Sensa, RITA na NIDA; ndugu wasiofanana

kevylameck

Member
Nov 3, 2013
18
19
Na Kevin Lameck.

Hisia mseto zimekuwapo kuhusu Zoezi la Sensa ya watu na makazi litakalofanyika jumanne ya August 23/2022. Takribani mwezi mmoja baadae kutokea leo.

Watanzania Wengine wanaona ni upotevu tu wa fedha, wengine wakiamini Sensa haina maana katika maendeleo ya kijamii.

Baadhi ya watu wanaamini kuwa kama ni takwimu za idadi ya watu basi zichukuliwe kutoka mamlaka mbili kubwa; RITA pamoja na NIDA.

Licha ya kuwa SENSA,RITA na NIDA kuwa ndugu wa kufanana kutokana na kushughulika na Takwimu na taarifa, ipo tofauti ya kimfumo,kiutendaji na kiuendeshaji kutokana malengo yake, madodoso na taarifa wanazozikusanya katika Ofisi zao.

Ili kufahamu tofauti ya Sensa,Rekodi katika Vitambulisho vya NIDA ama rekodi zinazokusanywa na RITA fuatilia maswali yatakayoulizwa wakati wa Sensa ya mwezi ujao;

- Zitaulizwa taarifa za Kidemografia kwa maana ya Umri, Jinsi, uhusiano, hali ya ndoa, uraia na kadhalika.

- Yataulizwa maswali yanayohusu Ulemavu.

- Zitaulizwa taarifa za elimu na viwango vya elimu tulizonazo.

- Yataulizwa maswali ya uhamaji pamoja na taarifa za watanzania ndugu zetu wanaoishi nje ya Nchi.

- Yataulizwa maswali kuhusu umiliki wa nyaraka za kitaifa kama vitambulisho vya NIDA, Mzanzibari Mkazi, cheti cha kuzaliwa, hati ya kusafiria na leseni ya udereva.

- Makarani wa Sensa watauliza pia maswali kuhusu shughuli za kiuchumi.

- Umiliki wa ardhi na taarifa za TEHAMA.

- Taarifa za Uzazi na vifo vilivyotokea ndani ya kaya.

- Vifo vitokanavyo na Uzazi.

- Hali ya nyumba za kuishi na umiliki wa rasilimali mbalimbali.

- Maswali ya mifugo na kilimo.

-na Mifuko ya hifadhi ya Jamii.

Kwa sifa na utofauti huo ni wazi kuwa zoezi la sensa ya watu na makazi ni zoezi kubwa zaidi kutokana na wingi wa taarifa ambazo Ofisi ya Takwimu itakazokuwa inazihitaji kutoka kwako.

RITA wao ni wakala wa serikali ambao umeundwa kutoka iliyokuwa idara ya kabidhi wasii Mkuu ambayo hujulikana sana kama vizazi na vifo.

Kazi yake kubwa ni kusajili tu vizazi na vifo na kutoa leseni kwa vizazi na vifo, kutayarisha takwimu za vizazi na vifo na kusajili ndoa na kutoa nakala za shahada za Ndoa.

Wajibu wa kuandikisha kizazi ni kwa wazazi ama walezi. Wajibu wa kuandikisha kifo ni wa jamaa wa marehemu ambaye kifo cha nduguye kimetokea akiwepo.

Licha ya kuwa ni kosa la jinai chini ya sheria ya uandikishaji wa vizazi na vifo, taarifa za mamlaka hii zinasema bado kuna changamoto kubwa ya watu kutojiandikisha kwao pale panapotokea uzazi au Kifo.

NIDA Yenyewe ni mamlaka ya vitambulisho vya Taifa (National Identification Authority). NIDA inatoa vitambulisho vya aina tatu, ambavyo ni kitambulisho cha raia, kitambulisho cha mgeni mkaazi, na kitambulisho cha mkimbizi.

Vitambulisho vya Taifa vilianza kutolewa Februari 2013 baada ya Rais Jakaya Kikwete kuzindua mpango huo na kusema vinatakiwa kutumika kwa miaka kumi kabla ya kuhuishwa kwake.


Tofauti na zoezi la Sensa lilivyo, NIDA haihusiki kabisa na kukusanya takwimu za Vifo na Uzazi,hali za kiuchumi au viwango vya elimu zetu na hali za makazi.

Kwa Uzoefu, NIDA hutaka kufahamu tu majina yako,Umri,Jinsia na mahali ulipozaliwa na ni vitambulisho ambavyo kazi yake kubwa ni kukutambua tu Kama Raia au Mgeni unayeishi nchini Tanzania.

Changamoto kubwa ya utendaji wa NIDA ni pamoja na kushindwa kuwapatia vitambulisho watanzania wengi kama ilivyokuwa inatarajiwa awali.

Watanzania wengi pia hawakuandikishwa wakati zoezi hili linafanyika na hata kwa walioandikishwa wengi wao hawajawahi kupata vitambulisho vyao. Wapo pia waliofariki baada ya kupata vitambulisho vyao,na wengine wamezaliwa baada ya zoezi lile kufanyika.

Rais wetu kipenzi Mama Samia Suluhu Hassan anasema "Ushujaa ni Kusensabika". Shime watanzania tushiriki katika zoezi la sensa ya watu na makazi.

Sensa inaharakisha Maendeleo yetu.Jiandae Kuhesabiwa
 
Back
Top Bottom