SERIKALI ITUKUMBUKE SISI WA AFYA

AG.6851

Member
Jul 31, 2013
97
87
Natoa pongezi kwa serikali namna inavyiendelea na majukumu yake mbalimbali lengo likiwa ni kila mtanzania kufaidika na keki ya Taifa.

Baada ya hayo, niiombe Serikali ya awamu ya tano kupitia Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii ituangalie na kutuhurumia sisi tunaosoma Certificate na Diploma kada ya afya.
Nikizungumzia kwa vyuo vya serikali, tumeona ongezeko La gharama kwa ghafla muhula huu wa masomo 2015/2016 pia tukiambiwa tunajitegemea kwa 100%.
Serikali itambue Wengi wetu tunawategemea wazazi au walezi wetu na hatuna msaada mwingine.

Mara zote Serikali imekuwa ikitoa mkopo na fedha za kujikimu kwa wanaosoma degree tu na ilhali hata sisi wa certificate au Diploma majukumu yetu pengine yakalingana.

Wito wangu kwa Serikali itutupie jicho na sisi tupate angalau hata fedha ya kujikimu, japo Tsh.4000/= kwa siku.

Mlioko huko juu tuteteeni kwani huku maisha magumu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…