MIMI BABA YENU

JF-Expert Member
Mar 1, 2019
304
696
1565669256136.png

Ujenzi wa mradi wa umeme katika Mto Rufiji umetajwa kuwa wa mfano katika nchi za SADC na nchi wanachama wa Afrika Mashariki wa EAC, kutokana na namna Serikali ilivyoamua kuusimamia.

Akizungumza katika kituo cha mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar leo na Wanahabari , Mkurugenzi wa Miundo mbinu katika Sekretarieti ya Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini Mwa Afrika ( SADC), Mapolao Makoena amesema mradi huo mkubwa unaojengwa nchini ni wa kipekee, ambao unasimamiwa moja kwa moja na Serikali na unagharamiwa na fedha za ndani.

“Mradi huu mkubwa wa Rufiji ni jambo la kujivunia, sisi SADC tunajivunia na si kwa SADC tu, lakini pia kwa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), amesema mradi huo ni wa kujivunia sana na kwamba ukikamilika utasaidia kuondoa changamoto ya nishati hiyo katika nchi wanachama wa SADC na nchi Wanachama wa Afrika Mashariki.

Mokoena amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwa uthubutu wake wa kutekeleza mradi huo mkubwa wa umeme, ambao utasaidia kupunguza tatizo la umeme katika nchi za SADC huku akisema SADC inamuunga mkono katika utekelezaji wa mradi huo mkubwa wa umeme.

Amesema mradi huo unaonesha unatoa funzo kwamba uongozi unahusika katika kuhakikisha miradi yenye tija inasimamiwa kwa nguvu zote ili kuzinasua nchi zetu katika matatizo ambayo yanaweza kutatuliwa kwa uwezo wa ndani.

Mokoena amesema kutokana na uhaba wa nishati unaozikabili nchi nyingi wanachama wa SADC, juhudi za ziada zinahitajika kuboresha upatikanaji wa nishati, ambayo ni muhimu katika kutimiza malengo ya uwekzaji katika viwanda na uzalishaji wa bidhaa.

Amesema miongoni mwa mikakati muhimu ya SADC kwa sasa ni kuhakikisha kuwa na uhakika wa nishati rahisi, yenye uhakika, gharama ya chini, kupitia mpango maalumu uliowekewa ukomo wa mwaka 2027.

PIA SOMA

TUHUMA ZA UFISADI NA HUJUMA

HISTORIA
 
1565678577880.png

KURUGENZI ya Miundombinu na Huduma ya Sekretarieti ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) imesema inajivunia mradi wa kuzalisha umeme kwa maporomoko ya maji ya mto Ruji (Mwalimu Julius Nyerere) kutokana na manufaa yake kwa nchi wanachama.

Aidha, imeipongeza Serikali ya Tanzania inayoongozwa na Rais John Magufuli kwa kuwa mfano wa kuigwa katika utekelezaji wa miradi ya kisekta ya miundombinu ambayo pamoja na kuipaisha Tanzania kiuchumi, pia ina manufaa makubwa kwa nchi za SADC na Afrika.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Mkurugenzi wa Miundombinu na Huduma wa Sekretarieti ya SADC, Mapolao Mokoena alimpongeza Rais Magufuli kwa uongozi wake na kuhakikisha mradi huo unatekelezwa. Mokoena alisema hayo wakati akijibu maswali ya waandishi wa habari baada ya yeye pamoja na wakurugenzi wengine kuwasilisha mada kuelezea shughuli na malengo ya kurugenzi mbalimbali ndani ya sekretarieti ya SADC.

Miongoni mwa maswali hayo lilitaka kupata maoni yake juu ya mradi mkubwa wa kuzalisha umeme uliozinduliwa hivi karibuni Ruji, mkoani Pwani, nchini Tanzania na Rais Magufuli. “Tunajivunia huu mradi,” alisema na kuongeza kuwa mradi huo una manufaa si tu kwa nchi za SADC bali pia kwa nchi za Afrika Mashariki na Bara zima. Rais Magufuli alizindua mradi huo mkubwa wa uzalishaji umeme Julai mwaka huu, ukitarajiwa kuwezesha nchi kupata umeme wa kutosha.

Unatarajiwa kuzalisha megawati 2,000 za umeme na Ujenzi wa bwawa hilo unaofanywa na wakandarasi kutoka Misri unatarajiwa kugharimu dola za Marekani bilioni 2.9; takribani Sh trilioni 6.5. Awali, akiwasilisha mada kuhusu maendeleo ya miundombinu na huduma ndani ya SADC kwenye eneo la nishati, alisema Mpango Kazi wa Maendeleo ya Miundombinu (RIDMP) wa mwaka 2012-2027 unalenga kuhakikisha kunakuwa na usalama wa rasilimali ya nishati na uhakika wa upatikanaji wake kama injini ya kuinua uchumi.

Alitaja eneo muhimu linalopewa kipaumbele na kutazamwa kiuchumi zaidi katika nishati kuwa ni upatikanaji na ugunduzi wa gesi na mafuta katika nchi wanachama na namna nchi hizo zinavyotumia nishati hizo kupata uhakika wa umeme kwa matumizi ya nyumbani na viwandani.
 
Kujivunia kitu ambacho ndo kwanza kinaanza kujengwa aisee, na naona hawa nao wapo kisiasa tu
 
Ujenzi wa mradi wa umeme katika Mto Rufiji umetajwa kuwa wa mfano katika nchi za SADC na nchi wanachama wa Afrika Mashariki wa EAC, kutokana na namna Serikali ilivyoamua kuusimamia.

SADC na AU wana upofu fulani wa kibinafsi ambapo wataunga mkono chochote kinachopingwa na mataifa ya magharibi na jumuia za kimataifa.

Na wanalojua ni kuunga mkono tu vipofu hawa. Hata Raisi katika nchi ya SADC akiua raia wake wote hutasikia kamwe wakitoa kauli kumlaani, wakisingizia ni mambo ya ndani ya nchi. Hizo zilikuwa enzi za kina Nyerere na Kaunda, sio hawa wa siku hizi.
 
Si mlisema taasisi za kimataifa zinasikiliza wapinzani huku mkiunda hash tags nyiingi mitandaoni ili mhurumiwe

Nilisema mimi? Quote hiyo post unayoifanyia reference. Kama ubongo wako una sehemu mbili kwamba kila unalosikia ni kutoka CCM au pinzani, muone daktari wa magonjwa ya akili.
 
View attachment 1179924
KURUGENZI ya Miundombinu na Huduma ya Sekretarieti ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) imesema inajivunia mradi wa kuzalisha umeme kwa maporomoko ya maji ya mto Ruji (Mwalimu Julius Nyerere) kutokana na manufaa yake kwa nchi wanachama.
Aidha, imeipongeza Serikali ya Tanzania inayoongozwa na Rais John Magufuli kwa kuwa mfano wa kuigwa katika utekelezaji wa miradi ya kisekta ya miundombinu ambayo pamoja na kuipaisha Tanzania kiuchumi, pia ina manufaa makubwa kwa nchi za SADC na Afrika.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Mkurugenzi wa Miundombinu na Huduma wa Sekretarieti ya SADC, Mapolao Mokoena alimpongeza Rais Magufuli kwa uongozi wake na kuhakikisha mradi huo unatekelezwa. Mokoena alisema hayo wakati akijibu maswali ya waandishi wa habari baada ya yeye pamoja na wakurugenzi wengine kuwasilisha mada kuelezea shughuli na malengo ya kurugenzi mbalimbali ndani ya sekretarieti ya SADC.
Miongoni mwa maswali hayo lilitaka kupata maoni yake juu ya mradi mkubwa wa kuzalisha umeme uliozinduliwa hivi karibuni Ruji, mkoani Pwani, nchini Tanzania na Rais Magufuli. “Tunajivunia huu mradi,” alisema na kuongeza kuwa mradi huo una manufaa si tu kwa nchi za SADC bali pia kwa nchi za Afrika Mashariki na Bara zima. Rais Magufuli alizindua mradi huo mkubwa wa uzalishaji umeme Julai mwaka huu, ukitarajiwa kuwezesha nchi kupata umeme wa kutosha.
Unatarajiwa kuzalisha megawati 2,000 za umeme na Ujenzi wa bwawa hilo unaofanywa na wakandarasi kutoka Misri unatarajiwa kugharimu dola za Marekani bilioni 2.9; takribani Sh trilioni 6.5. Awali, akiwasilisha mada kuhusu maendeleo ya miundombinu na huduma ndani ya SADC kwenye eneo la nishati, alisema Mpango Kazi wa Maendeleo ya Miundombinu (RIDMP) wa mwaka 2012-2027 unalenga kuhakikisha kunakuwa na usalama wa rasilimali ya nishati na uhakika wa upatikanaji wake kama injini ya kuinua uchumi.
Alitaja eneo muhimu linalopewa kipaumbele na kutazamwa kiuchumi zaidi katika nishati kuwa ni upatikanaji na ugunduzi wa gesi na mafuta katika nchi wanachama na namna nchi hizo zinavyotumia nishati hizo kupata uhakika wa umeme kwa matumizi ya nyumbani na viwandani.
KWA KWELI HUU MRADI NI MUHIMU SANA KWETU. SISI TUTATUMIA HUU UMEME WA KUFUA KWA MAJI NA HAO WA GESI WAWAUZIE NCHI ZA NJE HUO UMEME WAO WA BEI GHALI TUONE KAMA WATANUNUA. HONGERA TANZANIA IKIONGOZWA NA MAGHUFULI. TUTATOKA TU
 
Kujivunia kitu ambacho ndo kwanza kinaanza kujengwa aisee, na naona hawa nao wapo kisiasa tu
Amesifia uthubutu!!!

Pia uelewe kwamba pesa yote ya mradi ipo mfuko wa shati

Acheni siasa zitawazeesha mapema
 
Waafrica tangu lini wakapinga anachafanya mwenzao? wao matokeo sio ishu.

Kama ambavyo hawajawahi kumhoji raisi yeyote 'umeingiaje madarakani'.
 
Hawa SADC hawana agenda za mkutano wao, mradi hata haijafika mahali wameanza kuusifia, sasa sisi Praise team tufanye kazi gani.

Hebu wajitathimini
View attachment 1179838

Back
Top Bottom