Sauti ya hoja; Hivi CCM wanamnadi au ndio wanamuondolea kabisa Mbowe credibility na uhalali alionao mbele ya wanachama?

Maximilian Bukuru

New Member
Nov 15, 2018
1
0
1. Hivi kwa akili ya kawaida tu dada Mange, hapa CCM wanamnadi au ndio wanamuondolea kabisa FAM credibility na uhalali alionao mbele ya wanachama na wajumbe wa kamati kuu ya CHADEMA?

2. Hivi unadhani kuwa CCM hawatambui kwamba yule anayeungwa mkono na wao moja kwa moja, hakika ndio ataonekana kuwa adui na msaliti mbele ya macho ya wanaCHADEMA?

3. Kama wanalitambua hilo, kwa nini sasa CCM ioneshe kumuunga mkono FAM wanaemtaka, ilhali wakitambua wazi kuwa kwa kufanya hivyo wataipoteza huduma yake?

Ukiniuliza mimi juu ya nafasi ya CCM kwenye uchaguzi huu, jibu langu litakuwa simple na rahisi sana kuwasilishwa, as my opinion ni kuwa CCM necessarily hawamuhitaji aidha Lissu au Mbowe kuwa mwenyekiti, isipokuwa kitu pekee ambacho wao wanakitaka hivi sasa dhidi ya CHADEMA, ni kuona emergency ya confusion and chaos kati ya wanachama na wenye maono yenye nguvu ndani ya chama. Whether you believe it or not, kuna vita kubwa sana inayoendelea kati ya TAL na FAM, cha kushangaza watu wengi tumejikita zaidi kwenye migogoro hii inayoendelea badala ya kujiuliza vyema juu ya sababu ya msingi iliyowafanya watu hawa kuwa maadui kiasi hiki. Just for the sake of addressing that issue, ninaomba kuwasilisha maswali yafuatayo:

1. Ni kwa nini FAM baada ya kutoka gerezani alianza mission ya kuwashughulikia TAL, Heche, Msigwa, Lema na Wenje? Je ni kweli itakuwa sawa kuamini kuwa wivu wake dhidi yao na tamaa yake ya kuendelea kuwa A and Ω ndio iliyomfanya afikie maamuzi hayo?

2. Je, ni kwa nini Mbowe aliyeingia gerezani alikuwa tofauti na yule aliyetoka gerezani typically as how TAL has often been describing? Je UTOFAUTI huo ulikuwa ni upi? (Maana kama ni issue ya MBOWE kuwa soft, tabia hiyo haijaanza mwaka 2022, badala yake it has always been the main part of his personality for so long. Kama ni issue ya Mbowe kujihusisha na rushwa na uhuni, tabia hiyo kwake haikuanza mwaka 2022, as FAM amejikuta katika shutuma hizo kwa muda mrefu kuanzia mwaka 2008.).

3. Je, ni nini ambacho FAM alielezwa na SSH baada ya kukutana ikulu? Je ilikuwa ni kuhusu maridhiano pekee, au kulikuwa pia na ajenda mficho iliyowahusisha viongozi notable ndani ya CHADEMA?

4. Doesn't it make sense kwamba FAM alianza kutengeneza mpango wa kuiondoa camp ya Lissu CHADEMA, baada ya kugundua kuwa walikuwa sehemu ya mpango wa kumpindua wakati akiwa gerezani?

5. Je, ni kweli kuwa TAL ni msafi sana kama ambavyo wengi wakijaribu kumlabel?

6. Je, ni kweli kuwa shutuma za Wenje dhidi ya Lema, Heche, Lissu na Msigwa hazina ukweli wowote ndani yake?


NOTE: Ni rahisi sana kwa Lissu kumvika FAM maovu yake BINAFSI na ya CHAMA KWA UJUMLA, simply because FAM was a supreme leader who had a certain vetto authority ndani ya chama. Na ni ngumu kwa FAM kuyaweka bayana machafu makubwa ambayo TAL aliyafanya dhidi ya taifa hili kwa mgongo wa chama, simply because TAL wasn't a supreme leader who had vetto authority ndani ya chama.

With that being said, ukimshutumu Lissu kuwa alihusika na harakati za kumfukuza Zitto, Lissu will simply respond kuwa wakati huo alikuwa anafanya kazi chini ya mwenyekiti ambaye alikuwa na uwezo wa kumuwajibisha endapo kama ingeonekana kuwa alikiuka taratibu za chama kwa namna yoyote, such that kitendo tu cha mwenyekiti kulikalia kimya jambo hilo kipindi hicho, kuna mfanya mwenyekiti na yeye kuwa mshirika mkuu wa hujuma hiyo na possibly kumuweka TAL salama na safi mbele ya umma.

NB: Yawezekana shutuma za Wenje dhidi ya Lissu na kambi yake zisipate nguvu kwa sasa kama ambavyo shutuma za Msigwa dhidi ya FAM zilivyokuwa kwa miezi kadhaa iliyopita. But trust me, kuna wakati utafika na hoja zake zinazodharaulika zitaonekana kuwa na mashiko makubwa kuliko tunavyofikiria.

Maximilian Ludovick anaomba kuwasilisha 🙏🏿 ✊🏿.
 
Back
Top Bottom