SERIKALI IANGALIE MBADALA WA BOMOA BOMOA

Criterion

JF-Expert Member
Jan 8, 2008
11,797
11,890
Tanzanai ilibahatika kusomesha wataalamu katika fani mbali mbali muhimu hapo awali. Inao watu wenye weledi wa hali ya juu, wenye uzalendo, uadilifu, uaminifu na nia thabiti ya kujeng ataifa la Watanzania kwa ajilily ya Watanzania wa leo na vizazi vyao. Bahati mbaya serikali ya ccm kwa hila na ubaradhuli wake, imepoteza dira na kudharau taaluma za watu, na badala yake kuendekeza rushwa na ufisai kaisi cha kukanyaga kila jema ili mradi kuna milango ya ufisadi.

Leo tunaona bomoabomoa ikiendeshwa ki katiili na kiuonezi kwa misingi ya kutokuangalia asili ya utendaji kosa katika ujengi huo. Serikali iliwapa watu vibali halali wakajenga, sriakli iliwapelekea miundo mbinu kama maji na umeme, masoko n.k na ikakusanya kodi husika kutika kwa hawa watu. Serikali ikachukua kodi za majengo mengine makubwa na mengine madogo ili mradi kila wakati ilijipatia fedha kutoka kwa wadau hawa. Hivi mtu binafsi amekwenda ofisi za srikali, amemilikiswa eeno lile kihalali, amejenga na serikali imeendlea kujichumia haki zake kwa mtu yule, leo inapomvujia nyumba kwamba alijenga kimakosa. Ni ki makosa ya nani? Huy mjennzi anahukumiwa kwamba nyumba ibomolewe bila fidia, halafu akalale mitaroni na watoto watke, serikali liyompa support wakati wote wa ujenzi na utumiaji wa mahala pale, inaadhibiwa kwa utaratibu gani? Inatoa mchango gani kama adhabu ya makosa yake? Hapo si sahihi. Serikai inajiundia maadui pasipo sababu kwa ajili tu ya maamuzi ya papara na kujitakie sifa juu ya msingi w auharibifu ilyouasisi yenyewe.


Ushauri wangu:-

Serikali isiwakomoe raia as if kujenga nyumba ni dhambi. Serikali iache kujipendekeza kwa maskini kwa kuwapa kichwa kwamba wajione wao kutokuwa na nyumba nidyo faraja kwa kuw ahata waliokuwa nazo wanabomolewa. Hapa ni mwendelezo wa dhana ya kushusha elimu ili Tanzanai iwe na majuha wengi an majuha wafarijike kwa kuwa majuha ni wengi. Sserikali iache kufanya kazi hii bila weledi ila kwa kutafuta sifa.


Pili, ardhi ya Tanzania ni mali y asrikali. Inawapa watu kumilki ardhi kwa mikataba ya miaka kadhaa na inauwezo wa kikatiba kubadilisha matumzi ya ardhi wakati wowote. Kwa kutumia dhana hii, serikali ifanye uchambuzi kwa kuona ni kwa kiasi gani ramani na mipango ya matumizi ya ardhi imekikuwa hadi sasa. Iangalie thamani ya miundo mbinu ilyowekwa kwenye maeneo yasiyostahili kwa uchumi wa taifa na maisha ya Wananchi kwa ujumla. Ifanye cost benefit analysis ya kuvunja vunja ki kipofu bila kuajli, na kukaa chini kuangalia njia mbadala.

Njia mbadala ni pamoja na ku redesign ramani za majiji/miji, ili kuzuia uharibifu na gharama kubwa ya kuvnja vunja. Ku reallocate maeneo mapya kwa kuw abado tuna ample land ambayo inaweza kutumika kwa mambo yaliyofunikwa. Kuondoa ujenzi holela wa skwata kati kati ya miji kwa fidia na kuwapa wamiliki wa hivyo vitu maeneo mapya kwa mashrti maalumu kunaweza kupunguza gharama kwa serikali, kupungua uadui kati ya watu na serikali yao, kuhakikisha miundo mbinu na usafiri, maji, nishati na huduma za jamii zinakuwa conviniently accessible na watu wote, upanuzi wa miji na kuondoa misongamano isiyo sababu.

Ni zoezi linaloweza kuchukua muda na umakini lakini likafanyika kwa amani bila athari kubwa kwa serikali na watu wake. Ninachelea lisije hili likaishia kama operation vijiji ya kawawa 1974 ambapo watu wengi walliliwa na simba, nyumba zikachomwa moto wakabaki maskini na matokeo yake leo ni umaskini uliokithiri vijijini huku watu wakirudi kule walikoondolewa.

Hii bomoa bomoa ka am inalenga kusafisha miji na kufanya mipangilio mizuri kwa ustawi wa Wanchi, inaweza kufanyika vizuri sana kwa ushirikishwaiji wa wananchi, upangilijai mpya wa ramani za majiji kufuata hali iliyopo. Kusafisha makazi duni na kutengeneza mfumo sahihi kitu ambacho kinaweza kuwagusa watu wachache miongni wa wamiliki wa makazi duni huku wanaosalia wakipwa msharti ya kujenga nyumba bora na wanaoodolewa wakipewa fidia ambayo ni obvious ni ndogo na kutengenezewa maeneo mengine mbadala kwa masharti ya kukidhi viwango vy aujenzi katika maeneo yale.

Miji mingi ukiukwaji uliofanywa na serikali katika utoaji wa hati, uemfawanya watu kuenga majengo ya maana makubwa na vitga uchumi safi katika maeneo yanayofakiwa kuvunjwa sasa huku, maeneo yaliyofanywa kw aujenzi holela yakiachwa bila kuona kwamba ni hatari pia kwa afya na usalama wa watumiaji maeneo yale.

Ni vyema sasa serikali ikaacha kutumia ramani ilizozivuruga yenyewe, kuwavujia watu majengo waliyoyajenga kw gharama kubwa na kusababisha taharuki an uadui. Badala yake i review mipango miji, itengeneze ramani mpya iondoe vibanda kwwenye maeneo ya skwata kw afidia ndogo, ili miji iwe salama na ya kupendeza.

Ukivunja vibanda 50 ukalipa fidia za vibanda vile, ni nafuu kuliko kuvunjwa mahoteli ambayo si kwamba tu utafrusrate owners bali pia, ajira, huduma za jamii, na mapato ya kodi za serikali. Lakini pia ukibakiza haya majumba mazuri, na makubwa utabakiza miundo mbizu bora katika jamii badala ya kung'an'gnia kuyavunja kwa ramani ya kale ambayo serikali ndiyo iliivuruga kwa uzembe wake, hku mkiacha vibanda umiza eti kwa kuwa havikuvamia maeneo na kuendeleza uchafuzi wa miji na ujenzi holela.

Na kuanzia hapa, upimaji na ramani wahakikishe wamepima maneo yote kwa mahitaji ya mipango miji ili kuiswe na ujenzi wa holela. Mtu kaitaka kujenga makazi, duka viwanda ama garage, aonyeshwe eneo lilokwisha kupimwa yeya shughulikie hati na ajenge kinachohitakiwa kwa kiwango sahihil.

Hii biashara y akungojea watu wajenge ndipo wakapimiwe ni ulaghi na utapeli. Serikali imajiri upimaji na ramani na mipango miji na wanlipwa kodi za wananchi kila mwezi kwa ajira hizo lakini hawapimi maeneo hadi mtu ajijengeee na akitaka kupimiwa awalipe fedha. Hii ni nini? Hapa ndipo kwenye mwazo wa shida.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…