SC Villa ya Uganda imefungwa mabao 7-0 na FUS Rabat ya Morocco katika mchezo wa kwanza hatua ya 16 Bora Kombe la Shirikisho la Soka Afrika ugenini leo.
Mabao ya Rabat yamefungwa na Mourad Batna, As Mandaw, Abdessalam Benjelloun, Mehdi Ei Bassel, Maroune Saadane, Youssef El Gnaoui na Mohamed Fouzair.
Kwa matokeo hayo, SC Villa inatakiwa kushinda 8-0 katika mchezo wa marudiano Uwanja wa Taifa wa Nelson Mandela, Namboole, Kampala wiki ijayo.