Sasa ni wakati wa wananchi kukubaliana kutokukubaliana na mheshimiwa

MGANGA MCHAWI

Senior Member
Oct 15, 2015
199
393
Najaribu kuwafikiria wanafunzi walivyokua na iman ya mikopo ila haijawa hivo, nawatazama wagongwa walpokuwa na iman ya kupatikana kwa madawa ila imekua ndivyo sivyo, wahitimu wa vyuo vkuu waliokua na iman na ahadi ya ajira ila saiv wameshika tama, nawangalia wafanyakaz wa umma waliohaidiwa mishahara mikubwa kwa mapatano ya kuchapa kazi ila saiv hata kidogo walichokua wanakpata hakijtoshelez kutokana na gharama za maisha kupanda, najaribu kumsahau mkulima na imani ya kupatiwa pembejeo ila hadi saiv wamebaki na mshangao.

Najaribu kukumbuka ahadi ya viwanda ila hadi sasa tupo kwenye mshangao.
Najaribu kukumbuka kasi ya mawaziri walipoingia madarakan ila nawaona nao saiv hawajui wanaenda ofisin kufanya nn mana wanatoa maagizo na maamuzi asubuhi jion yanapanguliwa kwa vitsho kuwa asiekubaliana nae aachie ngaz.wamepewa spika huku mike anayomwenyewe.
Nan atamfunga paka kengele?

Kinachotokea saiv hakuna aliekitegemea??

Watanzania wote tulkua tunaishi peponi?

Sasa watanzania ni wakati muafaka wa kukubaliana kutokukubaliana na kuamua kuendelea na maisha kulingana na hali iliyokuwepo.Tuache kujpa iman kuwa tusubiri kesho mambo yatakua mazuri bila kufanya chochote.Naona wananchi wengi wanakua na iman labda leo atasema hiki afu mwshowe wanaishiwa kukatshwa tamaa.

Watanzania tuanze kuielewa ile nyimbo yao ya kpnd kile.Walituambia tutavimba na kupasuka sasa kwann leo tunashangaa??

Walisema tuachwe tuandamane (wajinga ss) wao ni mbele kwa mbele.
Sasa ni muda wa kufunga mkanda na kama haitoshi tukaze na kamba..
Tupambane na hali yetu na kuanza kufanya kinachowezekana maisha yasonge.

Wanafunz mliokua na imani ya kupata mikopo turudi kufanya kinachiwezekana twende shule, wafanyakazi mliokua na Imani ya mishahara minoo muishi na mnayopata na kurudsha upendo kw kazi zenu.Wakulima endeleeni kutumia samadi kulimia.

Endeleeli kuangalia mbegu kutoka kwenye mlichovuna.Walimu ndugu zangu mliomba kuhama ni wakati sasa wa kurudsha akili kwenye vituo vyenu vya zaman na kuchapa kazi.wananchi wakawaida jiandae na lolote ltakalotokea baada ya kukosekana kwa mvua.

Sasa ni wakati wa kuishi maisha halisi na kuacha kuishi kwenye dunia ya kusadikika.

TUACHE KUSUBIRI TRAIN UWANJA WA NDEGE.
 

"SERIKALI YANGU HAITATOA CHAKULA,NINAPOSEMA SILETI CHAKULA SILETI KWELI,WALA SIMUNG'UNYI MANENO NA SITALETA KWELI,MLIZOEA MANENO MATAMU SASA MIMI SINA MANENO MATAMU"alisisitiza Rais Magufuli.



MANENO YAKE YANATISHA SANA.

swissme
 
...
Sasa ni wakati wa kuishi maisha halisi na kuacha kuishi kwenye dunia ya kusadikika.
TUACHE KUSUBIRI TRAIN UWANJA WA NDEGE.
Maelezo marefu yasiyo na jambo jipya zaidi ya kulalama na kulaumu.

Nchi ina miaka zaidi ya 50, ni eneo lipi limebadilika kwa tawala zilizopita! Sababu kubwa ni sisi wenyewe kuwa tegemezi katika kila kitu, hata mawazo ambayo ni kama yaliyomo kwenye bandiko lako hili. Ila umeitimisha vizuri.

Mabadiliko hayaji kama mvua ila kwa mipango thabiti na uthubutu wa kuitekeleza, siyi Serikali tu, ila mimi, wewe, yeye, wao na sisi.

Nikinukuu hitimisho lako, tufanye kazi, kila mmoja wetu katika maeneo yetu, kwa umakini na uadilifu, hakika tutavuna tutakachopanda
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…