Black poison The Factor
JF-Expert Member
- May 31, 2020
- 1,440
- 2,053
Kutokana na wimbi la uhalifu kuongezeka mitaani huku chanzo kikiwa ni ukosefu wa ajira pamoja na elimu stahiki nashauri serikali ianzishe veta kwenye magereza.
Wakianzisha veta pale magereza wafungwa pamoja na mahabusu wote iwe ni lazima kusomea chochote, na kama kuna mtu ambaye ana elimu Fulani basi awe mwalimu palepale.
Kwamfano mtu amehukumiwa miaka mitano jela, basi ni vyema asomee chochote pale ndani alafu zile bidhaa wanazozitengeneza, zikiuzwa ile faida iwe inawekwa fungu pembeni ili mtuhumiwa siku akimaliza kifungo wanamnunulia vifaa vya kazi.
Maana yake wakirudi mtaani watakua ni watu wenye ajira rasmi kutokana na alichosomea, pamoja na kua na vitendea kazi vyake.
Naamini huu mfumo ukianzishwa baada ya miaka kumi mbele watu wengi watakua wana ajira zao.