Wadau tuungane tuifuatilie bajeti mpya 2017/18 ili tuelewe kuwa je,itakidhi kiu na matarajio yetu kuhusu vitu vifuatavyo vinavyogusa maisha yetu ya kila siku;
Je,itatoa nafasi za ajira kwa vijana hususani walimu,madaktari ,wakunga, manesi na kada nyingine .Kada hizi nimezitaja kwakuwa kuna uhaba mkubwa wa watumishi ,hususani hospitalini na shuleni.
Je itatoa kipaumbele ktk kilimo? Hususani pembejeo na ruzuku ktk kilimo.Kilimo ndio sekta inayotoa ajira kwa watu wengi ,zaidi ya asilimia sabini ya watanzania hutegemea kilimo.Hivyo kama bajeti itazingatia sekta hii maana yake itakuwa imegusa maisha ya kila siku ya mtanzania wa kawaida.
Je,itatoa nafuu kwa mtumishi wa umma? Yaani itazingatia ongezeko la mishahara,upandaji madaraja na ulipaji wa malimbikizo ya madeni ya watumishi wa umma
Je,itatoa ahueni ktk elimu? Yaani kuboresha sera ya elimu bure ambayo kwa sasa pesa inayopelekwa haikidhi mahitaji ya kumhudumia mwanafunzi ktk huduma kama chakula,kuajiri walimu wa sayansi na ulinzi shuleni.Pia haikidhi kutoa motisha kwa walimu.Kadhalika bajeti lazima izingatie mikopo kwa wanafunzi wote wa elimu ya juu bila ubaguzi kwakuwa nk mkopo na watatakiwa kuulipa .Mwisho bajeti ya elimu ikumbuke kurudisha heshima ya mwalimu kwa kumpa teaching and housing allowance
Je,itatoa mwanga kwa wajasiliamali wadogo wadogo kwa kuweka mazingira rafiki ya kodi na kuwezesha waweze kukopesheka kwenye taasisi za fedha?
Haya ndio mambo ya kuyajadili ktk bajeti ijayo.Tuhamishie mijadala yote kwenye suala la bajeti kwani lina maslahi mapana ya maisha ya kila siku kuliko mambo ya udaku