upelelezi wa jeshi la polisi kilichopo chini ya DCI,kunauwezekano kitengo hichi kutoa ripoti ya uongo kuhusu mashitaka flani,TIPOA itasimamia kitengo cha uchunguzi wa ndani wa jeshi la polisi ili kuhakikisha uchunguzi unafanywa kwa haki na ufanisi. TIPOA watakuwa na mamlaka kisheria kufanya uchunguzi zidi ya kitengo cha uchunguzi na hata kurudia uchunguzi wa mashitaka flani ikiwa hawataridhika na kazi ya ofisi ya DCI.
  4. Kufanya ukaguzi wa vituo vya polisi: Hii itahakikisha kuwa vituo vya polisi, vituo vya kizuizi, na majengo mengine ya polisi yanakidhi viwango vya msingi na kwamba watuhumiwa wanashughulikiwa kulingana na sheria,hii itasaidia pia kuhakikisha kwamba watuhumiwa wanahudumiwa kwa kuzingatia haki zao na mazingira ya kazi kwa askari ni mazuri.
  5. Kusimamia na kuchunguza operesheni na mbinu Zinazotumiwa pamoja na vitendea kazi:TIPOA itachunguza jinsi polisi wanavyofanya operesheni,mbinu na vifaa kazi ili kutambua maeneo yote yanayohitaji maboresho.
  6. Kushughurikia nidhamu ya ndani ya jeshi la polisi: TIPOA itachunguza jinsi jeshi la polisi linavyowachukulia hatua nidhamu maafisa wake kama kutakuwa na ukiukwaji TIPOA iwe na mamlaka kuwajibisha.
  7. Kutoa taarifa: IPOA itachapisha ripoti kuhusu uchunguzi wake kuhusu suala Lolote pia itachapisha ripoti ya mwaka katika tovuti Yankees na kutoa mapendekezo ya mageuzi katika jeshi la polisi.
  8. Kushitaki maofisa wa polisi waliokutwa na hatia katika mahakama.
  9. Kufuatilia maofisa wanaojihusisha na vitendo vya rushwa.

FAIDA ZA TIPOA.
  1. Itahakikisha maofisa wa polisi wanafanya kazi kwa kizingatia miiko na kanuni za kazi.
  2. Itasadia kukabiliana na rushwa katika jeshi la polisi.
  3. Itazuia polisi kujihusisha na siasa ama kutumiwa na wanasiasa kwa manufaa yao binafsi.
  4. Itahakikisha usimamizi bora wa rasilimali Za jeshi.
  5. Itahakikisha maofisa wa polisi wanafanya kazi katika mazingira rafiki.
  6. Itafanya tathimini ya ubora wa jeshi letu.
  7. Itazuia maofisa wa polisi kujihusisha na vitendo vya unyanyasaji kwa wananchi.
  8. Itahakikisha wananchi wanakuwa na sehemu yakuta malalamiko yao zidi ya jeshi la polisi.
  9. Itasaidia maafisa wa polisi kufanya kazi kwa uhuru pasipo kushurutishwa na wanasiasa
 
Back
Top Bottom