Salehe Songora wa Sonora Marine Transport awezeshwe kukuza uundaji meli na mashua

Naisujaki Lekangai

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
1,340
1,377
Habari nzuri zimeenea kwamba meli ya kisasa ya kubeba mizigo ziwa nyasa itazinduliwa hivi karibuni.Cha kufarahisha mno ni kwamba meli hiyo ya kisasa imeundwa hapa hapa nchini na mhandisi mzalendo aitwate Eng. Salehe Songoro.
Kwa serikali hii inayotaka kuhimiza ukuaji wa viwanda huyu mhandisi ni zawadi kubwa toka kwa Mungu. Ni mbegu nzuri ya kuanzisha viwanda vya kanda vya kuunda mashua na meli za kisasa.
Yapaswa sasa serikali iunde mkakati maalum wa kumtumia huyu mhandisi katika kutekeleza hiyo azma ya viwanda vya kanda vya mashua na meli kwa soko la afrika mashariki.
Yale makosa yaliyofanywa na wizara ya afya ya kumsononesha mtaalamu wa magonjwa ya moyo Dr Ferdinand Masao mpaka akafariki yasitokee hata chembe kwa mhandisi Songora.
Tukiletewa mbegu ya maendeleo toka kwa Mungu tuipande na sio kuichezea mpaka ipotee.
Opportunities never come twice. Songora akipata maudhi anaweza kwenda kenya au uganda na kufungua viwanda vya meli.Watampokeaje!
 
Sawa lkn sio hawa wa sasa wasiokuwa na vipaumbele wao ni kuburi na kutisha watu na kutoheshimu katiba
 
Kampuni ya Songoro naikubali sana, hawa ndio wazalendo wa kweli
Wameshatengeneza boti na vivuko vingi sana
 
Kampuni ya Songoro naikubali sana, hawa ndio wazalendo wa kweli
Wameshatengeneza boti na vivuko vingi sana
wapewe tenda waende ziwa victoria napo, ukerewe meli za serikali zishakufa zote na sijasikia kuwa watapelekewa meli
 
Songoro wako vizuri sana kwa uundaji Wa meli wawezeshwe zaidi .
 
Songoro hana elimu zaidi ya form 4 au uhandisi alinunua kiwanda cha serikali ambacho kinatengeneza boti n feri kiko mwz,wako mafundi ambao ndio hutengeneza hizo boti n feri,kwa kanda ya ziwa boti nyingi yeye ndio katengeneza
 
Kuna story mtaani eti huyo Songoro aliwaambia watu wa uokozi wasitoboe meli ya MV Bukoba ili kuokoa watu waliokuwa wamenaswa, lengo ilikuwa alete vivuko vyake waifunge meli kuelekea maji ya kina kifupi, hawakumsikikiza na wakaitoboa ikazama fyuuuuu! Tundu walilotoboa alilpita MTU moja tu.
Hii inainyesha tangu enzi huyu Songoro watu hawatambui mchango wake
 
wapewe tenda waende ziwa victoria napo, ukerewe meli za serikali zishakufa zote na sijasikia kuwa watapelekewa meli
Huyo Songoro kwao lake Victoria..vivuko vyote katengeneza yeye ni mkazi wa jiji la Mwanza
Lkn kwa serikali yetu mda wowote inaweza kumtumbua kwa kisingizio Kua bei yake ni kubwa
 
Songoro hana elimu zaidi ya form 4 au uhandisi alinunua kiwanda cha serikali ambacho kinatengeneza boti n feri kiko mwz,wako mafundi ambao ndio hutengeneza hizo boti n feri,kwa kanda ya ziwa boti nyingi yeye ndio katengeneza
Awe std 7, form iv, form vi siyo ishu. Ishu ni kwamba yeye ni mjasiriamali mzuri aliyeona fursa na akaitumia vizuri. Ni juu yake sasa kujitangaza vizuri kwenye hii kanda ya afrika mashariki na kati ili ajenge vyombo vya majini kwa nchi hizo, na serikali pia isikimbilie uholanzi inapohitaji meli, feri mashua nk. Pointi kwa serikali yetu ni: kama ng'ombe wa maziwa unaye nyumbani kwa nini uende kwa jirani mwenye ng'ombe kama wewe kutafuta maziwa?
 
"Hapo hapo nikamlipa sh.milioni 150 kati ya sh.milioni 250 tulizokubaliana kama advance ya kutengeneza kivuko katika ziwa Victoria Mwanza cha ajabu hadi ninapoandika kitabu hiki SALEH SONGORO hajatengeneza kivuko hicho imeshapita takribani miaka 10 sasa na pesa yangu hataki kunilipa.Mimi nimemwachia mungu nasonga mbele".Nimenukuu kutoka katika kitabu cha Eric James Shigongo kiitwacho JINSI YA KUTOKA KATIKA. UMASIKINI HADI MAFANIKIO [ukurasa wa 155].Hapo alikuwa anaelezea jinsi alivyotapeliwa na huyo ENG.SALEH SONGORO
 
nje kidogo ya mada,Eng Songoro aliwahi kumdhurumu ndg Shigongo mil 200 miaka ya nyuma kidogo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…