Bila shaka yoyote ile kilimo ndiyo sekta inayoweza kuajiri watu wengi zaidi hata kukiko viwanda kama serikali ingetilia mkazo somo la kilimo mashuleni hasa katika secondary
Nimepita katika shule nyingi za kata nimekuta hili somo halipo kabisa nilipo jaribu kuulizia kwa nini somo la kilimo alifundishwi sababu kubwa ni kua walimu wa kufundisha ilo somo hawapo
Sasa najiuliza wataalamu wa kilimo wanapatikana vip kama somo la kilimo alifundishwi mashuleni hasa secondary za kata ambazo ndiyo zilizobeba idadi kubwa ya wanafunzi ambao ndio tunaowategemea waje kusaidia taifa katika nyanja mbalimbali?
Somo la kilimo lingekuwa msaada sana hasa kwa wanafunzi wanao hitimu kidato cha nne na kushindwa kuendelea mbele ingewasaidia kujiajiri na hii ni kutokana na ukweli kwamba somo la kilimo lingeweza kufundishwa kwa vitendo zaidi kuliko nadharia