Serbia paa la kituo cha Treni limeangua aliyekuwa Waziri kakamatwa na kushtakiwa, Tanzania kilijengwa kituo cha Mabasi Jangwani aliyekuwa Waziri kawa

Lord denning

JF-Expert Member
Jun 3, 2015
14,327
29,351
Uwajibikaji na kuwajibishana ni moja ya nguzo kubwa sana ya maendeleo.

Huko Serbia aliyekuwa Waziri wa Ujenzi wakati wa Ujenzi wa Kituo cha Treni amekamatwa na kushtakiwa baada ya paa la kituo hicho kuanguka.

Tanzania tunakumbuka aliyekuwa Waziri wa Ujenzi wakati wa Ujenzi wa kituo cha Mabasi ya Mwendokasi kasi kilichojengwa kwenye eneo la Mafuriko jangwani na kupelekea kuharibika kwa magari mengi yaliyokuwa yanapakiwa kwenye eneo hilo alikuja kupitishwa na chama cha mapinduzi kuwa mgombea wa Urais na baadae alikuja kuwa Rais wa Tanzania wa Awamu ya Tano.

Kwa hali hii acha tu tuendelee kushangaa mafanikio ya wazungu!
Screenshot_20241231_143643_YouTube.jpg
 
View attachment 3189397
Wewe una ujinga wa aina fulani na chuki binafsi na JPM.

Kwani kipindi JPM akiwa ni waziri wa ujenzi nani alikuwa ni rais?

Waziri alipendekeza kituo kiwe Magomeni mapipa lakini wakubwa wake wakang'ang'ania kiwe hapo Jangwani kwenye mto Msimbazi halafu bila aibu unaibuka kumlaumu JPM hizo ni akili za mfu.

JPM alikufanya kitu mbaya, alipofariki tu ukajifanya kujisogeza kwa aliyepo lakini matarajio yako yakapotea hivi sasa unamponda kwa siri bila kumtaja huku ukurusha madongo kwa JPM.

Ungekuwa mtu wa maana ungemtaja JKM
 
Ujinga upi?

Chuki gani dhidi ya JPM? Kutumia uhuru wangu wa kutoa maoni kumeanza lini kuwa chuki dhidi ya JPM?

Tupe ushahidi kuhusu yeye JPM kutaka kituo cha Mwendokasi kujengwa Jangwani?

Tupe ushahidi pia ya hao wakubwa waliokataa?
 
Sisi Huku Samia anawaambia wateule wake kuleni rushwa Kwa urefu wa kwamba zenu
Mkuu, ile video ni ya kweli au ya kutengeneza?? Kama ni ya kweli, nilisikitika sana siku ile..

Alafu kuna siku nilimsikia akisema, "tusiisahau Zanzibar yetu" akiwa Zanzibar katika uzinduzi mpaka nikawa ninajiuliza, hivi huyu ni Rais wa Zanzibar au wa Jamuhuri ya Muungano??..
 
Wewe una ujinga wa aina fulani na chuki binafsi na JPM.

Kwani kipindi JPM akiwa ni waziri wa ujenzi nani alikuwa ni rais?

Waziri alipendekeza kituo kiwe Magomeni mapipa lakini wakubwa wake wakang'ang'ania kiwe hapo Jangwani kwenye mto Msimbazi halafu bila aibu unaibuka kumlaumu JPM hizo ni akili za mfu.

JPM alikufanya kitu mbaya, alipofariki tu ukajifanya kujisogeza kwa aliyepo lakini matarajio yako yakapotea hivi sasa unamponda kwa siri bila kumtaja huku ukurusha madongo kwa JPM.

Ungekuwa mtu wa maana ungemtaja JKM
Ulisikia statement ya mama Tibaijuka??
 
Sisi Huku Samia anawaambia wateule wake kuleni rushwa Kwa urefu wa kwamba zenu
Watanzania hatuna pa kukimbilia, maana ni afadhali na ccm kuliko chadema ambako mwenyekiti ndiyo anayefanya michongo ya rushwa.
 
Hizi ni fikra mgando tu!

Nchi itaendelea na itapata maendeleo yasiyoelezeka hao CCM wakiondoka madarakani.
 
Imagine ccm wameondoka halafu nchinimeshikwa na mpiga dili Mbowe!!!. Mlima Kilimanjaro asubuhi tu unakuwa ushauzwa.
 
Hizi ni fikra mgando tu!

Nchi itaendelea na itapata maendeleo
Kwasasa hamna chama pinzani kinachotoa matumaini ya kulifikisha hili taifa panapostaili , acha tu haohao CCM waongoze mpaka wapinzani watakapokuwa stable.

Tutajikokota hivohivo kwa kupigizana kelele.
 
Uwajibikaji na kuwajibishana ni moja ya nguzo kubwa sana ya maendeleo.

Huko Serbia aliyekuwa Waziri wa Ujenzi wakati wa Ujenzi wa Kituo cha Treni amekamatwa na kushtakiwa baada ya paa la kituo hicho kuanguka.

Tanzania tunakumbuka aliyekuwa Waziri wa Ujenzi wakati wa Ujenzi wa kituo cha Mabasi ya Mwendokasi kasi kilichojengwa kwenye eneo la Mafuriko jangwani na kupelekea kuharibika kwa magari mengi yaliyokuwa yanapakiwa kwenye eneo hilo alikuja kupitishwa na chama cha mapinduzi kuwa mgombea wa Urais na baadae alikuja kuwa Rais wa Tanzania wa Awamu ya Tano.

Kwa hali hii acha tu tuendelee kushangaa mafanikio ya wazungu!
View attachment 3189397
Bongo, wangeunda tume na hakuna chochote kinachofanyika Tena Baada ya hapo.
 
Back
Top Bottom