jingalao
JF-Expert Member
- Oct 12, 2011
- 35,951
- 29,533
Moja ya watu wasumbufu katika masoko ni wale wanaomiliki vizimba zaidi ya kimoja na kuwapangishia wafanyabiashara wengine. Hii husababisha migogoro mingi.
Kwa mfano, soko lenye vizimba 100 linaweza kuwa na madalali, wahuni au wanasiasa wawili au watatu wanaomiliki vizimba 30 hadi 40, ambavyo wanavikodisha kwa wafanyabiashara. Hawa ndio chanzo cha migogoro masokoni.
Pendekezo langu ni kwamba, kuanzia Julai mosi, kizimba kimoja kiwe na mmiliki mmoja tu. Hii ina maana mtu anayeweza kumiliki vizimba 30 kwa kulipia Tsh 100,000 kwa serikali, halafu yeye anavipangisha kwa Tsh 600,000, na bado anatamba mjini huku akileta taharuki, atapunguzwa.
Ikibidi sheria itungwe ili umiliki wa vizimba uwe na uwiano wa 1:1. Kama mfanyabiashara ana hela nyingi, anaweza kumiliki vizimba maeneo mengine kwa utaratibu wa kizimba kimoja kwa kila soko.
KWA HISANI YA MTU WA TANZANIA!