Serikali inajenga mnara wa babeli haitafanikiwa

mdukuzi

JF-Expert Member
Jan 4, 2014
20,022
49,180
kitabu cha mwanzo 11 na kuendelea kinaelezea jinsi mnara wa babel ulivyokuwa ukijengwa chini ya Nimrod(siyo nimrod mkono) ule ujenzi haukufanikiwa kwa sababu watu wale walikuwa wanaongea lugha tofauti
serikali ya awamu hii haitafankiwa kwa sababu watanzania wanaongea lugha tofauti
kazi ya kwanza aliyotakiwa kufanya bwana Nimrod wetu (narudia sio mkono )ni kuhakikisha watanzania wanaongea lugha moja kwa kutibu vidonda vya uchaguzi na baada ya uchaguzi leo wazanzibari wenewe kwa wenewe wanaongea lugha tofauti,huku bara hali kadhalika,wapinzani na watawala tangu uchaguzi wanaongea lugha tofauti kuna watu wa dini moja wameanza kuongea lugha tofauti wanahisi wanabaguliwa,kuna kanda moja inaongea lugha tofauti inahisi kupendelewa.
tanzania si moja tena lugha zimekuwa nyingi kwa mukhtadha huu mnara wa babeli(nchi ya viwanda)haitafanikiwa mpaka watu wote waongee lugha moja
 
Mnara wa BABEL ulijengwa na UKAWA kwa kumkaribisha Lowasa.Mungu akaubomoa kuanzia kule Zanzibar CUF haikushinda hadi huku bara CHADEMA na LOwasa wakashindwa.Akaamua kuuvunjilia mbali mnara wenu wa babeli mliokuwa mkijenga.
 
Mnara wa BABEL ulijengwa na UKAWA kwa kumkaribisha Lowasa.Mungu akaubomoa kuanzia kule Zanzibar CUF haikushinda hadi huku bara CHADEMA na LOwasa wakashindwa.Akaamua kuuvunjilia mbali mnara wenu wa babeli mliokuwa mkijenga.
kura milioni sita unadhani ni kidogo tena za watu wenye uelewa watu wanaojenga nchi kwa kiasi kikubwa bila hao mnara haujengeki
 
kura milioni sita unadhani ni kidogo tena za watu wenye uelewa watu wanaojenga nchi kwa kiasi kikubwa bila hao mnara haujengeki
Hata mnara wa babeli ulipanda juu sana Lakin ukaporomoshwa chini...!!
 
I think YEHODAYA is right kwa sababu vijisent siyo fisadi ndo maana kapewa uenyekiti wa bunge; na Escrow account bado iko BOT na walisema zimeondolewa waongo. Hata wale wa Mkombozi nao waongo; mapilato wale wanaodaiwa kuvuta wanasingiziwa tu kwa sababu ya wivu wa kike . Hata yule kunani msaidizi wa jimbo na wasaidizi wake nao wamesingiziwa tu kisa? Wivu wa kike. Acheni kabisa hayo. Sinai ni wasafi. Lila nyie Babel yenu UKAWA kwishine. Mlie tu. Nani anabisha?
 
Tanzania nchi ya ajabu sana duniani kwa sababu kila kitu ni siasa. Leo nimepita dukani kununua vocha ya simu nimekuta mwenye duka ana gunia zima la sukari tena ile nzuri ya TPC anabembeleza watu kununua nikikumbuka vizuri juzi juzi tu watu hawa hawa walikuwa wanamtusi Rais wetu na kumsema ameshindwa kazi sababu ya kukosekana sukari sasa leo haina hata mnunuaji. Shemaa Tanzania na siasa zake uchwara mara Babeli, mara plasta midomoni basi ili mradi kila mtu ni mjuaji
 
kilo ya sukari umeuziwa kwa sh ngapi mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…