MwanaDiwani
JF-Expert Member
- Mar 22, 2013
- 5,536
- 2,266
MIMI Mwenyekiti wenu nipo imara na kwa hulka yangu, mimi hizi kejeli na matusi kwangu ni kama vile maji katika mgongo wa bata, halowani. Kwa hiyo, waendelee tu, pengine tumeanza kuwabaini.
Hiyo ni kauli ya Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba, Samuel Sitta, kwa wajumbe wa Bunge hilo wiki hii, wakati akitoa taarifa juu ya utaratibu wa kupokea mawasilisho ya kazi zilizofanywa na Kamati za Bunge, mjini Dodoma.
Kauli hiyo ya Sitta ililenga kufikisha ujumbe kwa watu na makundi mbalimbali wanaolalamikia mwenendo wa sasa wa Bunge Maalum la Katiba, wa kuendelea kupokea maoni mapya kutoka makundi mbalimbali ya kijamii kwa ruhusa yake, huku wengine wakishinikiza Bunge hilo lisitishwe.
Kwa sisi tunaomfahamu Sitta, kauli yake hiyo ya kwamba kejeli na matusi kwake, ni sawa na maji kwenye mgongo wa bata yanayoteleza tu na kumwacha bata bila kulowana mwili wake, alimaanisha hivyo. Kwa historia yake, Sitta si mtu wa kutikiswa wala kutishiwa nyau!
Amekuwa ni mtu wa mapambano tangu enzi za ujana wake hadi sasa. Na pengine, ujasiri wake wa kutomnyenyekea mtu, ndio umemwezesha kuwa hapo alipo leo kisiasa katika umri wake wa takriban miaka 72 sasa.
Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, alianza kumfahamu vizuri Sitta, pale alipowaongoza wanafunzi wenzake wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kupinga utaratibu wa kuwalazimisha kujiunga na mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) mara tu baada ya kuhitimu chuo kikuu, wakisema utaratibu huo ulikuwa ni zaidi ya ukoloni.
Mwalimu kama mkuu wa nchi, mwasisi wa mafunzo hayo ya JKT na pia Mkuu wa Chuo hicho, kwa hasira kubwa, aliamua kuwatimua kina Sitta na kuwaagiza wakaripoti kwa wenyeviti wa vijijini vyao kwa uangalizi zaidi wa tabia zao.
Kwa hakika kabisa, Sitta, ni mtu wa mapambano. Kama angekuwa mwanasiasa legelege na hohehahe, historia ya siasa za nchi hii ingekuwa imekwishamsahau. Kwa muda mrefu amepigwa vita jimboni kwake ili ashindwe ubunge, lakini mara zote ameibuka kidedea katika vita hiyo.
Leo hii, kama kuna jimbo linaloongoza kwa wingi wa pikipiki, baiskeli na simu za mkononi, basi ni jimbo la Urambo Mashariki analoliongoza Sitta. Mahasimu wake wa kisiasa, mara kadhaa wamekuwa wakimwaga pikipiki, baiskeli na simu za mikononi kwa wapigakura ili wasimpigie kura Sitta kila unapofika uchaguzi, lakini hadi leo yumo tu.
Lakini pia, Sitta amepigwa sana vita ya kutaka kushushiwa heshima yake katika mkoa mzima wa Tabora, kiasi cha baadhi ya mahasimu wake wa kisiasa kuwatawaza watu kutoka nje ya mkoa huo kuwa machifu wa Wanyanyembe ili tu kumwondolea hadhi na heshima mwanasiasa huyo mbele ya Wanyanyembe wenzake.
Katika mazingira hayo na mengine mengi tu ambayo yamekuwa yakimzunguka katika hatua yake ya kisiasa, ninachoweza kumshauri Sitta kwa sasa, na hasa katika kipindi hiki ambacho anakabiliwa na jukumu zito la kuhakikisha Watanzania wanapata Katiba mpya, ambayo kwa mara ya kwanza katika historia ya Uhuru wa nchi hii wameshirikishwa kuiandaa wenyewe kupitia maoni yao, ni kujizuia na hamaki pamoja na kuwapuuza baadhi ya wabaya wake kwa sababu wabaya wake hao wa sasa, hawana nguvu yoyote ya kukabiliana na naye, wakilinganishwa na wabaya wake wa nyuma walioshindwa kufua dafu kwake.
Waswahili wana msemo wao wa kwamba mti wenye matunda ndio unaopopolewa mawe. Sitta ni mti wenye matunda, kamwe hawezi kukwepa kupopolewa mawe. Ikifika siku akajikuta amezungukwa na wachekeshaji pekee kama wale wa Ulaya aliowataja bungeni wakati akitoa kauli yake hiyo hapo juu, basi atambue kwamba nguvu yake kisiasa imekwisha, itampasa akapumzike kijijini kwake Urambo.
Lakini kwa kuwa kwa sasa Sitta bado ni yule yule wa jana na leo, itambidi atulie apopolewe kwa mvua ya mawe, kwa sababu wanaompopoa mawe hayo wanajua wanachokifanya. Kumyumbisha ili aachane na agenda iliyoko mbele yake ya kupata Katiba itakayopendekezwa na Bunge Maalum ili ikapigiwe kura za maoni na wananchi.