Sasa imefikia tuchukue hatua ya kujilinda wenyewe

Justine Marack

JF-Expert Member
Jul 31, 2014
606
1,675
Sasa imefikia tuchukue hatua ya kujilinda wenyewe.

Kwasasa tunatakiwa kufanya yafuatayo:

1. Polisi waje wamevalia sare

2. Polisi wautaarifu umma uliopo karibu kuwa wanamkamata mtuhumiwa kwa kosa gani na wanampeleka wapi.

3. Muhimu zaidi Polisi wakubali kurekodiwa Ili kuweka kumbukumbu ya usahihi wa kazi ya ukamataji.

Endapo mkamataji yeyote akitaka hayo yasifanyike basi tumuhesabu kuwa Mtekaji.

Kwa maoni yangu binafsi, kwakua hawa watu wanaichafua serikali na jeshi la Polisi.
 
TRA

MAMLAKA YA MAΡΑΤΟ ΤΑΝΖΑΝΙΑ

TAARIFA KWA UMMA

UFAFANUZI KUHUSU SHAMBULIO LA GARI NA WATUMISHI WA TRA KATIKA ENEO LA TEGETA (Kwa Ndevu)

Dar es Salaam, 06 Desemba, 2024:

Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) inasikitika kuutarifu Umma kwamba gari yake yenye namba za usajili STL 9923, ikiwa na Watumishi watatu katika doria za kawaida za udhibiti na ukamataji wa magendo na magari yaliyoingia nchini kinyume na taratibu za Forodha na kutolipiwa ushuru, imeshambuliwa na watumishi kuumizwa katika eneo la Tegeta kwa Ndevu, tarehe 05 Disemba, 2024, usiku.

Kadhia hii imetokea baada ya watumishi wa TRA kubaini kwamba gari namba T229 DHZ aina ya BMW X6 ilioingizwa nchini kinyemela bila kulipa kodi za serikali stahiki kwa mujibu wa sheria na kuifuatilia kwa lengo la kuikamata ili kuchukua hatua stahiki kwa mujibu wa sheria za kodi.

Wakati Watumishi wa TRA wanatimiza wajibu wao, walihusishwa na kitendo cha utekaji, kilichopelekea wao na gari kushambuliwa.

Mamlaka ya Mapato Tanzania, inawapa pole watumishi wake waliojeruhiwa wakiwa wanatimiza wajibu wao, pamoja na wengine wote waliojeruhiwa katika kadhia hii, na kuwaombea wapone kwa haraka.

Mamlaka ya Mapato Tanzania inauhakikishia umma kuendelea kutimiza wajibu wake kwa mujibu wa sheria.

"Pamoja Tunajenga Taifa Letu"

Imetolewa na;

IDARA YA ELIMU KWA MLIPAKODI NA MAWASILIANO
downloadfile-1.jpg
 
Back
Top Bottom