Sasa nimeamini ajira za walimu mwaka huu ni kitendawili

Rutorial k

JF-Expert Member
Jun 8, 2014
951
843
Katika bajeti ya wizara ya TAMISEMI waziri aliomba sh.17 bilion kwa ajili ya ajira mpya za walimu ambazo zingetolewa mwezi May. Pia Naibu waziri elimu akijibu swali la mbunge wa Mlimba, Suzan Kiwanga ni lini serikali itaajiri walimu ili kukabiliana na uhaba uliochangiwa na ongezeko la wanafunzi mashuleni alisema ajira zitatoka kati ya mwanzoni mwa mwezi May na mwishoni. Leo ni tarehe 31 hakuna lolote.

Hiyo haitoshi leo bungeni naibu waziri TAMISEMI ameulizwa swali ni lini walimu watapelekwa mashuleni kajibu ni hadi pale mchakato utakapokamilika.

Hivi hawa wanasiasa huwa lazima waseme uongo? Kwanini wasiwe wawazi ili kama mtu umepata mkataba wako shule za private ujue usaini muda gani?
 
Malalamiko ni sehemu ya maisha ya kila Mtanzania, Madaktari, Walimu, Wafanyikazi, Wafanyibiashara, Wakulima, Wafugaji, Wanafunzi, Wahitimu......
 
Shidaa
 
Hawatutendei haki kwa kweli!.....

Ilaaa haiba ndo tunayoitetea tofauti na hapo na sie tungeanzisha chama cha walimu tarajali aisee maana hali ni mbaya!...
(Just jocking)
 
UDSM....Wameandamana leo wamepewa Boom....Zamu yetu sasa WAKE UP......
 
 
Inasikitisha sana, bora waseme ukweli ili watu wajue wafanye nn ktk mipango yao. ila nadhan hata kada zingne bado tuendelee kusubili.
 
Nina mashaka makubwa sana hata huo mwezi wa 7 ukapitiliza hadi wa 10+ , Wanazingua sana wawe wakwel tu hata wakisema desemba mtu iwe unajua
 
mwaka huu unafika tangu tumalize chuo,wangetupa taarifa kuwa ajira mpaka mwez flan mwaka flani watu tungejua tunafanya nn kabla ya hayo maajira yao,nasikia mishahara ya watumishi wa uma mwez huu ilichelewa sana na kama wanafunzi wamekosa boom na huko jeshi(uhamiaji) hawajapewa fedha zao za kujikimu/chakula,waadhiri UDOM waligoma kwa sababu za kimasilahi.Unadhani sisi tutaajiriwa soon kwa nchi hii inayodharau taaluma ya ualimu? Acha tuisome namba eeeh........malizia
 
Magufuli alikataa viongozi wa serikali kasema tuko kwenye mchakato Je huyu sio jipuuuuu
 
Magufuli alikataa viongozi wa serikali kasema tuko kwenye mchakato Je huyu sio jipuuuuu
kwa serikali hii ya kubana matumiz na kukusanya kodi,nikaju swala letu litakuwa rahisi,lakin hadi saiv naona namba tushaisoma sana tuu
 
kwa tz hii nahic mpk watuone barabarani au tuongee na waandishi wa habari vingnevyo hatutoboi me nlimsikia simbachawene kati ya mwezi wa 3&4 kwenye clouds 360 akadai wameshaandaa wanasubir tu bajeti ipitishwe sasa cjui tuna bajeti tofauti na nliyosikia juzi bungeni...?
 
Hata Kigwax alisema hivyohivyo kwenye ajira za sekta ya afya,
Tulieni na muwe na subra hadi mwaka ujao wa fedha.
 
Walimu ubovu wenu mnasubiri vya kuchinjwa muwekewe mezan, sio bora nyie mna matumaini?je wenzenu tuliosoma kada mbali na kula vumbi la chaki?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…