Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 1,093
- 2,625
Simba roho juu, huwenda waka-katwa alama ishu ya mchezaji Yusuph Kagoma kusaini Yanga kisha kuwatosa na kuibukia mitaa ya Msimbazi.
Mchambuzi na expert wa mambo ya usajili, Hans Rafael amedai kuwa Kamati ya sheria na hadhi za wachezaji, Leo asubuhi imesikiliza kesi ya kiungo wa Simba Yusuph Kagoma, na kuamuru mchezaji huyo asimame haraka kuitumikia klabu hiyo.
Yanga wao wamethibitisha kuwa hawajamsamehe Kagoma, na wanataka haki ifuatwe.
Pia Yanga wanashinikiza Simba wapokwe pointi sita za ligi ambazo walizipata kwa kumtumia mchezaji batili (Kagoma) kwenye mechi dhidi ya Tabora na Fountain Gate.
Sakata hili pia lilimuibua mdau wa michezo na Waziri wa Fedha, Dkt. Mwigulu Nchemba na kuzungumza uhalisia wa namna anvyofahamu sakata hili la Kagoma kusaini pande zote mbili.
Swali la kujiuliza aliwezaje kucheza mechi kama usajili wake ulikuwa na utata kuitumikia Simba SC?
Soma ==>Mwigulu awaomba viongozi wa Yanga wapotezee suala la Kagoma ili aweze kucheza Simba