Sakata la Gwajima: Maaskofu Pentekoste mlimtuma Mch. Ikongo?

kitumbotala

JF-Expert Member
Aug 6, 2015
516
623
Wakuu habari za jioni,
Kwa wale wenzangu Asalaam Alekyum, hongereni kwa kupata futari.

Nilikuwa najiuliza maswali mengi sana katika kipindi hiki cha swaum za wenzetu, mimi ni kijana mpenda amani wa nchi yetu japokuwa kwenda kanisani sio sana.

Lakini swali ambalo nimejiuliza yule anaitwa askofu Ikongo ambaye aliwaita waandishi wa habari akaanza kuyasema yale ya Askofu Gwajima yeye ndio mkuu wa Maaskofu wa Pentekoste au alikwazika tu kama mwananchi?

Je, kama alkwazika kuna neno linalomhusu kati ya yale aliyoyaongea Gwajima?

Pia ninachojiuliza au hawa Maaskofu walimtuma jamaa aongee na waandishi wa habari, na kuishauri Serikali kulifuta hilo kanisa?

Kama walimtuma, je waliwalipa waandishi sh. ngapi ilikutoa taarifa yao? Au taarifa huwa hazilipiwi?

Nafurahini sisi wakatoliki hatuna maaskofu wengi hivyo usaliti kwetu hakuna japo kwenye vigango kama kawa tunapepetana.

Alafu nilipata picha ya Ikongo akiwa na Mh. fulani (jina kapuni kwa heshima) wa chama cha (jina kapuni kwa heshima), na yeye alikaribishwa na kutambulishwa kama kada. Sasa nikiangalia matukio haya nasema ,<Maria Mtakatifu mama wa Mungu, utuombee sisi wakosefu sasa na saa ya kufa kwetu hata milele amin

Haya maswali jamani ndio mara ya kwanza nasikia Maaskofu wakishauri kanisa kufutwa.

Hakika Katoliki ni dini imara.

Naomba kujibiwa wahusika wa tukio.
 
Katoliki ni dini kumbe okay uko sahihi! Sasa Bishop Ikongo ni makatoliki kwani? Jitahidi utafute kumjua Yesu kama wewe ni Mkristu/Mkristo maana hautaenda mbinguni kwasababu wewe ni mkatoliki bali kwasababu ni mfuasi wa Kristo kwa maneno na matendo yako! Warumi 10:9
 
Sasa mmesababisha hadi mimi nitafute Ikongo ni nani maana nilikua sijawahi kumsikia kabla.
 
Ndugu zangu wanajamvi nawasalimu sana muungwana mwenzenu,

Bila kupoteza wakati naomba niende moja kwa moja katika hoja yangu. Sikuchache zilizopita mchungaji IKONGO wa kanisa PPFT aliitisha vyombo vya habari na kuzungumzia sakata la Askofu Gwajima, na Kutoa matamko mengi yanayo husu sakata hilo kutoka na kile ambacho Askofu Gwajima alisema kama mawazo yake na si ya kanisa wala ya Maaskofu wa Makanisa ya kipentekoste,

Jambo kubwa ambalo Askofu Ikongo alilifanya ni kuita waandishi wa habari na kusema kauli hiyo ya Gwajima ni ya Uongo, uchochezi na Uchoganishi na hivyo kufika mbali hata kuitaka serikali ifute uhalali na usajiri wa kanisa hilo linaloongozwa na Askofu huyo kanisa la Ufufuo wa uzima, Wadau, katika taarifa yake huyo mchungaji ikongo alishindwa kuthibitisha uongo wana huo aliyouita uchochezi wa askofu gwajima aliyousema mbele ya waandishi wa habari, lakini pia mch. Ikongo alikazia na kusema kuwa yeye huyo gwajima sio msemaji wa maaskofu wa umoja wa kipentekoste Tanzania(CPCT) huku akidai kuwa mchungaji gwajima alishaondolewa katika umoja huo. Jambo linalonishangaza ni kuwa mch. Ikongo alisimama na kuwazungumzia nyie wapentekoste wote au nyie viongozi wetu ndio mliomtuma ayaseme hayo?. Maana tangu alipotamka kwenye vyombo vya habari nanyie mpo kimya na hakuna kiongozi wa CPCT toa tamko lolote la kumsapoti au kumpinga mnapoo kaa kimya tuwaeleje?. Mimi sijawai kuona kibali cha kanisa kinafutwa kwa matakwa ya watu wachache kama akina mch. Ikongo na waliomtuma kulizungumzia swala hili, na wala hyo sio sawa kwani serikali mtatengeneza chuki na wananchi wenu jambo ambalo sio zuri.

Katika vipindi vya kigoda cha mwalimu Ulimwengu aliweka wazi mawazo yake tena yeye alizama zaidi kuliko huyo Gwajima .

Maaskofu mki kaa kimya ktk hili mtaonyesha ni jinsi gani ambavyo mpo tayari kuona makanisa yakifutwa na hivyo kuhatarisha uwepo wa imani yetu ya kipentekoste. Jambo hili pia ndugu zangu waislamu nao waliangalie kwa makini kwani linazidi kukua ikizingatiwa ilianza kwa akina shekhe ponda kuwekwa ndani na kunyimwa dhamana kwa kile kinachosemekanaa alitoa maneno ya uchochezi.

Jambo kubwa linalonishangaza ni kua Tanzania tunaanza kupoteza utofauti kati ya uhuru wa kujieleza na uchochezi kwani mtu anapotoa mawazo yake bila kujificha anaonekana ni mchochezi,



USHAURI KWA GWAJIMA.

Askofu gwajima japokuwa sinauhakika kama utasoma hii nakala au la, na sijui kama upo Jf au la au kama unawatu wapohumu naomba wakufikishie ulipo huko Dubai, ninachokiona mimi kinachoendelea hakuna askofu aliye upande wako maana mpaka now hakuna yoyote ambaye ametoa tamko juu ya ikongo kuishauri serikali kwanza nashangaa kama yeye Ikongo ni Askofu kweli anawezaje kushauri eti kanisa lifutwe? Uliwai kusikia wapi kanisa au msikiti unafutwa? Hapa ikongo ameonekana katika picha mbalimbali akihudhuria mikutano na hafla za chama Fulani akiwa kama kada. Na akiwa pamoja na waheshimiwa wa chama hicho sasa usifikiri wewe gwajima hapo unamarafiki eti maaskofu hamna kitu kama hicho wengi ni makada hao na wanachama wa vyama fulani wewe muombe mungu wako na waumini wako salini sana mnyezi mungu mwingi wa rehma atawasaidia. Gwajima simama kama mtu unaejitegemea kama kakobe au mzee wa upako na usiwe na wazo eti chama cha maaskofu…pyuuuuu

Napongeza ndugu zangu waislamu mnabidii na kusaidiana sana mnajua umoja sana kuliko siye wakristu wengi wetu tumejaa uwoga na unafiki na kujipendekeza kwa kwa viongozi wa kisiasa.

Napend kuwasilisha .
 

Attachments

  • UJUMBE.docx
    18.7 KB · Views: 80
Mawazo mazuri sana haya.

Nilibahatika kuwa grup moja la wassap la wachungaji na maaskofu wa Kipentekoste na huyu Ikongo alikuwemo.

Kabla huyu jamaa hajaita waandishi wa habari kujadili hili kauli ya Gwajima alianza kwanza kuwashirikisha watumishi wenzie mawazo yake, wengi wao walimpinga sana na kumkanya kuwa anachokifanya kinaenda kinyume na wito wake kama askofu.

Watumishi hawa wa Mungu walienda mbali zaidi na kudai kuwa kwa taifa lilipofikia inabidi wawepo kina Gwajima kila kona ya nchi hii maana Mungu hawezi kukosa kinywa duniani kiasi hiki.

Kilichonishangaza pamoja na kuonywa hivi na wachungaji na maaskofu wenzake lakini bado huyu Ikongo aliita waandishi wa habari kueleza kile alichokatazwa na wenzie.

Bado naamini kuwa Ikongo yale yalikuwa ni mawazo yake tu, hakutumwa na maaskofu wenzie na mbaya zaidi anaonekana kama mtafuta kiki kwa mgongo wa Gwajima.
 
Alikuwa alikuwa anataka kiki
 
Alikuwa alikuwa anataka kiki
Ila nimeshangaa huyo Askofu kutaka kiki ni kama aibu Fulani au amenunuliwa yaani maana sio kawaida Askofu etiunashauri wamfutie kibari mwenzio duuuu..hii ipo wapentekisto wa Tz tuu sijaona kwingine
 
Huyo ikongo ni nan kwan...??
 
Unaonaje ungewasiliana naye huyo
 
Ma askofu ni wengi kama walimu wa primary siku hizi sijui ni nani anaye wapa daraja la uaskofu kiholela hivi.
 
Katoliki imekimbiwa na waumini kwa sababu ya mafundisho yao elekezi sasa huo ukatoliki wa siku hizi hata. Mimi nimeamua kuukacha sikuhizi nasoma biblia tu maana siamini kanisa hata moja mpaka sasa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…