Serikali ikifute chuo cha Chimala

Kizibo255

JF-Expert Member
Jan 4, 2011
510
368
Hiki chuo kinatoa mafunzo ya wahudumu wa afya(Medical Attendants), ndicho chuo kinachoongoza kwa kuuza vyeti kwa watu bila hata kupata mafunzo katika chuo hicho then watu hao ndio wanaenda kutoa huduma katika mahospitali, zahanati na vituo vya kutolea huduma za afya.

Yaani mtu amefeli kidato cha 4 baada ya miaka miwili unakuta ni mhudumu wa afya ktk hospitali, zahanati au kituo cha afya huku wenzie waliofaulu wakiendelea kuumia masomoni(vyuoni au A level).

Tafadhali wahusika walifanyie kazi suala hili pamoja na vyuo vingine vya aina hii. Pia wana JF tuwasaidie wahusika kwa kuvitaja vyuo vya aina hii.
Nawasilisha
 
Taarifa Yako Haija Jitosheleza Kwahiyo Haiwezi Kuwekwa Katika File La Kufanyiwa Investigation!
Hebu Weka Wazi ili Tupate Vizibiti vya Kuaminika Kama Kweli Unayodai ni Ukweli Mtupu! Usiogope Utakapoeka Wazi Manyago Yanayofanywa Hapo na ikithibiti kuwa ni Kweli, basi umeshaokoa taifa.
 
Taarifa ya huyo Jamaa haitakiwi kubezwa hata kidogo, chuo cha nursing chimala ni jipu kubwa , wahitim wanaotoka pale hawana ujuzi hata kidogo, halafu kina magumashi balaa, I,e kuuza vyeti KWA watu ambao hawajapata mafunzo ya nursing hata abc hawana lakini anamiliki cheti kutoka chimala
 
Unatka nini ili niongeze (km ninakifahamu)
 
Nashangaa mkuu watu wengine hofyo kabisa. Ngoja waje wawachome sindano za jicho ndo watajua ninacomaanisha
 
Hao unawaita medical attendance kwa uhalisia ni medical assistance. Hata katika nchi zilizoendelea wapo na wanafanya kazi kwenye mahospitali makubwa. Wanafanya kazi nyingi ambazo daktari alitakiwa kuzifanya kama kutafuta veins kwa mgonjwa, kuchukua blood culture na vitu vingine vingi. Hii course haiwezi kufutwa inaweza kuboreshwa zaidi ili na wapewe majukumu mengi zaidi.
 
hicho chuo kipo mbeya ktk wilaya mbalali ..kimeanza kupigiwa kelele muda mrefu sana ..na kilisha wahi fungiwa na mamlaka husika , sasa cjui kama kimeboreshwa au lah ..maana bado kinatoa mafunzo kama kawa ...
 
hicho chuo kipo mbeya ktk wilaya mbalali ..kimeanza kupigiwa kelele muda mrefu sana ..na kilisha wahi fungiwa na mamlaka husika , sasa cjui kama kimeboreshwa au lah ..maana bado kinatoa mafunzo kama kawa ...
Labda kwa serikali hii
 
jamani chimala nursing ni uozooooo msiweke masihara kumbukeni hawa wanahusika na maisha ya watu sisi tulio nyanda za juu kusini sio wageni na hiki chuoo
 
Chimala ni chuo za zamani sana kinachukua darasa la7 na waliopata dv 0 ya iv ila sijui huwa wanapata wapi vyeti maana utawakuta wapo kwenye hsptar kubwa tu. Wizara ya afya inakazi ngumu maana mafeki yamejaa sana.
 
Polee,dogo una wivu...na ninakwambia ukiendelea na huo wivu wako hutoboi ng'o,mfano ni baba mdogo yangu ana miaka40 amejikatia Tamaa ya maisha
 
Polee,dogo una wivu...na ninakwambia ukiendelea na huo wivu wako hutoboi ng'o,mfano ni baba mdogo yangu ana miaka40 amejikatia Tamaa ya maisha
Hopeless kabisa. Nina kazi yangu nineajiriwa serkalini mshahara unanitosha miradi inaenda bila shida. Wivu!!!!!????? Mini!!!!!!????????
 
Mnaomponda huyo jamaa ni walewale mnaopenda shortcut..ipo siku mtakutana nao ndo mtaelewa shortcuts hazifai..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…