Sekta ya utalii inatoa mianya ya kufanya na kufanyiwa ujasusi. Tuzibe mianya hiyo sasa na tuitumie sekta hii kwa manufaa ya taifa

Lidafo

JF-Expert Member
Sep 26, 2019
864
1,696
Usalama wa taifa ni muhimu kwa maendeleo ya taifa lolote duniani, Hii inajumuisha usalama wa ndani ya nchi na nje ya nchi ambapo wote kwa Pamoja unajumuisha ujasusi wa kiuchumi, Kisiasa na kijamii. Nchi isipokuwa salama matokeo yake huonekana moja kwa moja kwa raia wake hivyo suala la usalama wa taifa sio suala la kuchukilia mzaha hata kidogo.
Nitajikita kuelezea eneo moja la utalii ambalo kama taifa inabidi kuwa ama kuongeza umakini ili kuzuia kufanyiwa ujasusi ambao madhara yake tunaweza tusiyaone sasa ila baada ya miaka 10 na kuendelea au kizazi kijacho kikakumbana na matatizo ambayo yamesababishwa na sisi kutokuwa makini.
Eneo hili sio tu tulitumie ili kuziba mianya ya taifa letu kufanyiwa ujasusi na mataifa ya nje bali pia sisi wenyewe tulitumie kuimarisha usalama wa taifa letu.

Sekta ya utalii hii ni sekta ambayo tunapaswa kama taifa kuiangalia kwa jicho la karibu kwani ni katika sekta zinazotoa nafasi ya taifa letu kuchangamana na mataifa ya kigeni kwa ukaribu, Katika hao watalii huenda kukawa na majasusi kwa ajili ya ku collect data and other info, Inashangaza kutokuwa na utaratibu mzuri kama taifa la ku monitor watalii walipo na wanachofanya nitatoa mfano mdogo, Tuna kambi nyingi za kijeshi ambazo zipo karibu na maeneo ya barabara ambapo ni rahisi mtu kupita nje na kusoma mazingira na kujua jiografia ya kambi zetu za kijeshi, Je serikali haioni kutokuwa na mfumo mzuri wa kumonitor watalii kunaacha mwanya wa sisi kama taifa kufanyiwa espionage?
Tunapenda tukuwe katika sekta ya utalii lakini ukuwaji huo uwendane na uboreshaji wa usalama kw taifa letu. Leo dunia inapambana kiuchumi, Kama nchi tuna jukumu la kufanya research za kutosha kujua maeneo yote potential ambayo yataweza kutusaidia kukua kiuchumi, Itakuwa ni jambo la ajaabu sana wazungu kuja kugundua maeneo potential katika nchi yetu na sisi tukiwa tupo tu na tunajisifu tunawataalamu.

Lakini pia sekta ya utalii kwa asili yake inatoa fursa kwa wageni kufahamu rasilimali zetu kama misitu, Wanyama n.k Hii ni hatari kiusalama kwani hupelekea wanyama wetu kuibiwa na kusafirishwa embu fikiria kesi za kusafirishwa Wanyamapori unadhani yale yanatokea kwa bahati mbaya? Nilazima tujizatiti kiusalama ili kutoruhusu haya yote.
Watalii wanapokuja nchini mwetu ni lazima tuwe na sera nzuri za kiusalama sio tuwaone wanazagaazagaa mtaani. Kama anakibali cha kuja kutalii Serengeti basi tumkute Serengeti na sio yupo Dodoma ana randaranda mitaani au monduli – Arusha anazunguka ovyo ili ni jambo hatari kwa usalama wa taifa ni hatari kiuchumi, kisiasa na kijamii.
Katika swala la ku control watalii ni vyema serikali ikaanzia mpango mkakati katika viwanja vyetu vya ndege huko waweke maafisa wa usalama wenye weledi ili watusaidie katika usalama wa nchi yetu, Pia katika mbuga za wanyama na hifadhi za taifa wawepo maafisa usalama .

NI JINSI GANI TUTAWEZA WATUMIA WATALII KWA FAIDA ZA KIJASUSI KWA TAIFA LETU ?

Kwa kuwa utalii unaruhusu mataifa ya kigeni kuja nchni mwetu, Hii ni fursa kwa sisi kuwatumia watalii hao kupata taarifa zinazo husu nchi zao tarifa ambazo zitatusaidia sisi kijasusi, Kujua mambo mengi na sio tu kutegemea taarifa za balozi zetu zilizopo ugenini, Unajua raia halisi wa nchni mwake anaweza kuwa na deep information ambazo zina faida kubwa kijasusi hivyo ni nafasi yetu sisi kuwatumia na hata kuwa convince wengine wawe spy kwa ajili ya mafuaa kwa nchi yetu. Hili linawezekana kama tutaamua kujiimarisha haswa katika maswala haya ya ulinzi kwa taifa.

Mwisho niseme kwamba tumekuwa na matukio mengi na mambo mengi ambayo yanaashiria udhaifu katika maswala ya kijasusi hasa katika ujasusi wa kiuchumi utakuta wawekezaji wanakimbilia kuwekeza kenya wakati ukiangalia Tanzania ndio ilikuwa katika nafasi nzuri ya kufanyiwa uwekezaji. Hivyo tunakosa nafasi za ajira kwa watu wetu kwa kutozingatia mambo ya msingi.
Lakini pia suala la ujasusi linahusisha sekta nyingi hivyo ni muhimu pia kutupia jicho katika sekta nyingine na maeneo mengine kama madini, dini, majeshi yetu yote kwani kuna mianya mingi ya kuziba.
Ahsanteni.
 
Back
Top Bottom