Sababu za Msingi kwanini Bomba la mafuta Uganda lipite Bandari ya Tanga

Bilionea Asigwa

JF-Expert Member
Sep 21, 2011
16,515
28,487
Hongera sana Professor Muhongo, Dr. James Mataragio na timu yako kwa kulitetea taifa na nimepenyezewa ubuyu kuwa mambo sasa safi, Bomba ni confirmed linapita Tanga.

Miongoni mwa hoja mlizozijenga kwa mama Irene Muloni na msafara wake kutembelea bandari ya Tanga ya kwa nini wajenge bomba lao kupitia Tanzania na si Kenya ni hzi.

1. kina cha bandari ya Tanga kina urefu wa zaidi ya mita 40 wakati meli za mafuta zinahitaji mita 18 hivyo kuwa bandari salama zaidi kwa meli za mafuta. tofauti na Lamu ambapo kina chake ni kifupi mno, hivyo inabidi kuongeza kina kwa kuchimba zaidi.

2. Bandari la Lamu ina mawimbi makubwa mno, kutokana na kutokuwa na visiwa vya pembezoni mwake vinavyopakana nayo, upepo toka bahari za mbali unavuma moja kwa moja mpka bandarini, sio salama kwa meli ya mafuta ukilinganisha na bandari ya Tanga iliyoko katikati ya visiwa vya Pemba na Unguja hivyo haina mawimbi makubwa na kuwa salama zaidi kwa meli za mafuta ambazo huhitaji utulivu wa hali ya juu wakati wa kupakia shehena yake ya mafuta kwani huchukua siku nyingi sana kupakia mzigo na inahitaji utulivu sana.

3. Bandari ya Lamu iko mpakani na Somalia hivyo nirahisi kwa meli za mafuta kutekwa na maharamia ya kisomali wakati Tanga ipo katikati ya Zanzibar na Bara hivyo kuna doria za jeshi la Tanzania na vikosi vya Zanzibar hivyo sio rahisi kuvamiwa na maharamia.

4. Tanga tayari kuna miundombinu ya mafuta tofauti na Lamu inabidi ijengwe. Pia vifaa vya ujenzi vitashuka Tanga na kwenda site moja kwa moja ,tofauti na Kenya vifaa itabidi viteremshwe mombasa na kusombwa kwa maroli kwenda site.

5. Tanzania imetoa ofa ya kutenga bandari ya Tanga kuwa mahususi kwa mizigo ya Uganda na tayari kuna miundombinu ya reli na barabara ambapo Lamu hakuna reli wala barabara ya kwenda huko.

Maelezo haya yaliwaridhisha na Irene Musoni na team yake wameahidi kutuma wataalamu baada ya wiki mbili kukagua njia zitakazotumiwa kupita bomba la mafuta.

“Nimeona taarifa ya mradi iliyowasilishwa hapa na wataalamu na pia nimepata fursa ya kutembelea Bandari ya Tanga na kimsingi nimeridhika na wiki ijayo nitatuma timu ya wataalamu ili kuja kufanya uhakiki wa njia mradi utakapojengwa na mahali ujenzi wa matangi ya kuhifadhia mafuta yatakapokuwepo ili kushauri kabla ya utekelezaji rasmi kuanza,”
alisema Muloni.

Naona katoa muda wa kwenda kumueleza Uhuru kuwa dili limebuma.

>>Much Respect kwako Mukulu anko Magu kwa "kichwa ngumu" hakuna ile mambo ya kuwa soft soft, ume prove kwa watanzania kuwa wewe ni Ngosha kweli
>>Much respect kwako Silent Killer Professor Muhongo kwa umafia kwa kimya kimya ulioufanya, umelibeba taifa.
>>Much respect kwako balozi Mahiga kwa Economic Diplomacy na Intelligence iliyotukuka.
>>Much Repect kwako Mataragio kwa agressiveness yako kuu kwa hawa manyang'au.
NB:

Nachowaomba serikali yangu sikivu ni kuona namna ya ku-mjoin South Sudan katika bandari ya Tanga awe na ka-portion kake pale maana itamuhakikishia fursa ya kupunguza hustling anazopata kwa sasa, hasa ukizingatia Mkenya hanaga jema kwa mtu zaidi ya kuangalia maslahi yake.
Lakini pia mpige hatua mbele zaidi ya kuangalia namna ya kumuamsha Mganda katika usingizi mzito alio nao wa namna ya kuichangamkia South Sudan ili iwe partner wake kiuchumi kwa kupitisha bomba lake la mafuta Uganda kuja Tanga maana hio itamuongezea mapato Uganda pia tofauti akizubaa bomba likapitia Kenya, Uganda hatapata hata mia
 
Swala sio technical analysis kwa nin bomba lipite kwetu,issue ni economic benefit gani tutapata kama nchi? hii issue imebebewa bango sana sasa cjui ni kusahaulisha watu mambo ya zanzibar au kuna ukweli wowote.
 
nawapongeza sana ndug zangu watanzania, katika hii issue tumetanguliza TAIFA mbele, tumeweka tofauti pembeni. huu mradi una maslai makubwa sana kwa taifa letu. tuendelee kulipigania taifa letu. tunaimani viongozi hawatatuangusha. tukimalizana na UG tukomae na S.SUDAN nae aje TANGA. ni mwendo wa kukomaa hata majirani wakinuna
 
Swala sio technical analysis kwa nin bomba lipite kwetu,issue ni economic benefit gani tutapata kama nchi? hii issue imebebewa bango sana sasa cjui ni kusahaulisha watu mambo ya zanzibar au kuna ukweli wowote.

yaaani wewe unawaza siasa siasa siasa siasa, ujui kuna kazi baada ya siasa, kweli watanzania tuna njia ndefu hadi tufike, hivi mtu kama huyu, hajui umuhimu hata mmoja wa ilo bomba jaman??
 
Swala sio technical analysis kwa nin bomba lipite kwetu,issue ni economic benefit gani tutapata kama nchi? hii issue imebebewa bango sana sasa cjui ni kusahaulisha watu mambo ya zanzibar au kuna ukweli wowote.
Mkuu inabidi uelewe kuwa tozo ya kupitisha pipa moja kwa katika ardhi ya nchi nyingine ni $14 na Uganda inapitisha mapipa 200,000 kwa siku maana yake kwa mwaka serikali inaingiza zaidi ya Trillioni 2, na hio ni fedha ya kigeni kwa haraka haraka ni US Dollars.
Pia ukumbuke pato la ndani kwa mwaka kwa serikali kwa sasa ni almost Trillioni 4 maana yake pato la ndani litakua limeongezeka kwa 50%, sasa hapo huoni hio faida??

Kumbuka pia kama tukipwa dollar hizo maana yake shillingi ya Tanzania dhidi ya Dollar ya mmarekani itaimarika sana na hivyo kutupa advantage katika maununuzi ya nje.

Kiuchumi hii kitu ina faida sana.
 
yaaani wewe unawaza siasa siasa siasa siasa, ujui kuna kazi baada ya siasa, kweli watanzania tuna njia ndefu hadi tufike, hivi mtu kama huyu, hajui umuhimu hata mmoja wa ilo bomba jaman??
Ndo uniambie ww sasa, nachojua mm Uganda ni land locked kwa vyovyote lazima atumie Kenya au Tanzania kufanya export zake, usiniambie vitu vidogo vidogo nataka nijue faida kubwa na risk za sis kukubali kufacilitate potential export za Uganda
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…