last king of uscoch
JF-Expert Member
- Mar 21, 2015
- 2,728
- 3,980
Sera ya utolewaji wa elimu bure mashuleni kuanzia darasa la kwanza hadi kidato cha nne ilianza kutelelezwa rasmi kuanzia mwaka 2015,Pale mheshimiwa Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Hayati Dr.J.P.Magufuli alipotoa tamko.
Baada ya tamko hilo wananchi wakaambiwa kuwa hakutakuwa na michango tena mashuleni,badala yake serikali itagharamia gharama zote zihusuzo elimu kwa madarasa husika.Na kweli kwa kipindi kile alijitahidi kwa kiasi chake,wazazi hawakusumbuliwa na hata pesa ya mzazi kuhusu masuala ya elimu ikawa inaogopwa sana.
Sasa ile michango ya mashuleni imerudi upya,pasipo kutujulisha ya kwamba ni sera imebadilika au ni ukiukwaji wa tamko la awali,Kuna shule wazazi wanachangishwa hadi 100k kwa mwaka kwa mtoto wa shule ya msingi ukiondoa mahindi na maharage,Mbaya zaidi watoto wanarudishwa mashuleni wakawalete wazazi tena kwa viboko.
Hatukatai kuwa maendeleo ya elimu yanahitaji gharama kubwa lakini serikali ituambie wazazi kama michango imerudi shuleni? Kwa sababu kwa shule za msingi watoto wanachangia hadi ream of paper,hela ya waalimu wa kujitolea kwa lazima na mtoto kama hana anafukuzwa kwa viboko.
Wakuu nimelileta kwenu hili ili tu nipate kujua hii sera imekaaje? Huu utaratibu umerudi wa awali au ni watu wanavunja sheria