Seif al- Islam al-Gaddafi atangaza kuwania Urais wa Libya

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,569
9,432
1636970342899.png

Mtoto wa kiume wa kiongozi wa zamani wa Libya Muammar Gaddafi ametangaza rasmi nia yake ya kuwania urais katika uchaguzi uliopangwa kufanyika mwezi Desemba wenye lengo la kumaliza miaka kadhaa ya machafuko tangu baba yake alipoondolewa madarakani.

Seif al- Islam al-Gaddafi mwenye umri wa miaka 49, amejitokeza na kuonekana katika mkanda wa vidio uliotolewa na ofisi inayosimamia uchaguzi, akitia saini nyaraka katika kituo cha uchaguzi kusini mwa mji wa Sebha.

Baadhi ya wagombea wengine ni pamoja na kamanda wa kijeshi upande wa mashariki Khalifa Haftar, waziri Mkuu Abdulhamid al-Dbeibah na spika wa bunge Aguila Saleh.

Jina lake ni miongoni mwa majina yanayojulikana sana Libya, na amekuwa na jukumu kubwa katika sera za nchi hiyo kabla ya vuguvugu la mwaka 2011 lililoungwa mkono na Jumuiya ya kujihami NATO na kuharibu utawala wa familia yake.Seif amekuwa nje ya macho ya umma kwa karibu muongo mmoja.
 
Je, wameshaandaa katiba ya kidemokrasia ambapo hata huyo Al Islam akija hatalazimisha kazi irudiwe tena?

Kinachotusumbua hata sisi hapa kinachosababisha CCM watawale bila ridhaa ya wananchi ni katiba mbovu.
 
Infact Seif Al Islaam kabla ya mapinduzi alikuwa anasimamia project ya Mageuzi nchini mwao. Na alifanya mistake moja iliyougharimu utawala wa baba yake.

Yeye ndiye aliyeshawishi kuachiwa kwa wahalifu wakubwa kwenye magereza ya Libya, hao wahalifu siku chache baadaye wakajiunga na waasi kumng'oa Ghadaffi
 
Je, wameshaandaa katiba ya kidemokrasia ambapo hata huyo Al Islam akija hatalazimisha kazi irudiwe tena?

Kinachotusumbua hata sisi hapa kinachosababisha CCM watawale bila ridhaa ya wananchi ni katiba mbovu.
Wananchi gani wa kuachiwa wafanye mwamuzi ya Nani ashike hatamu hapa!?..wanaompigia mtu Kura kisa anafanya kampeni kwa helikopta!!!?..demokrasia inahitaji watu wenye shule,wachambue alichonena mgombea
 
Anaweza kuwa kiongozi mzuri shida ni kwamba hatoifikisha Libya kokote sababu wababe wa dunia hawamuamini na unajua fitna zao zilivyo kama hawakukubali.
wababe gani wa Dunia hawamkuli? Ana backup ya jasusi Tony Blair, ana masters ya uchumi kutoka London university. Bila shaka atatoboa, kama sio uchaguzi huu, basi ujao.
 
wababe gani wa Dunia hawamkuli? Ana backup ya jasusi Tony Blair, ana masters ya uchumi kutoka London university. Bila shaka atatoboa, kama sio uchaguzi huu, basi ujao.
Unajua kwamba kuna khalifa Haftar ambae anaungwa mkono na Marekani na Ulaya waziwazi, kama isingekuwa Uturuki sasa hivi angekuwa Rais.
 
Namtakia kila la heri. Hivi yupo wapi Askari Kanzu ? Nakumbuka mjadala kali juu ya Libya. Na niliwaambia EU watapatikana...tumeanza kuyaona huko Belarus na Poland mpakani!
 
Back
Top Bottom