Dalton elijah
JF-Expert Member
- Jul 19, 2022
- 433
- 933
Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir ametoa wito wa utulivu nchini humo kufuatia kushambuliwa kwa helikopta ya Umoja wa Mataifa siku ya Ijumaa.
Kulingana na jeshi la Umoja wa Mataifa la kulinda amani Sudan Kusini (UNMISS) watu kadhaa wanahofiwa kufa na wengine kujeruhiwa baada ya helikopta ya Umoja wa Mataifa iliyokuwa ikijaribu kusaidia uokozi wa wanajeshi wa Sudan Kusini kushambuliwa.
Jenerali David Majur Dak kutoka Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Sudan Kusini (SSPDF) na maofisa wengine, wameripotiwa kupoteza maisha katika tukio hilo, kulingana na taarifa iliyotolewa na UNMISS.
"Naomba niendelee kusisitiza kuwa nchi yetu haitorudi tena vitani. Mtu yeyote asijichukulie sheria mkononi," alisema Kiir.
"Serikali ninayoiongoza itakabiliana na janga hili, tukiendelea kujizatiti ili tupate amani," aliongeza.
Sudan Kusini, ambalo ni taifa changa zaidi duniani, lilimaliza miaka mitano ya vita vya wenyewe kwa wenyewe mwaka 2018, kufuatia mpango wa kugawana madaraka kati Kiir na Makamu wa kwanza wa Rais Riek Machar.
Hata hivyo, wafuasi wa Kiir wameshutumu vikosi vinavyoongozwa Machar kwa kukuza machafuko katika eneo la Nasir.
"Shambulizi dhidi ya maofisa wa UNMISS halivumiliki na ni uhalifu wa kivita chini ya sheria za kimataifa," amesema mkuu wa UNMISS Nicholas Haysom."Tuna huzuni kufuatia vifo vya watu tuliokuwa tukiwaokoa," aliongeza.