Sababu zinazonifanya nisitazame Bongo movie tena

nanawoo

JF-Expert Member
Jan 2, 2015
1,302
1,263
1. Wachawi wanakamatwa na mgambo.
2. Majeruhi na maiti zinabebwa kwa mikono mitupu.
3. Jini anavuka barabara anaangalia kushoto na kulia anatizama usalama kwanza.
4. Risasi inachukua dakika kumfika mpigwaji.
5. Mtu yupo na demu wake super maket wanachukua nusu saa nzima wakati muvi ina saa moja na nusu.
6.Mtu akipigwa ngumi anaangallia pakuangukia kwa usalama wake.
7. Milio ya risasi kama unawasha njiti za kiberiti.
8. Kahaba lazima avute sigara.
9. Jambazi lazima livae koti refu na miwani meusi.
10. Mganga wa kienyeji lazima awe porini mchafu na anaongea kwa ukali.
11.Kwenye Subtitle mgeni anaitwa new people.
12. Hospitalini wapo wao tu.
13.Jambazi anavua viatu akivamia kwenye nyumba.
14.Mtanga na Serengo lazima wawe walinzi.
15.Jini lazima awe mwanamke.
16. JB anavaa shati moja kwenye muvi sita.
17. Tokeo linaoneshwa lilitokea mwaka 1977 halafu ukutani kuna picha ya raisi wa sasa Magu.
18. Familia ya kitajiri lazima waongee kizungu Dadi!" Mami!!.
19. Tajiri lazima amuoe maskini.
20. Gereza ni nyumba ya mtu yenye madirisha ya chuma.
21. Kila anaetoa habari za maisha yake ya nyuma lazima anyanyue uso juu.
22. Mapenzi yanaanza pale mwanamke anapoharibikiwa na gari alafu mwanamne anatokea kusaidia.
23. Mlinzi wa getini lazima awe hana akili vizuri.
24. Kitu pekee kinachovunjika ni glasi.
25. Movie inaanza mtoto mweusi kichwani kipipili cha nguvu, akiwa mkubwa ni mweupe na ana nywele za kiarabu.
No log off Bongo movie.
27. Dalili ya mimba ni kutapika tu...


Hiyo ndo Bongo movie.
 
Mtu aliyeuawa kwa risasi au kitu chenye ncha kaki anaonekana anapumua.
Mhusika anayejinyonga hawezi kuonekana mzima mzima akining'inia. Anaoneshwa nusu nusu.
 
Tumezichoka hizi hauna nyingine?
 
Mwenye daresalam yake anakuchora tu. Sema Mambo mengine kichefu chefu. Eti ktk mkoa wangu. Mkoa wako!!!!!?
 
Nyngne niliona eti jini kaangusha glasi akesma "ooh,my God" bongo muv bana
 
niliangalia muvi moja juzi kati puuuuuu, kuna watoto wawili eti wanamfanyia saplaiz uncle wao kuhusu mke wake kuwa na mwanaume mwingine ndani, wakamfunga kitambaa cheusi usoni, alafu na wale wengine waliokua chumbani nao wakafungwa vitambaa alafu wakaongozwa hadi sebuleni,

ile kufika sebuleni uncle wao akauliza tena kwa sauti nzito kabisa NIFUNGUE? wale wakamjibu hapana subiri kwanza, baadae kidogo walipokuja kufungua vitambaa eti wale wagoni ndio wakajifanya kushituka, inamaana hawakumsikia alipokua anauliza nifungue na watoto kumjibu hapana?

pale pale nikamwambia wife embu change hyo channel haraka, weka katuni
 
Hahahaha eti katunj
 
Wenzako wamejikita zaidi kutafuta mkate wa asubuhi kuliko ubora wa kitu.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…