SoC04 Sekta ya elimu ikiwa hivi naiona Tanzania mpya baada ya miaka kumi na tano(15)

Tanzania Tuitakayo competition threads

ahssan shebughe

New Member
Feb 11, 2014
1
2
Utangulizi,
Sekta ya elimu Tanzania ndio inaandaa wadau wote wa maendeleo, Kila mmoja katika nafasi yake akijengwa kujua kitaaluma kuino nafasi yake katika maendeleo ya taifa kuna uhakika wa mabadiliko chanya katika katika sekta zote za kiuchumi Tanzania.

Mapungufu ya sekta:
Kwa bahati mbaya mara zote mabadiliko ya katika sekta ya elimu yanalenga mtaala na maslahi ya wadau wa sekta. Kiukweli hizo ni baadhi tu ya changamoto, lakini Kwa upande wangu nataka kuzungumzia mabadiliko katika mfumo wa kisekta hasa katika usimamizi na matokeo. Sekta ya elimu imepungukiwa usimamizi wa kimkakati kuanzia utungaji wa sera , maboresho ya mitaala, ufundishaji na ujifunzaji, na hatimae imekuwa sekta rahisi inayokwenda kiholela.

Mabadiliko:
1. Mabadiliko katika mfumo wa kisekta wa elimu.
Tanzania kwa sasa sekta binafsi inafanya vizuri zaidi katika elimu kuliko sekta ya imma. Hii ni dhahiri sekta ya umma inahitaji maboresho. Tukaondoe aina ya uendeshaji wa shule za umma ili uwe rahisi kuusimamia, elimu itolewe or-tamisemi kisha ijitegemee, walimu wakuu wawe mameneja wa shule, wawe wao wanaopimwa katika matokeo ya kielimu sio hao wanaitwa maafisa. Hii italeta uwajibikaji wa kweli kwa watumishi wa sekta hii na kupunguza ufanyaji kazi wa mazoea katika shule zetu.

2. Mabadiliko katika sera na mtaala.
Inawezekana tunakimbizana na mabadiliko ya kidunia katika uundaji wa sera, lakini ukweli ni kwamba tunakosea kwa namna fulani. Tumeacha kuwa mahiri katika nafasi tunazozimudu na kushiriki katika sera za mataifa makubwa bila sisi kujua, alisema mwalimu "wao wakienda mwezini, sisi twendeni shambani". Hii maana yake nini, tunazijua sekta halisi za kiuchumi tunazoweza kufanya vizuri kwa nafasi tuliyo nayo kama kilimo na ufugaji lakini hatuzipi kipaumbele katika elimu yetu. Hii imezaa wimbi kubwa la wasomi wasio na ajira maana elimu waliyonayo mtaani haina soko lakutosha.

Napendekeza shule zikawe mashamba au viwanda aidha vya bidhaa au huduma. MASOMO kama ujasiriamali, kilimo chakula na lishe,
 
Mabadiliko katika mfumo wa kisekta wa elimu.
Tanzania kwa sasa sekta binafsi inafanya vizuri zaidi katika elimu kuliko sekta ya imma. Hii ni dhahiri sekta ya umma inahitaji maboresho. Tukaondoe aina ya uendeshaji wa shule za umma ili uwe rahisi kuusimamia, elimu itolewe or-tamisemi kisha ijitegemee, walimu wakuu wawe mameneja wa shule, wawe wao wanaopimwa katika matokeo ya kielimu sio hao wanaitwa maafisa. Hii italeta uwajibikaji wa kweli kwa watumishi wa sekta hii na kupunguza ufanyaji kazi wa mazoea katika shule zetu.
Nimeipenda hii, meneja wa shule. Shule zote ziwe ni taasisi. Sema hapo itabidi tujibu suala la gharama za uendeshaji na upatikanaji wa huduma. Na ninadhani kubadilisha jina kutampatia heshima mkuu wa shule atakapoitwa meneja. Meneja ina uzito wake bwana. Ni motisha fulani ambayo haishikiki 'intangible'. Nzuri.

Inawezekana tunakimbizana na mabadiliko ya kidunia katika uundaji wa sera, lakini ukweli ni kwamba tunakosea kwa namna fulani. Tumeacha kuwa mahiri katika nafasi tunazozimudu na kushiriki katika sera za mataifa makubwa bila sisi kujua, alisema mwalimu "wao wakienda mwezini, sisi twendeni shambani". Hii maana yake nini, tunazijua sekta halisi za kiuchumi tunazoweza kufanya vizuri kwa nafasi tuliyo nayo kama kilimo na ufugaji lakini hatuzipi kipaumbele katika elimu yetu. Hii imezaa wimbi kubwa la wasomi wasio na ajira maana elimu waliyonayo mtaani haina soko lakutosha.

Napendekeza shule zikawe mashamba au viwanda aidha vya bidhaa au huduma. MASOMO kama ujasiriamali, kilimo chakula na lishe,
Hii ndiyo kusema ni lazima kama Taifa tuwe na tafsiri ya maendeleo ya kwetu wenyewe.

Na hilo liakisiwe na mitaala ya elimu zetu. Wow!
 
Back
Top Bottom