chiembe
JF-Expert Member
- May 16, 2015
- 16,225
- 27,382
Halmashauri ya Wilaya ya Chato, wakati Joseph Pombe Magufuli akiwa Rais, waligawa maelfu ya viwanja kwa viongozi wakuu wa Serikali, watumishi wa Umma, binafsi, na wafanyabiashara.
Lakini tangu Magufuli afariki, wamevitelekeza, havijajengwa, na hata hawavitembelei. Yamekuwa mapori makubwa yanayoweza kulisha makundi hata 100 ya tembo.
Baadhi walioanza kujenga gesti na hoteli kwa ajili ya wageni wanaokuja kumuona Magufuli, nao wameacha magofu na kutokomea kusikojulikana.
Naomba Serikali iingilie kati. Wakati wa Magufuli viwanja vilipanda bei vikawa havishikiki, lakini sasa hivi, mtu anamtafuta wa kumuuzia hampati.