Nsanzagee
JF-Expert Member
- Jun 28, 2023
- 2,209
- 4,769
Kuna wakati viongozi wa CCM hujaribu kuwatukana watanzania matusi ya rejareja
Ni nani atakayeamini hiki wasemacho kina Kinana?
Jambo la mapato kuongezeka, ni kweli linaendana na uhalisia?
Mimi nasema hivi, halina uhalisia kwa sababu nyingi tu,
Moja ya sababu ni pamoja na kuwepo sababu za kwamba, bandari zetu hatuwezi kuziendesha kwa sababu serikali imeshindwa kuzuia wezi pale bandarini, mapato yanapotea sana na ndiyo sababu ya kupewa mwekezaji! Sababu hii iwapo ndiyo iliyopelekea kubinafisishwa bandari zetu, basi, hii ndiyo inayoniaminisha kwamba, Mapato yetu yangelikuwa juuu sana ukilinganisha na hiki wanachojitapa Viongozi wa CCM
Kwa sababu hiyo hiyo moja tu, inatosha kabisa kutuaminisha kwamba, mapato yetu iwapo yangelisimamiwa kimagufuli, tusingelikuwa na mapato hayo tu wayasemao viongozi hawa wazembe
Ukiondoa la Bandari, Serikali inasimamia mambo mangapi ambayo nako kunaupigaji mwingi?
Mambo ya upigaji, ndiyo hayo Magufuli alikuwa akilala nao mbele wezi hao na ambao sasa wanatetewa na CCM
Kumzungumzia Magufuli eti alikuwa ni mporaji wa kodi, ni kufabaisha udhaifu uliopo sasa
Ripoti za CAG hazishughurikiwi, uzembe na wizi ndio umetamalaki
Utamwambia nini mtanzania mwenye akili timamu kumhusu JPM?
Tokea JPM ameondoka, ni kipi kikubwa sana kilichofanyika na ama kinachofanyika ambacho Watanzania wanaona ni juhudi binafsi na ama ujasiri wa kipekee kutoka kwa awamu hii?
Je, ni bandari na DPW? Je, ni wamaasai na Ngorongoro? Au jambo lenye ukakasi kuhusu Bima za Afya
Ni nini hasa zaidi tu ya kushukuru ujasiri wa alioufanya hayati Magufuli kuanzisha miradi mkibwa na yenye kuleta heshima katika nchi yetu?
JPM hakupora mtu yeyoyote zaidi ya kuwanyang'anya mafisadi pesa wizi!
Hata hivyo tunayonafasi bado ya kufanya makubwa zaidi na tukajivunia nayo, shida ni kwamba, hatuwezi kufikia matarajio hayo kwa sababu hata waliowekwa kwenye kusimamia masilahi ya nchi, wengi wao hawana uthubutu wa kukemea mafisadi kwa sababu hata wao ni mafisadi