MICROF COMPANY LIMITED
Kampuni ya Microf inajishughulisha na utoaji huduma za mafunzo katika soko la Microfinance na pia Kampuni ya Microf inamiliki gazeti la Ujasiriamali liitwalo TAJIRIKA. Hivyo, tuna nafasi za kazi zifuatazo:
TRAINING COORDINATOR (NAFASI 1)
Sifa: Awe anajua vizuri soko la Microfinance na SACCOS maana mafunzo yetu yamejikita katika soko la Microfinance na Ushirika (SACCOS), Awe na elimu kuanzia shahada ya kwanza, awe na uzoefu usiopungua miaka 3.
MHARIRI WA GAZETI (NAFASI 1)
Mhariri (Editor) wa gazeti letu TAJIRIKA linaloandika habari na makala juu ya ujasiriamali, biashara na fedha. Awe na uwezo wa kuhariri, awe na uzoefu usiopungua miaka 2 katika sekta ndogo ya uandishi wa habari za magazeti, elimu kuanzia shahada ya kwanza inayohusiana na Mass Communication.
GRAPHIC DESIGNER & LAYOUT (NAFASI 1)
Graphic designing & layout ya gazeti TAJIRIKA; Awe na uelewa mzuri wa sekta ya habari hususani uandishi wa habari za magazeti, uzoefu usiopungua mwaka 1, elimu kuanzia diploma na kuendelea.
WAANDISHI WA HABARI ZA MAGAZETI ( NAFASI 5)
Waandishi wa habari na makala juu ya mada mbalimbali za ujasiriamali, biashara na fedha, elimu kuanzia shahada ya kwanza inayohusiana na mass communication
Tuma maombi yako yenye barua, nakala ya vyeti na wasifu (CV) kwa CEO, Microf Company Limited, P. O. Box 75779 Dar Es Salaam, e-mail:
microfmd@gmail.com au unaweza kuleta maombi yako ofisini kwetu Kinondoni B, kwa mawasiliano zaidi usisite kutupigia 0754 273 582 au 0718 508 927 Mwisho wa kupokea maombi ni Jumamosi tarehe 1 Oktoba, 2016