Sehemu ya 1: Namna ya kuweka matangazo ya kulipia kwenye mitandao ya kijamii (Facebook Ads na Instagram Ads) hatua kwa hatua

Jay_255

JF-Expert Member
Sep 26, 2014
725
1,288
Imekuwa ni changamoto kubwa sana kwa wafanyabiashara na wajasiriamali wengi kufanya matangazo yao kwa ajili ya kuwafikia wateja wengi zaidi kupitia mitandao ya kijamii (Hasa hasa facebook na instagram ambayo ndio imekuwa inawatembeleaji wengi zaidi).
Nitaonesha hapa hatua kwa hatua namna ya kutengeneza account ya matangazo na kuanza kuweka ads zako.

NB: KUFUATA HATUA HIZI NI BORA ZAIDI IKIWA UTATUMIA COMPUTER/LAPTOP NDIO UTAFANYA KWA UFASAHA ZAIDI
Vitu unavyotakiwa kuwa navyo unapohitaji kuweka matangazo ya kulipia ni

1.Facebook account (account ikiwa ni ya muda mrefu zaidi inakuwa salama zaidi kuepuka kupigwa ban, si salama kuanza kurun ads kwenye account ambayo ni mpya umetoka kuitengeneza hiv karibuni)

2.Facebook business page (Hii unaweza kuitengeneza muda huo huo haina tatizo tofauti na facebook account)
3.Instagram Account (kama utahitaji matangazo yako yatokee na instagram pia)

Ukishakuwa na vitu hivyo hapo juu unakuwa upo tayari kuanza kutengeneza matangaazo ya kulipia

HATUA YA KWANZA
ingia hapa (business.facebook.com)hapa ndipo utakapokuwa una control shughuli zako zote za matangazo. Utakutana na ukurasa huu kisha bonyeza hapo create an account

facebookads1.png


Itakuletea ukurasa wa kukusajili na wewe kuweka taarifa zako kama jina la account nambalo ungependa utumie na jina lako pamoja na email.

facebookads2.png


Ukibonyeza submit watakutumia email ya kuconfirm

facebookads3.png


Ingia kwenye email yako uliyowapa facebook utakutana na email anayokuhitaji kuconfirm matumizi ya business manager
facebookads4.png


Ukisha confirm watakupeleka kwenye business mnager ambapo hapo sasa utaweza kuweka details zako zote.

facebookads5.png


Utaona hapo juu facebook business manager inaweza kucontrol karibu kila kitu kinachohusu mawasiliano ya kimarketing kuanzia facebook yenyewe instagram na whattsapp
.
Kwa wale ambao hawana facebook business page ninaelekeza hapa namna ya kutengeneza facebook business page ambayo ndio utatumia kuweka matangazo yako.

Ingia katika facebook account yako kisha utabonyeza hicho kialama cha jumlisha halafu chagua page
facebookads6.png


Weka taarifa za biashara yako kama vile jina na category ya biashara yako
(nimetengeneza page ya mfano kwa ajili ya kujifunzia - wauzaji wa magari)

facebookads7.png


Ukishaweka taarifa zako bonyeza create page.Baada yapo kazi yako itakuwa ni kuweka taarifa zako tu kama vile website,phone number,address , working hours pamoja na whatsapp unayotaka iungane na ukurasa huu wa facebook.Ni suala la kubonyeza next mpaka utakapomaliza kuweka taarifa zako (sio lazoma uweke zote weka taarifa muhimu tu)

Baada ya hapo ukurasa wako utakuwa tayari kuanza kuutumia.Ili ukurasa wa facebook ukunufaishe ni lazma uwe na wafuasi kama la sivyo tutautumia katika facebook ads kwa ajili ya kuanza kupata watu wa kulike na kuanza kufuatilia post utakazo weka
facebookads10.png


Hapo tumeshamalizana na facebook page sasa ni wakati wa kulink ile business manager account tuliyotengeneza pamoja na hii facebook page.

Rudi katika facebook business manager ambayo utaipata kwa kuingia business.facebook.com/setting
Katika business setting utaenda moja kwa moja kwenye sehemu ya page kisha uta add page yako unayotaka kuendeshea matangazo yako. Angalia picha zifuatazo

facebookads12.png


facebookads13.png
facebookads14.png
facebookads15.png


Mpaka hapa tayari utakuwa umeshaunganisha page yako na facebook business manager na ipo tayari kwa matangazo.

SEHEMU YA PILI YA SOMO NAIANDAA (NAMNA YA KUWEKA NJIA ZA MALIPO NA TUTAJUA AINA TOFAUTI TOFAUTI YA MATANGAZO)

Kama kuna sehemu haijafahamika vizuri unaweza kuuliza hapa kwenye comment.....
 

Attachments

  • facebookads13.png
    facebookads13.png
    20.7 KB · Views: 58
  • facebookads14.png
    facebookads14.png
    18.4 KB · Views: 61
Back
Top Bottom